Aunty Molly Afunguka Kuhusiana na Uhusiano Wake na Harmonize

Aunty Molly Afunguka Kuhusiana na Uhusiano Wake na Harmonize

Mrembo kutoka Afrika Kusini, Aunty Molly, amevunja ukimya na kufafanua uvumi uliokuwa ukisambaa mitandaoni kuhusu uhusiano wake na staa wa Bongo Fleva, Harmonize. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aunty Molly amejibu shabiki aliyeuliza nafasi ya Harmonize maishani mwake, ambapo ameeleza wazi kuwa Bosi huyo wa Konde Gang si mpenzi wake kama inavyodaiwa, bali ni mjomba wake kwa upande wa baba. Ufafanuzi wa Aunty Molly umekuja wakati ambapo mashabiki wengi walikuwa wakimhusisha na Harmonize, wakidhani ni uhusiano mpya wa kimapenzi unaochipuka, lakini ukweli umebainika kuwa ni wa kifamilia. Kwa muda mrefu sasa, Harmonize ambaye pia ni bosi wa lebo ya Konde Gang, amekuwa akihusishwa na tetesi mbalimbali za kimapenzi, hasa kutokana na ukaribu wake na wanawake wenye umbo kubwa, hususan makalio makubwa. Hali hii imekuwa ikizua mjadala mkubwa mitandaoni kila mara jina lake linapojitokeza.

Read More
 Lady Jaydee Atoa Somo Kwa Mashabiki Kuhusu Misaada

Lady Jaydee Atoa Somo Kwa Mashabiki Kuhusu Misaada

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mahitaji na maombi ya mashabiki, akiwahimiza wasitegemee msaada wa wengine kwa sababu watu wana malengo na vipaumbele tofauti. Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Lady Jaydee amesema si wajibu wa mtu mwingine kutatua shida za kila mtu, na kwamba hata yeye mwenyewe hana wajibu wa kushughulikia matatizo ya watu wote. Amewaomba mashabiki wakome kumwelezea matatizo yao kwa matarajio ya msaada mara moja, kwani kila mtu ana mipango yake na uwezo wake. Msanii huyo amewahimiza wale wanaokabiliwa na matatizo ya kibinafsi kutafuta msaada kwa viongozi wa dini, akitoa mfano wa mapadri ambao kwa imani yake wanaweza kusikiliza kwa faragha na kutoa ushauri stahiki bila kutangaza siri. Lady Jaydee pia amesisitiza umuhimu wa kujitegemea na kujenga mbinu za kutatua matatizo binafsi, akisema kujitegemea kunawasaidia watu kuwa na uhakika wa maisha yao na kuepuka utegemezi usiofaa. Kwa Lady Jaydee, ujumbe huo ni sehemu ya mafunzo ya maisha yanayomwita kila mtu kuchukua uwajibikaji wa hali zake na kutambua kuwa wema wa mtu mwingine hawezi kuwa suluhisho la kila tatizo.

Read More
 Mbosso Adai Nusra Atoe Uhai Akiwafurahisha Mashabiki Simba SC

Mbosso Adai Nusra Atoe Uhai Akiwafurahisha Mashabiki Simba SC

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, amefunguka kuhusu namna alivyoweka nguvu kubwa kuhakikisha onyesho lake kwenye Simba Day linakuwa la kipekee, akieleza kuwa nusra ajitoe uhai wake ili kuwafurahisha mashabiki wa Simba Sports Club. Kupitia Instagram, Mbosso amesema alijiandaa kwa moyo wake wote na kuweka nguvu, muda na rasilimali nyingi kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Amebainisha kuwa mapenzi yake kwa Simba SC na mashabiki wake ndiyo yaliyomsukuma kufanya maandalizi ya hali ya juu, akisisitiza kuwa alijitolea zaidi ya kawaida ili burudani iwe ya kukumbukwa. Licha ya mafanikio makubwa ya perfomance yake, msanii huyo pia amewaomba mashabiki na viongozi wa Simba SC msamaha endapo kulikuwa na mapungufu yoyote katika utendaji wake wa Kazi, akisema yeye ni mwanadamu na hawezi kufanya kila kitu kwa ukamilifu. Simba Day hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuzindua msimu mpya wa klabu hiyo yenye mashabiki wengi, na mwaka huu Mbosso alipewa nafasi ya kuwa headliner, nafasi ambayo amesema itaendelea kubaki kuwa kumbukumbu muhimu katika maisha yake ya muziki.

