Gloria Ntazola Azua Gumzo kwa Kauli Kuhusu Ujauzito

Gloria Ntazola Azua Gumzo kwa Kauli Kuhusu Ujauzito

Socialite Gloria Ntazola ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kutoa kauli tata kuhusu suala la ujauzito. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Gloria alieleza wazi kuwa iwapo atapata mimba kwa sasa, ataichukua hatua ya kuitoa kwa sababu hana mpango wa kuzaa kwa wakati huu. Alisema hana mpango wa kulea mtoto kwa sasa na hakusita kusisitiza msimamo wake, akiongeza kuwa hata kejeli za watu haziwezi kumbadilisha maamuzi. Kauli hiyo imeibua hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake, baadhi wakimtuhumu kwa kupuuza thamani ya maisha, huku wengine wakimtetea kwa kusema kila mtu ana haki ya kuchagua mustakabali wa maisha yake. Hii si mara ya kwanza Gloria Ntazola kuzua mjadala mtandaoni kupitia kauli zake zenye utata. Wengi wanamfahamu kwa mtindo wake wa maisha wa kifahari na tabia ya kuzungumza kwa uwazi bila kujali maneno ya wakosoaji. Kauli yake ya sasa imeendelea kugawanya mitazamo ya mashabiki, huku ikitarajiwa kuibua mjadala mpana zaidi kuhusu maadili, uhuru wa wanawake katika kufanya maamuzi ya uzazi, na nafasi ya mitazamo ya kijamii kwenye maisha binafsi.

Read More
 Mashabiki Wataka Zuchu Atumbuize Kombe la Dunia 2026

Mashabiki Wataka Zuchu Atumbuize Kombe la Dunia 2026

Mashabiki wa muziki Afrika Mashariki wameonyesha shauku kubwa ya kutaka msanii wa WCB Zuchu kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026, baada ya kuandika historia usiku wa kuamkia leo katika Siku ya Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Katika onyesho hilo lililohudhuriwa na zaidi ya mashabiki elfu 60, Zuchu alidhihirisha ubunifu wa kimataifa kwa mtindo wa kipekee wa kuingia jukwaani. Msanii huyo alifika uwanjani ndani ya chombo kilichofanana na ua kubwa, ambacho baadaye kilifunguka taratibu kama ua linalochanua, na Zuchu akaibuka kutoka ndani yake huku akiibua shamrashamra za burudani. Mbali na hilo, aliwashangaza mashabiki kwa kuingia na kundi kubwa la madansa zaidi ya 200, hali iliyoongeza hamasa na kuifanya show yake kuzungumziwa kote mitandaoni. Zuchu alisema kuwa kiwango cha ubunifu kilichoonyeshwa hakijawahi kutokea kwenye historia ya shoo kubwa za uwanjani Tanzania. Hali hiyo imezua mjadala mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa hatua kubwa ya kuvuka mipaka ya burudani ya ndani na kuonyesha kwamba wasanii wa Afrika Mashariki wanaweza kushindana kimataifa. Baadhi ya mashabiki wameenda mbali zaidi wakimtaka Zuchu aorodheshwe miongoni mwa wasanii watakaopamba ufunguzi wa FIFA World Cup 2026, wakisema ubunifu na hadhi yake sasa inatosha kushindana na wakali wa dunia.

Read More
 Baunsa wa Alien Skin Ashushiwa Kichapo Katika Bifu na Kambi ya Chameleone

Baunsa wa Alien Skin Ashushiwa Kichapo Katika Bifu na Kambi ya Chameleone

Bifu kati ya msanii mkongwe Jose Chameleone na msanii mtukutu Alien Skin limechukua mwelekeo mpya baada ya mmoja wa walinzi wa Alien Skin, aitwaye Punisher Pro Max, kudaiwa kushushiwa kichapo cha mbwa na wanachama wa Leone Island usiku wa Alhamisi. Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea kufuatia mfululizo wa vitisho na matusi kati ya kambi ya Chameleone na ile ya Fangone Forest inayoongozwa na Alien Skin. Baunsa huyo anadaiwa kuwa katika mstari wa mbele kumtetea bosi wake, hali iliyochochea uhasama na kusababisha mashambulizi hayo. Video zilizozagaa mitandaoni zilimuonyesha Chameleone akionya vikali kambi ya Alien Skin, akisisitiza kuwa atawafundisha nidhamu kwa nguvu ikiwa wataendelea kumvunjia heshima. Kwa upande wake, Alien Skin alijibu vitisho hivyo kwa msimamo mkali, akisisitiza kuwa haogopi mapambano na yupo tayari kukabiliana na Chameleone pamoja na ndugu zake Pallaso na Weasel Manizo. Kichapo cha baunsa huyo kimeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, baadhi wakionya kuwa bifu hili linaweza kuathiri taswira ya muziki wa Uganda na hata kupelekea vurugu zaidi endapo pande zote mbili hazitatuliza hasira.

