Allan Skin Atuhumiwa Kupora Mazao ya Kasisi Uganda

Allan Skin Atuhumiwa Kupora Mazao ya Kasisi Uganda

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, anakabiliwa na tuhuma nzito za wizi baada ya kasisi maarufu wa jiji la Kampala, Martin Ssempa, kudai kuwa alihusika katika uporaji wa mazao yake ya shambani. Kwa mujibu wa Ssempa, msafara unaodaiwa kuwa wa Allan ulisimamisha gari la mmoja wa mfanyakazi wake katika barabara ya Nakawuka-Natete,na kisha kumshushia kichapo kikali kabla ya mazao yote kuporwa. Kasisi Ssempa amesema tukio hilo limekuwa pigo kubwa kwake, kwani mazao hayo yalitarajiwa kusaidia familia yake pamoja na shughuli za kijamii za kanisa. Ametoa makataa ya siku mbili kwa Allan Skin kurejesha mazao hayo, akionya kuwa iwapo hatatii agizo hilo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Hata hivyo Ssempa amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba vitendo vya kupora mali ya wengine haviwezi kuvumiliwa katika jamii. Tukio hilo linaripotiwa kutokea usiku wa manane mapema wiki hii, wakati mfanyakazi wa kasisi huyo alipokuwa akisafirisha mzigo wa maharagwe na viazi kutoka Kabale kuelekea nyumbani.

Read More
 Shirikisho la Riadha Duniani Lafanya Mabadiliko kwa Hofu ya Joto Tokyo

Shirikisho la Riadha Duniani Lafanya Mabadiliko kwa Hofu ya Joto Tokyo

Shirikisho la Riadha Duniani limetangaza kuwa mabadiliko yamefanywa kwenye nyakati za kuanza kwa mashindano yote ya barabarani yatakayoandaliwa katika siku tatu za kwanza za Mashindano ya Riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini Tokyo, Japan, kutokana na hali ya juu ya joto inayotarajiwa jijini humo ambayo inaweza kuhatarisha afya na usalama wa wanariadha. Mashindano yaliyoathiriwa na mabadiliko haya ni pamoja na shindano la kutembea kilomita 35 kwa wanawake na wanaume litakalofanyika Jumamosi hii, pamoja na mbio za marathoni za wanaume zitakazofanyika Jumatatu ijayo. Mbio hizo sasa zitaanza dakika 30 mapema kuliko ilivyopangwa awali. Katika taarifa ya pamoja, Shirikisho la Riadha Duniani pamoja na Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo wamesema hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kutoa kipaumbele kwa afya na usalama wa wanariadha. Hata hivyo, nyakati za kuanza kwa mashindano ya ndani ya uwanja katika kipindi hicho bado hazijabadilishwa. Mashindano ya Riadha ya Dunia ya mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi Jumamosi hii jijini Tokyo.

Read More
 YouTube Yaanzisha Rasmi Mfumo Mpya wa Lugha Tofauti Katika Video

YouTube Yaanzisha Rasmi Mfumo Mpya wa Lugha Tofauti Katika Video

Kampuni ya YouTube imezindua rasmi mfumo mpya unaowezesha watazamaji kuchagua sauti za lugha mbalimbali katika video moja, hatua ambayo inalenga kuvunja mipaka ya lugha na kuongeza ushawishi wa maudhui duniani kote. Mfumo huu, ambao ulikuwa katika majaribio tangu mwaka 2023, sasa umewekwa rasmi kwa watumiaji wote. Mfumo huu unafanana na ule unaotumika kwenye majukwaa kama Netflix, ambapo video moja huweza kuwa na tafsiri za sauti (dubbing) katika lugha tofauti. Tofauti na mfumo wa manukuu (subtitles), sasa watazamaji wanaweza kusikiliza video hiyo kwa lugha wanayoielewa kabisa, kwa kuchagua sauti ya lugha nyingine moja kwa moja. Hatua hii ni ya mapinduzi kwa watengenezaji wa maudhui, hasa wale wanaotumia lugha ya Kiswahili, kwani sasa wataweza kuwafikia watazamaji ambao hawazungumzi Kiswahili. Watengenezaji wa maudhui watahitaji kupakia sauti za lugha nyingine kama sehemu ya video zao ili kutoa nafasi kwa watazamaji kuchagua lugha wanayoitaka. Kwa mfumo huu mpya, YouTube inatarajiwa kuongeza usambazaji wa maudhui kwa kiwango kikubwa, na kuwapa watayarishaji wa video fursa ya kufikia hadhira ya kimataifa bila kikwazo cha lugha.