Read More
 Willy Paul Afunguka Kujihusisha na Kiki Kabla ya Kuachia Nyimbo

Willy Paul Afunguka Kujihusisha na Kiki Kabla ya Kuachia Nyimbo

Msanii wa muziki wa Kenya, Willy Paul, amefunguka hadharani baada ya kukosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kujihusisha na kiki au kuvutia umaarufu kabla ya kuachia kazi zake mpya. Kupitia Insta Story, Willy Paul ameeleza kuwa tabia hiyo ya kudhaniwa kuwa anafuata umaarufu ni sehemu ya mitazamo potofu ya baadhi ya mashabiki, na kwamba lengo lake ni kushirikiana na mashabiki wake na kuhakikisha nyimbo zake zinawafikia watu wengi. Mkali huyo wa Toto, ameongeza kuwa kutumia mitandao ya kijamii kuendesha mijadala au kuunganisha mashabiki siyo kutafuta kiki au clout bali ni mbinu ya kisasa ya kukuza muziki. Aidha, msanii huyo amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijitahidi kuunda uhusiano wa karibu na wapenzi wa muziki wake, huku akisisitiza kuwa kila hatua ya matangazo ya nyimbo yake ni kwa lengo la kushirikisha mashabiki na si kwa kujihusisha na umaarufu bandia. Kauli yake imekuja mara baada ya kushtumiwa na VJ Patelo kwa kukaidi makubaliano ya malipo baada ya video shoot, madai yaliyowafanya mashabiki kuhisi alitengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni kabla ya kuachia wimbo wake mpya Ijumaa wiki hii.

Read More
 Mwimbaji wa Kenya Sofiya Nzau Ashirikishwa kwenye Soundtrack ya EA Sports FC 2026

Mwimbaji wa Kenya Sofiya Nzau Ashirikishwa kwenye Soundtrack ya EA Sports FC 2026

Mwimbaji maarufu wa Kenya, Sofiya Nzau, amefanikisha hatua kubwa katika taaluma yake ya muziki baada ya kuhusishwa kwenye soundtrack rasmi ya mchezo wa video wa EA Sports FC 2026. Kampuni ya EA Sports ni kampuni kubwa ya michezo ya video inayojulikana kwa kutengeneza michezo maarufu kama FIFA, NBA, na Madden NFL. Sasa, wimbo wa Sofiya utasikika na mamilioni ya watu duniani kote wanapokuwa wakifuatilia michezo hiyo. Kujumuishwa kwa Sofiya Nzau kwenye soundtrack ya EA Sports FC 2026 inaonyesha jinsi wasanii wa Afrika wanavyopata fursa kubwa kwenye majukwaa ya kimataifa ya michezo na burudani. Mashabiki na wapenzi wa muziki sasa wanaweza kufurahia kazi yake huku wakiwa sehemu ya mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote. Hii ni hatua muhimu kwa Sofiya, ikimshirikisha katika fursa zaidi za kimataifa na kuongeza umaarufu wake katika sekta ya muziki na michezo ya video.

