Gossip

Bahati Asema Hana Wivu Baada ya Baby Mama Wake Kuvishwa Pete

Bahati Asema Hana Wivu Baada ya Baby Mama Wake Kuvishwa Pete

Msanii wa muziki nchini Kenya Bahati ameamua kumpongeza mama mtoto wake, Yvette Obura, kwa uchumba wake mpya baada ya kupewa shinikizo na mashabiki wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati ametoa ujumbe wa kumpongeza Yvette baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha akivishwa pete ya uchumba na mwanaume mrefu, mwenye ngozi ya kahawia na sura ya kuvutia.

Bahati amesema amekuwa akitagwa sana kwenye video hiyo na mashabiki zake, akionyesha kuridhishwa na uamuzi wa Yvette kumpata mwanaume wa ndoto zake. Ameongeza kuwa hana kinyongo na akamkaribisha mchumba huyo wa baby mama wake kwa chakula cha pamoja ili wajuane vyema.

Ujumbe wake uliwavutia mashabiki wengi waliomsifu kwa ukomavu wa kiakili na ucheshi wake, huku wengine wakimpongeza kwa kudumisha urafiki mzuri na mama mtoto wake licha ya tofauti zao za zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *