Mchekeshaji na Mwanaharakati, Eric Omondi, amewashangaza mashabiki wake baada ya kukutana ana kwa ana na jamaa anayefanana naye kwa kiasi kikubwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric amepakia video akionekana pamoja na kijana huyo wanaofanana kimwonekano, wakiwa wanashiriki matangazo ya kibiashara. Video hiyo imezua gumzo kubwa mtandaoni, mashabiki wengi wakishangaa kufanana kwao kiasi cha wengine kushindwa kutofautisha yupi ni Eric halisi.
Mashabiki wamefurahishwa na hatua ya Eric kukutana na pacha wake, huku wengine wakisifu ubunifu wake wa kutumia tukio hilo kama fursa ya kibiashara.
Tukio hilo limejiri siku chache tu baada ya Eric kutangaza hadharani kwamba alikuwa akimtafuta kijana huyo anayedaiwa kutoka Githurai, Nairobi, kufuatia video iliyosambaa ikimuonyesha jamaa huyo akionekana kama nakala halisi ya mchekeshaji huyo.