Read More
 Stevo Simple Boy Ajibu Wanaodai Anatumia Magari Kutafuta Umaarufu

Stevo Simple Boy Ajibu Wanaodai Anatumia Magari Kutafuta Umaarufu

Msanii Stevo Simple Boy amenyosha maelezo kuhusu umiliki wa gari aina ya Nissan March aliloinunua hivi karibuni. Hii ni baada ya walimwengu kutilia shaka uhalali wake na kuhoji kwamba msanii huyo amekuwa akitumia magari kutafuta kiki mtandaoni ilhali sio mmiliki halisi. Kupitia Insta Story yake, Stevo amekanusha kutumia magari kutafuta umaarufu, akisisitiza kuwa safari yake ya maisha inachukua mwelekeo mpya. Amewataka mashabiki waamini maendeleo yake kwani ununuzi wa gari hilo ni sehemu ya mafanikio anayojivunia licha ya changamoto nyingi alizopitia. Wiki hii, mjadala uliibuka mitandaoni baada ya Stevo kutangaza umiliki wa gari jipya, mashabiki wakibaki na maswali kuhusu ni magari mangapi anamiliki. Wengine walidai kuwa Nissan March ni gari lake la tatu, wakikumbusha mahojiano ya awali ambapo msanii huyo alikiri baadhi ya magari aliyopiga picha nayo yalikuwa ya kutumia kwa clout pekee.

Read More
 Patello Afunguka Kuhusu Video ya Mkewe Dee Akimpiga Kofi

Patello Afunguka Kuhusu Video ya Mkewe Dee Akimpiga Kofi

Msanii wa muziki kutoka Kenya VJ Patello amevunja ukimya baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikimuonyesha akipigwa kofi na mkewe, Dee, tukio ambalo lilizua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki. Akipiga stori na 2Mbili, Patello ameeleza kuwa kilichoshuhudiwa kwenye video hakikuwa ugomvi, bali ni tukio lililotokea wakati hakuwa na hamasa ya kutumbuiza. Amesema mkewe alikuwa akijaribu kumtia moyo ili achangamke na kuendeleza burudani kwa mashabiki. Hata hivyo, Patello amesisitiza kuwa hana tatizo na mkewe na kwamba wawili hao wanaendelea vizuri, akiwataka mashabiki wasichukulie video hiyo kwa mtazamo hasi. Kauli hiyo imeibua mitazamo tofauti miongoni mwa mashabiki. Baadhi wanamtetea Dee wakisema alifanya hivyo kwa nia ya kumtia moyo mumewe, huku wengine wakihisi kitendo hicho kilikuwa cha kudhalilisha msanii huyo mbele ya mashabiki wake.

Read More
 DJ Shiti Atangazwa Balozi Mpya wa Unga Farisi Premium

DJ Shiti Atangazwa Balozi Mpya wa Unga Farisi Premium

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, DJ Shiti, ametangazwa rasmi kama balozi mpya wa Unga Farisi Premium. Hatua hii inaashiria mafanikio makubwa kwa msanii huyo ambaye amejipatia umaarufu kupitia vichekesho vyake vinavyovutia mamilioni ya mashabiki. Kwa mujibu wa kampuni ya Farisi, DJ Shiti ameteuliwa kutokana na ushawishi wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na uwezo wake wa kuwasiliana na wafuasi kutoka tabaka mbalimbali za kijamii. Kupitia nafasi hiyo, ataongoza kampeni mbalimbali za kutangaza na kusambaza chapa hiyo ya unga sokoni. Tangazo hili limepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake mtandaoni, wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo mpya inayoongeza sura ya wasanii kuhusishwa katika sekta ya kibiashara. Hatua ya DJ Shiti kuingia kwenye ubalozi huu inatajwa kama ishara ya jinsi sanaa na biashara zinavyozidi kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.

Read More
 Betty Kyallo Kuongoza Timu ya Kenya Kutangaza Utalii wa China Mitandaoni

