
Meneja wa Msanii Diamond Platnumz, Babu Tale ambaye pia mmoja wa wakurugenzi wa kampuni inayojihusisha na shughuli za burudani, Tip Top Connections Company Limited yuko hatarini kufungwa jela kutokana na kushindwa kumlipa mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Mbonde, fidia ya KSh milioni 13.
Tayari Sheikh Mbonde ameshafungua maombi Mahakama Kuu akiiomba mahakama hiyo iamuru BabuTale akamatwe na afungwe kwa kushindwa kumlipa fidia hiyo.
Sheikh Mbonde amefungua maombi hayo dhidi ya Tip Top na Babu Tale baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali taarifa yao ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaamuru kulipa fidia hiyo, Agosti 17, 2022.