Read More
 John Segawa Amshauri Chameleone Kuachana na Bifu na Alien Skin

John Segawa Amshauri Chameleone Kuachana na Bifu na Alien Skin

Mkurugenzi wa filamu nchini Uganda, John Segawa, ameibua mjadala baada ya kutoa maoni yake kuhusu bifu linaloendelea kati ya nyota wa muziki Jose Chameleone na msanii chipukizi mwenye ushawishi mkubwa, Alien Skin. Akizungumza kuhusu mvutano huo, Segawa amesema wazi kuwa Chameleone, kiongozi wa Leone Island, hana nafasi ya kushindana na Alien Skin kwa sababu ya hali yake kiafya na tofauti ya kizazi. Kwa mujibu wa Segawa, Chameleone ni mgonjwa, hafahamu mienendo ya kisasa ya muziki, na kujaribu kuingia katika mapambano na kundi la Fangone Forest kutamletea madhara makubwa. Amefafanua kuwa Chameleone hana nguvu wala nafasi ya kupigana na Alien Skin kwa kuwa vijana ndio wanaoongoza burudani kwa sasa. Aidha, amesisitiza kuwa msanii huyo mkongwe akijaribu kuendeleza bifu hilo, ataishia kupata mateso zaidi badala ya ushindi. Segawa pia ameeleza kuwa bifu hilo linamnufaisha zaidi Alien Skin, kwa sababu msanii huyo bado ni kijana mwenye nguvu na ana miaka mingi ya kufanya muziki mbele yake. Ameongeza kuwa katika hali yoyote ya mvutano, Fangone Forest ingepata ushindi dhidi ya Chameleone kwa sababu ya nafasi yao kubwa katika mwelekeo wa muziki wa sasa.

Read More
 YouTube Yavunja Rekodi ya Watazamaji NFL Opening Night

YouTube Yavunja Rekodi ya Watazamaji NFL Opening Night

YouTube imeandika historia mpya katika ulimwengu wa matangazo ya moja kwa moja ya michezo baada ya kuvunja rekodi kupitia matangazo yake ya mchezo wa ufunguzi wa msimu wa NFL (National Football League) maarufu kama NFL Opening Night. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zaidi ya watazamaji milioni 17.3 walitazama kwa kila dakika ya wastani, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa hapo awali kwa jukwaa la kidijitali. Hili limeiweka YouTube katika nafasi ya juu kama moja ya majukwaa makubwa ya kurusha matangazo ya michezo moja kwa moja, na kuwapa changamoto majukwaa ya jadi ya televisheni. Mchezo huo wa ufunguzi, uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki wa mpira wa miguu wa Marekani, ulionyesha ushindani mkubwa na burudani ya hali ya juu jambo lililochangia kuvutia idadi kubwa ya watazamaji kutoka pande zote za dunia. Takwimu hizi zimeonesha mabadiliko makubwa ya tabia ya watazamaji, ambapo wengi wao sasa wanategemea majukwaa ya kidijitali kama YouTube badala ya televisheni za kawaida. Hatua hii pia ni mafanikio makubwa kwa YouTube TV, ambayo imewekeza kwa kiasi kikubwa katika haki za matangazo ya michezo mbalimbali maarufu. Kwa kuzingatia mafanikio haya, wataalamu wa tasnia ya habari na burudani wanatarajia kuona ongezeko kubwa la uwekezaji wa majukwaa ya kidijitali katika matangazo ya moja kwa moja ya michezo, huku teknolojia ikiendelea kuleta mapinduzi katika namna ambavyo watu hutazama na kufurahia michezo duniani kote. Kwa sasa, YouTube imeonesha kuwa si tu jukwaa la video, bali pia mchezaji mkubwa katika mustakabali wa utangazaji wa michezo ya moja kwa moja.

Read More
 Timu ya Kenya Police Bullets Yabanduliwa katika mashindano ya CECAFA

Timu ya Kenya Police Bullets Yabanduliwa katika mashindano ya CECAFA

Timu ya Kenya Police Bullets imebanduliwa katika mashindano ya CECAFA kuwanai kufuzu kwa fainali za kombe la klabu bingwa barani Afrika miongoni mwa akina dada baada ya kulazwa mabao 4-2 na Jeshi La Kujenga Taifa, JKT Queens ya Tanzania, kupitia kwa mikwaju ya penalty wakati wa mchuano wa nusu fainali ulioandaliwa katika uwanja wa Moi Kasarani. Timu hizo mbili zilitoka sare bao moja kwa moja katika muda wa kawaida na wa ziada na mikiki ya penalty ilitumiwa ili kumuamua mshindi.JKT ilifunga mikwaju yake ya penalty kupitia kwa Winfrida Mzoefu, Aaliyah Salu, Melissa Minja na Bahera Crista ilhali Police ilipoteza mikwaju yake miwili iliyopigwa na Emily Moranga na Leah Andiema. Kufuati ushindi huo JKT Queens sasa itamenyana na Rayon Sports ya Rwanda katika fainali ya michuano hiyo. Rayon iliinyuka Kampala Queens mabao 4-3 kupitia kwa mikwaju ya penalty katika mchuano mwingine wa nusu fainali ulioandaliwa jumapili. Fainali ya mashindano hayo imepangwa kuandaliwa tarehe 16 mwezi huu huku mshindi akijinyakulia tikiti ya kuliakilisha eneo la CECAFA katika mashindano kuwania ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika yatakayoandaliwa mwezi Novemba.