Read More
 Huddah Aanikwa Mtandaoni kwa Kutorejesha Mkopo wa Milioni 6

Huddah Aanikwa Mtandaoni kwa Kutorejesha Mkopo wa Milioni 6

Mfanyabiashara anayejiita Madollar Mapesa, amezua gumzo baada ya kuweka wazi kwamba anamdai mrembo na mfanyabiashara, Huddah Monroe, shilingi milioni 6 za Kenya. Kupitia Instagram yake, mkopo huo ulitolewa kupitia meneja wake na ulitarajiwa kurejeshwa kwa wakati, lakini hadi sasa haujalipwa. Mapesa amesema kwamba mara nyingi huwa anawasaidia watu wengi kupata mikopo mikubwa kwa masharti nafuu kuliko benki au taasisi nyingine za kifedha, akisisitiza kuwa amewaokoa wengi dhidi ya kupoteza mali na biashara zao kwa sababu ya minada. Hata hivyo, amesema licha ya ukarimu huo, baadhi ya watu maarufu wamekuwa wakikosa kuheshimu makubaliano ya kurejesha mikopo kwa wakati. Madollar ameonya kuwa ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai yake endapo Huddah atakanusha. Pia ametuma ujumbe kwa wadaiwa wengine anaowadai akiwataka kulipa kabla hajaanza kampeni za kuwataja majina hadharani. Taarifa hizi zimechochea mjadala mkubwa mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wanamtaka Huddah kujitokeza na kueleza ukweli, huku wengine wakipuuza madai ya Mapesa wakiyataja kama mbinu ya kutafuta umaarufu.

Read More
 Teacher Wanjiku Alalamikia Usafi Duni Kwenye Vituo vya Mafuta Kenya

Teacher Wanjiku Alalamikia Usafi Duni Kwenye Vituo vya Mafuta Kenya

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Teacher Wanjiku, ameibua malalamiko dhidi ya wamiliki wa vituo vya mafuta kufuatia hali mbaya ya usafi kwenye vyoo vyao. Kupitia ujumbe wake, Wanjiku ameeleza kuchoshwa na hali duni ya usafi katika baadhi ya vituo vya mafuta jijini Nairobi, akisema kwamba licha ya wateja wao kununua bidhaa na huduma, wengi wa wamiliki hao wamepuuza jukumu la kuhakikisha vyoo vinabaki safi na salama kutumika. Aidha, ameshauri wamiliki wa vituo hivyo kutafuta suluhu ya kudumu kwa kuanza kutoza ada ndogo kwa wateja wanaotumia vyoo, ili fedha hizo zitumike kugharamia usafi. Wanjiku amesema alijikuta kwenye hali ya kudhalilishwa baada ya kutumia choo katika kituo kimoja jijini Nairobi, na kusisitiza kuwa suala la usafi linapaswa kupewa kipaumbele ili kuenzi utu wa binadamu na kulinda afya za wananchi.

Read More
 Mwigizaji Mtandaoni Am Kabugi Akanusha Taarifa za Kupatwa na Msongo

Mwigizaji Mtandaoni Am Kabugi Akanusha Taarifa za Kupatwa na Msongo

Mwigizaji wa mtandaoni, Am Kabugi, amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa anapitia changamoto za msongo wa mawazo kutokana na hali ngumu ya maisha jijini Nairobi. Kupitia Insta Story yake, Kabugi amefafanua kuwa hana tatizo la msongo wa mawazo kama inavyodaiwa, bali anatafakari uwezekano wa kuhamia miji mingine mikubwa kama Nakuru, Kisumu, Mombasa, au Eldoret ambako anaamini maisha yanaweza kuwa nafuu zaidi. Msanii huyo kutoka Kenya, ameongeza kuwa kauli yake kuhusu maisha ya Nairobi haikumaanisha kwamba amelemewa kimaisha, bali ilikuwa ni njia ya kuonesha jinsi gharama ya maisha jijini Nairobi inavyozidi kuongezeka kila siku. Hii ni baada ya mapema leo kutoa kauli kwamba maisha jijini Nairobi yamekuwa magumu, hali iliyotafsiriwa na baadhi ya mashabiki kuwa huenda anaathirika kisaikolojia.

