
Msanii wa muziki wa Kenya, Dufla Diligon, amezua mjadala mtandaoni baada ya kufichua kuwa amefungiwa (blocked) na mchekeshaji maarufu Mulamwah kwenye mtandao wa Instagram.
Kupitia Instastory yake, Dufla alisimulia tukio hilo kwa mshangao na utani, akisema kuwa aligundua amefungiwa wakati alipokuwa akitafuta akaunti ya Mulamwah akiwa katika mazungumzo na msanii Lyanii.
“Jana tulikuwa na mazungumzo na @officialiyanii, halafu nikaamua kutafuta akaunti ya Mulamwah kwenye IG. Nilishangaa kuona nimefungiwa. Kumbe mimi na Obinna tuko kwa listi moja!” aliandika Dufla.
Katika ujumbe wake, Dufla hakusita kuonyesha mshangao wake na hata kumtaka Mulamwah “kupunguza hisia”, akionekana kutofahamu chanzo cha hatua hiyo ya mchekeshaji huyo.
“Punguza feelings buda!!!” aliongeza, kwa mtindo wa utani lakini uliobeba ujumbe mzito.
Hadi sasa, Mulamwah hajatoa majibu yoyote hadharani kuhusu hatua hiyo, wala kueleza sababu ya kuwazima Dufla na Obinna kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo, mashabiki wa pande zote wameendelea kutoa maoni tofauti, wengine wakisisitiza haja ya kuwepo kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahusika badala ya kupeana block mitandaoni.