Betty Kyallo Kuongoza Timu ya Kenya Kutangaza Utalii wa China Mitandaoni

Mwanahabari maarufu Betty Kyallo pamoja na wachekeshaji Mulamwah, Terence Creative na MC Jessy, wamechaguliwa kushiriki katika ziara maalum ya kutembelea majimbo ya Hunan na Fujian nchini China kuanzia Septemba 15 hadi 23. Ziara hiyo imetangazwa rasmi na Ubalozi wa China nchini Kenya, ikilenga kuonyesha tamaduni, mandhari, na maendeleo ya taifa hilo kupitia maudhui yatakayoundwa na nyota hao wa mitandaoni na burudani. Kwa mujibu wa maelezo ya ubalozi, hatua ya kuwaalika wasanii na wanahabari wa mitandaoni inalenga kuongeza uelewa na kuimarisha uhusiano wa kijamii kati ya watu wa China na Kenya. Washiriki wanatarajiwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kitamaduni, kutembelea maeneo ya kihistoria, pamoja na kushuhudia maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia ya taifa hilo. Betty Kyallo anajulikana kwa mchango wake katika uanahabari na mitindo ya maisha, huku Mulamwah na Terence Creative wakitamba katika ucheshi na maudhui ya mtandaoni. MC Jessy, ambaye pia ni mwanasiasa chipukizi na mchekeshaji maarufu, atajiunga nao katika kuwasilisha hadithi za safari hiyo kwa mashabiki wao kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali. Ziara hii imeibua matarajio makubwa kutoka kwa wafuasi wa nyota hao, ambao wanatarajia kuona maudhui mapya na ya kipekee yatakayowapa mtazamo wa karibu kuhusu maisha, mandhari na maendeleo ya kisasa nchini China.

Read More
 Mashabiki Wamshinikiza Toxic Lyrikali Kuachana na Nyimbo za Mahaba

Mashabiki Wamshinikiza Toxic Lyrikali Kuachana na Nyimbo za Mahaba

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Toxic Lyrikali, yuko chini ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wake baada ya kuachia nyimbo mbili za mahaba, “Bud Flowers” na “Mpenzi” aliyomshirikisha mwanamuziki Bridget Blue. Mashabiki wengi wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka arejee kwenye mtindo wake wa zamani wa hardcore gangster rap uliomtambulisha kwenye muziki wa hip hop. Wanaeleza kuwa Toxic Lyrikali alijijengea jina kutokana na mistari mikali yenye simulizi za maisha ya mtaani, hivyo kuingia kwenye muziki wa mapenzi kunahatarisha utambulisho wake wa kisanii. Baadhi ya mashabiki wameeleza hisia zao kwa kusema kuwa nyimbo za mahaba hazimpendezi msanii huyo, na kwamba anafuata mkumbo wa soko badala ya kudumisha uhalisia wake. Wengine, hata hivyo, wamesema ni kawaida kwa msanii kubadilika na kupanua wigo wa muziki wake ili kufikia hadhira pana zaidi. Wachambuzi wa tasnia ya muziki wanaona mwelekeo huu unaweza kuwa ni mkakati wa kibiashara, lakini shinikizo la mashabiki linaweza kumlazimisha Toxic Lyrikali kurudi kwenye midundo ya rap kali aliyozoeleka nayo. Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki yapo kwa Toxic Lyrikali ili kubaini iwapo ataendelea kusimama na mwelekeo wa nyimbo za mahaba, au atasikiliza wito wa mashabiki wake na kurudi kwenye muziki wa mitaani uliomtambulisha.

Read More
 Kenya Yavizia Mataji ya Dunia Tokyo Kwa Uongozi wa Chebet na Kipyegon

Kenya Yavizia Mataji ya Dunia Tokyo Kwa Uongozi wa Chebet na Kipyegon

Macho yote yataelekezwa kwa wanariadha nyota Faith Kipyegon na Beatrice Chebet, wanaoshikilia rekodi za dunia, wakati Mashindano ya Riadha ya Dunia yatakapoanza leo katika Uwanja wa Kitaifa wa Japan, jijini Tokyo. Mwanariadha Beatrice Chebet, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 5000 na mita 10,000, atashiriki kwa mara ya kwanza katika mbio za mita 10,000 kwenye mashindano haya, akiwa na azma ya kutwaa mataji mawili ya dunia msimu huu. Chebet tayari ameonyesha uwezo mkubwa katika majukwaa ya kimataifa, baada ya kunyakua nishani ya fedha na shaba katika mbio za mita 5000 kwenye Mashindano ya Dunia yaliyofanyika Eugene, Marekani (2022) na Budapest, Hungary (2023). Mwanariadha huyo atawaongoza wenzake wakiwemo Agnes Jebet Ngetich ambaye amekuwa akiandikisha matokeo bora katika mbio za kilomita 10 ambapo aliweka rekodi ya dunia ya dakika 28 na sekunde 46 jijini Valencia, na bingwa wa Afrika Janeth Chepngetich ambaye alishinda mbio za majaribio humu nchini. Mbio za mita 10,000 kwa wanawake zitaendelea kuwa kivutio kikuu, huku taji la dunia likishikiliwa kwa sasa na Gudaf Tsegay wa Ethiopia, ambaye pia anatarajiwa kutetea ubingwa wake.

Read More
 Spotify Yaleta Sauti ya HiFi kwa Watumiaji Wake

Spotify Yaleta Sauti ya HiFi kwa Watumiaji Wake

Kampuni ya huduma ya muziki mtandaoni, Spotify, imezindua rasmi mfumo wake mpya wa sauti wa Lossless, hatua inayolenga kuwapa watumiaji wake uzoefu wa kipekee wa kusikiliza muziki kwa ubora wa juu zaidi. Mfumo wa Lossless Audio ni teknolojia ya sauti isiyopoteza ubora wowote wa faili ya muziki wakati wa kusambazwa, tofauti na mifumo ya kawaida inayopunguza ukubwa wa faili kwa gharama ya ubora wa sauti. Kwa teknolojia hii mpya, watumiaji wataweza kusikia kila nota, ala, na sauti kwa usahihi na uwazi wa hali ya juu sawa na kiwango kinachotumika katika studio wakati wa kurekodi. Spotify imetangaza kuwa huduma hii itapatikana kwa watumiaji wa mpango maalum wa HiFi, ambao unatarajiwa kuanzishwa katika miezi ijayo. Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, teknolojia ya Lossless itawezesha watumiaji wake kufurahia muziki katika kiwango cha ubora wa CD au hata zaidi, kulingana na kifaa na spika wanazotumia. Katika ushindani mkali na majukwaa mengine kama Apple Music na Tidal, ambayo tayari yalikuwa yameanzisha huduma za sauti za kiwango cha juu, uamuzi wa Spotify kuingia rasmi katika soko hili unatazamiwa kuvutia wapenzi wa muziki wanaothamini ubora wa sauti kuliko yote. Hata hivyo, Spotify imeeleza kuwa huduma hii mpya itawekwa kwa hiari, kwa kuwa inahitaji data zaidi na vifaa maalum ili kuweza kusikiliza sauti kwa kiwango kamili cha Lossless. Kwa hivyo, huduma hiyo inawalenga zaidi watumiaji wanaotumia vifaa vya kisasa na wanaohitaji ubora wa hali ya juu zaidi.

Read More
 Rapcha Aomba Radhi BASATA kwa Video Yenye Maudhui ya Ngono

Rapcha Aomba Radhi BASATA kwa Video Yenye Maudhui ya Ngono

Msanii wa Bongofleva, Rapcha ameomba radhi kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kwa Watanzania baada ya wimbo wake uitwao Yeeh kusambaa mitandaoni ukiwa na video yenye maudhui ya ngono. Rapcha alifika katika ofisi za BASATA na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji, Dkt. Kedmon Mapana, ambapo alielezwa kuhusu ukiukwaji wa maadili uliopo kwenye kazi hiyo ya sanaa. Katika kikao hicho, msanii huyo alikiri kosa lake na kuomba msamaha kwa jamii, akiahidi kuwa atazingatia maadili ya kitamaduni na kisheria katika kazi zake zijazo. Mara baada ya mazungumzo hayo, Rapcha alichukua hatua ya kuondoa video ya wimbo huo kutoka kwenye majukwaa yote ya kidijitali. BASATA, kwa upande wake, imesisitiza kuwa litaendelea kushirikiana na wasanii ili kuhakikisha kazi zao zinabaki kuwa na maudhui chanya kwa jamii. Hatua ya Rapcha imepokelewa kwa hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na wadau wa sanaa, huku baadhi wakimpongeza kwa kukubali makosa na kuonyesha mfano wa uwajibikaji, ilhali wengine wakitoa wito kwa wasanii kujitathmini kabla ya kuachia kazi zao kwa umma.

Read More
 Chino Kidd Alalamikia Kukosa Heshima Licha ya Safari Yake Kisanaa

Chino Kidd Alalamikia Kukosa Heshima Licha ya Safari Yake Kisanaa

Msanii na mcheza densi maarufu, Chino Kidd, amefunguka kuhusu changamoto anazopitia katika tasnia ya burudani. Staa huyo, anayejulikana kwa umahiri wake wa kucheza na pia sauti yake ya kipekee, amesema kuwa licha ya juhudi na historia ndefu ya kujituma, bado hajapewa heshima anayohisi anastahili. Chino Kidd amesema safari yake imekuwa ngumu, ikianzia kwenye hustling za kila aina ili kutoboa kisanaa. Amedai kuwa wengi wanaufahamu mchango wake, hasa kwenye muziki na dansi, lakini mara nyingi anapuuzwa au kuonekana kana kwamba mchango wake hauna thamani kubwa. Aidha, msanii huyo amesisitiza kuwa nia yake si kutafuta huruma, bali kutambulika kwa kazi na nidhamu yake. Anasema kuwa changamoto hizo hazijamvunja moyo, bali zinampa nguvu zaidi ya kusukuma muziki na dansi zake mbele, huku akiwataka mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono.

Read More