Read More
 Eve Mungai Aumizwa na Taarifa za Mrembo wa Ex Wake Trevor Kupata Uja Uzito

Eve Mungai Aumizwa na Taarifa za Mrembo wa Ex Wake Trevor Kupata Uja Uzito

Youtuber maarufu mtandaoni, Eve Mungai, ameonekana kuumizwa na taarifa za mpenzi wake wa zamani, Director Trevor, kuthibitisha kuwa anatarajia mtoto na mrembo wake wa sasa anayejulikana kama Kiki Love. Eve, kupitia mitandao yake, aliandika ujumbe ulioonekana kuashiria kwamba hana furaha kubwa na taarifa hiyo, akisema kuwa “sio wa kwanza kupata uja uzito.” Kauli hiyo imeibua tafsiri tofauti kwa mashabiki wake, wengi wakihisi kwamba inaweza kuwa ishara ya machungu au hisia za wivu kwa hatua ya maisha ya ex wake licha ya kujaribu kujionyesha mwenye nguvu mbele ya umma. Hii inajiri baada ya Trevor mwenyewe kuthibitisha habari za ujauzito wa mrembo wake kupitia mitandao ya kijamii, akishare picha na ujumbe wa furaha akitangaza kuwa yeye na Kiki wanatarajia mtoto wao wa kwanza. Alienda mbali zaidi na kuwataka wafuasi wake wampendekezee majina watakayompa mtoto wao.

Read More
 Kauli ya Kiroho ya Mavokali Yaacha Mashabiki na Maswali

Kauli ya Kiroho ya Mavokali Yaacha Mashabiki na Maswali

Msanii wa Bongofleva, Mavokali, ameacha mashabiki wake wakijiuliza maswali baada ya kutoa ujumbe mzito wenye maudhui ya kiroho, uliojaa sala na toba kwa Mungu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mavokali ameonekana kujiweka kwa unyenyekevu mbele za Mungu, akisema kwamba hana nguvu ya kutimiza maagizo yote ya kiimani, ila anaomba rehema na msamaha kwa dhambi anazozifanya kwa siri. Katika kauli yake, Mavokali amesema kwamba siku atakapoitwa mbele za haki, anamuomba Mungu ampoke pamoja na madhaifu yake, amstiri kwa rehema na kumpunguzia maumivu ya umauti. Hitmaker huyo wa Komando, ameongeza kuwa anahisi aibu kufika mbele za Muumba akiwa na rundo la dhambi, lakini anaamini rehema za Mungu ndizo zitakazombeba. Maneno hayo yamewagusa mashabiki wake wengi, huku baadhi wakiyatafsiri kama sala binafsi ya msanii huyo, na wengine wakiamini huenda ni sehemu ya lyrics za wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni.

Read More
 Harmonize Afurahia Mapokezi Makubwa ya Video ya “LALA”

Harmonize Afurahia Mapokezi Makubwa ya Video ya “LALA”

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, amejipatia sifa kemkem baada ya mashabiki wake kuipokea kwa kishindo video ya wimbo wake mpya “LALA” aliyomshirikisha Abby Chams. Video hiyo, ambayo imekuwa gumzo mitandaoni, imepewa nyota tano na mashabiki wengi, huku ikitajwa kuwa Video Bora ya Mwaka 2025 katika ukanda wa Afrika Mashariki. Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonesha furaha yake, akisema kuwa hathamini sana namba au nyota alizopewa, bali anafarijika kuona kazi yake ikipokelewa kwa upendo. Msanii huyo amesifu jitihada za director Joma, akisema amefanya kazi safi na kuibua ubora uliowavutia wengi. Wengi wa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameeleza kuwa “LALA” ndiyo video bora zaidi mwaka huu, wakisisitiza ubunifu, ubora wa picha na utayarishaji uliosukwa kwa umakini mkubwa. Kauli kama “LALA Looks Like East African Video of the Year 2025” zimekuwa zikijirudia mara kwa mara kwenye maoni ya mashabiki.