Read More
 Mashabiki Tanzania Wakosoa Muziki wa Zuchu kwa Kudai Ni wa Kitoto

Mashabiki Tanzania Wakosoa Muziki wa Zuchu kwa Kudai Ni wa Kitoto

Baadhi ya mashabiki wa muziki nchini Tanzania wameeleza kutoridhishwa kwao na muziki wa staa wa Bongo Fleva, Zuchu, wakidai nyimbo zake zinaonekana kuwa za kitoto na hazina mvuto wa kipekee kwa watu wazima. Kwenye maoni yaliyosambaa mitandaoni, mashabiki hao wamesema wanapata ugumu kusikiliza nyimbo zake kwa muda mrefu kwani sauti na mitindo yake inawafanya kuhisi kwamba muziki huo unalenga zaidi watoto kuliko hadhira pana ya muziki wa kizazi kipya. Hata hivyo, upande mwingine wa mashabiki wake umejitokeza kumtetea, wakisisitiza kuwa Zuchu ni msanii mwenye kipaji cha kipekee na nyimbo zake zimekuwa zikifanya vizuri si tu Tanzania, bali pia kwenye majukwaa ya kimataifa. Wanasema sauti yake ya kipekee ndiyo inamtofautisha na wasanii wengine, na ndicho kilichompa nafasi ya kufanikisha mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi. Zuchu, ambaye ni msanii wa lebo ya WCB Wasafi, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na nyimbo kama “Sukari”, “Cheche” na “Kwikwi”. Pamoja na ukosoaji huu, nyimbo zake bado zinaendelea kupata mamilioni ya watazamaji na wasikilizaji kwenye majukwaa ya kidijitali, jambo linaloonyesha kuwa bado ana hadhira kubwa na yenye ushawishi.

Read More
 Rapcha Amshutumu Khaligraph Jones kwa Kujumuisha Polisi Kwenye Ugomvi Wao

Rapcha Amshutumu Khaligraph Jones kwa Kujumuisha Polisi Kwenye Ugomvi Wao

Bifu kati ya mtangazaji wa Kenya, Rapcha the Sayantist, na rapa nyota, Khaligraph Jones, limechukua mkondo mpya baada ya Rapcha kudai kuwa Khaligraph aliwahusisha polisi katika mgogoro wao. Mzozo huu ulianza baada ya Rapcha, kupitia podcast yake, kumtaja Khaligraph kama msanii feki, akipinga lafudhi yake, asili yake ya Kayole, mtindo wa rap na uhalisia wa kazi zake za muziki. Kauli hizo zilichochea mjadala mkali mitandaoni na kugawanya mashabiki wa hip hop Afrika Mashariki. Khaligraph alipuuza shutuma hizo akizihusisha na mbinu za kutafuta kiki, na akamtangaza Rapcha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa mtindo wa kebehi, akionesha kuwa hatambui hoja zilizotolewa. Hata hivyo, mambo yalichukua sura mpya baada ya Rapcha kudai kuwa Khaligraph alihusisha polisi ili kuzima bifu hilo. Kwa mtangazaji huyo, hatua ya kupeleka mgogoro wa muziki kwa vyombo vya usalama ilikuwa ni ishara ya udhaifu na kutojiamini katika kukabiliana na changamoto za kisanaa. Alieleza kuwa tabia ya aina hiyo inaua roho ya hip hop, kwa sababu badala ya kujibu hoja kwa ubunifu au kuendeleza mashindano ya kisanaa, wasanii wakubwa wanatumia nguvu zao kuwakandamiza wanaowakosoa. Mashabiki wameendelea kutofautiana, baadhi wakimtetea Khaligraph kama msanii mwenye hadhi ya kimataifa asiye na ulazima wa kujibu kila ukosoaji, huku wengine wakimpongeza Rapcha kwa uthubutu na kuibua mijadala mipya katika tasnia ya muziki. Mpaka sasa, Khaligraph hajajibu moja kwa moja madai ya kuhusisha polisi. Wachambuzi wa burudani wanasema bifu hili linaweza kubaki kama mjadala wa kawaida wa mitandaoni au kugeuka kuwa mvutano mkubwa unaoweza kuathiri taswira ya hip hop Afrika Mashariki.