Read More
 Kauli ya Vera Sidika Yazima Uvumi wa Kurudiana na Brown Mauzo

Kauli ya Vera Sidika Yazima Uvumi wa Kurudiana na Brown Mauzo

Socialite maarufu wa Kenya, Vera Sidika, amezima madai yanayoenezwa mitandaoni kuwa anapanga kurudiana na mzazi mwenzake, mwanamuziki Brown Mauzo licha ya kuendelea kushirikiana naye katika malezi ya watoto wao. Kupitia ujumbe aliouweka kwenye Instagram, Vera amekanusha vikali uvumi huo na kueleza kuwa maamuzi yake yamelenga tu kuhakikisha watoto wao wanapata malezi bora. Amesisitiza kwamba hatua ya kuruhusu Brown kuwa karibu na watoto wao haimaanishi kuwa anataka kurejesha mahusiano, bali ni kutambua wajibu wake kama baba. Mwanamama huyo pia amewakumbusha mashabiki wake kuwa alishawahi kuandaa “divorce party” kama alama ya kufunga ukurasa wa ndoa yake na Mauzo, jambo analosema linatosha kuonyesha kuwa hawezi kurudiana naye. Hii inakuja baada ya mijadala kuzuka mitandaoni, mashabiki wakidai kitendo chake cha kumruhusu Brown Mauzo kuja nyumbani kwake na kukaa na watoto wao ni ishara ya wawili hao kutaka kufufua uhusiano wao wa kimapenzi.

Read More
 Remix ya “Pawa” Yamletea Nyota Ndogo Zawadi ya KSh100,000 Kutoka kwa Khaligraph Jones

Remix ya “Pawa” Yamletea Nyota Ndogo Zawadi ya KSh100,000 Kutoka kwa Khaligraph Jones

Mwanamuziki wa Pwani, Nyota Ndogo, amejipatia zawadi ya shilingi laki moja kutoka kwa rapa Khaligraph Jones, hatua inayohusishwa moja kwa moja na kampeni yake ya hivi karibuni ya kumtetea Papa Jones aingizwe kwenye remix ya wimbo “Pawa” wa Mbosso. Nyota Ndogo amefichua kupitia Instagram kuwa alishtuka alipokea ujumbe wa malipo (M-PESA) kutoka kwa Khaligraph, akieleza kuwa rapa huyo alimwambia zawadi hiyo ilikuwa ni ishara ya kumshukuru kwa kusimama upande wake kwenye mjadala wa remix hiyo. Wiki kadhaa zilizopita, Nyota Ndogo alitumia mitandao ya kijamii kushinikiza wasanii na mashabiki kuona umuhimu wa Khaligraph kushirikishwa katika remix ya Pawa. Alisisitiza kuwa iwapo rapa huyo angepewa nafasi, remix ya Mbosso ingezidi kupata nguvu na mvuto mkubwa katika soko la muziki wa Afrika Mashariki. Kitendo cha Khaligraph kimepongezwa na mashabiki mitandaoni, wengi wakikitafsiri kama heshima kubwa kwa msanii huyo wa Pwani na pia kuthibitisha jinsi rapa huyo anavyoweza kuthamini wale wanaomuunga mkono. Kwa sasa, bado haijathibitishwa rasmi iwapo Khaligraph atashirikishwa kwenye remix ya Mbosso, lakini tukio hili limezua mjadala mpana kuhusu ushirikiano wa wasanii wa Tanzania na Kenya, na jinsi sapoti ya wasanii wenzao inaweza kubadilisha mwelekeo wa muziki.

Read More
 Bruno K Akanusha Tuhuma za Kusababisha Kifo cha Gogo Gloriose

Bruno K Akanusha Tuhuma za Kusababisha Kifo cha Gogo Gloriose

Msanii wa muziki kutoka Uganda, Bruno K, amekanusha vikali tuhuma za kusababisha kifo cha mwimbaji wa Injili kutoka Rwanda, Gogo Gloriose, aliyefariki dunia nchini Uganda tarehe 4 Septemba baada ya kuugua kwa muda mfupi. Bruno K amesema kuwa aliumizwa sana na madai ya baadhi ya wanablogu wa Uganda ambao walieneza uvumi kuwa alimfanyisha kazi kupita kiasi Gogo, jambo ambalo lilidaiwa kuchangia kifo chake, ili kumchafua mbele ya mashabiki wa Rwanda. Akipiga stori na Royal FM, amesema hatua ya kubebeshwa lawama kwa misingi ya uongo ni ya kikatili, akisisitiza kwamba lengo lake lilikuwa kumuinua Gogo kisanii na kumsaidia kupiga hatua katika muziki. Bruno K pia ameonyesha masikitiko yake kwa namna baadhi ya watu walivyopuuza kipaji cha marehemu wakati akiwa hai, lakini baada ya kifo chake wakaanza kuonyesha mapenzi makubwa kwake. Hata hivyo ametoa wito kwa mashabiki kuacha kupotoshwa na simulizi za uongo, badala yake waonyeshe mshikamano na familia ya Gogo katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Read More