Read More
 Video ya “Kumbaba” Yaondolewa YouTube kwa Sababu za Hakimiliki

Video ya “Kumbaba” Yaondolewa YouTube kwa Sababu za Hakimiliki

Video ya wimbo maarufu “Kumbaba” wa kundi la rap kutoka Kenya, Wakadinali, imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia madai ya ukiukwaji wa hakimiliki. Hatua hiyo imezua mazungumzo makubwa miongoni mwa mashabiki wa kundi hilo, ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuonyesha mshangao na kutoridhishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, video hiyo ambayo ilipata umaarufu mkubwa kutokana na mashairi yake ya kipekee na ubunifu wa Wakadinali, ilishutumiwa kwa kutumia vipengele vinavyodaiwa kuwa na hakimiliki bila idhini. Hata hivyo, haijabainika wazi ni ni nani au taasisi ipi iliyowasilisha malalamiko hayo kwa YouTube. Mashabiki wameeleza masikitiko yao, wengi wakisisitiza kuwa “Kumbaba” ilikuwa kati ya kazi bora zaidi za Wakadinali na mchango mkubwa katika kuendeleza hip hop ya mitaani nchini. Baadhi wamehoji kwa nini masuala ya hakimiliki hayakutatuliwa kabla ya video hiyo kuondolewa, wakihofia huenda hatua hiyo ikapunguza kasi ya ukuaji wa kazi za wasanii wa hapa nyumbani. Wakadinali, ambao wanajulikana kwa midundo yao mizito na mashairi yanayochora picha halisi ya maisha ya mitaani, bado hawajatoa kauli rasmi kuhusu sakata hilo. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo video ya “Kumbaba” itarejeshwa mtandaoni au iwapo kundi hilo litachukua hatua nyingine ya kisheria au kiubunifu ili kulinda kazi zao.

Read More
 Daddy Owen: “Ni Rahisi Kukubali Kifo Kuliko Talaka”

Daddy Owen: “Ni Rahisi Kukubali Kifo Kuliko Talaka”

Msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen ameibua mjadala baada ya kutoa kauli yenye kugusa hisia kuhusu ndoa na changamoto za talaka. Akizungumza kwenye mahojiano, msanii huyo amesema kuwa kwa mtazamo wake, ni rahisi zaidi mtu kukubali kifo cha mpendwa wake kuliko kukabiliana na talaka, hasa pale ambapo kuna watoto. Kwa mujibu wa Daddy Owen, talaka huacha jeraha refu kwa sababu yule uliyeachana naye ataendelea kuwepo kwenye maisha yako kupitia majukumu ya malezi. Msanii huyo ameongeza kuwa hali huwa ngumu zaidi endapo bado kuna hisia za kimapenzi kwa mtu huyo, jambo linalomfanya aliyeachika kupata wakati mgumu zaidi kisaikolojia na kihisia. Kauli hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti miongoni mwa mashabiki na wafuasi wake. Wapo waliomuunga mkono wakisema imani na uzoefu wake unaonyesha uhalisia wa maisha ya kifamilia, huku wengine wakihisi kuwa kulinganisha kifo na talaka ni jambo zito na tata. Daddy Owen amekuwa wazi mara kadhaa kuhusu changamoto za maisha yake ya kifamilia na imani yake katika dini, na mara nyingi hutumia hadithi zake binafsi kutoa mafunzo kwa jamii.

Read More