Mjasiriamali na socialite maarufu, Huddah Monroe, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kutoa matamshi makali akiwakosoa baadhi ya wanaume wa Kenya kwa kile alichokiita tabia ya kuwadhalilisha na kutowaheshimu wanawake.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Huddah amesema hataki tena kuzungumza au kujihusisha na wanaume wa “millennials”, akiwataja kama kizazi kisichoheshimu wanawake na kinachopenda kutumia maneno ya dharau. Amesema kuwa kulingana na uzoefu wake, wanaume wa kizazi hicho mara nyingi hukosa adabu wanapowasiliana na wanawake.
Huddah ameongeza kuwa anaona afadhali kuzungumza na kizazi kipya cha Gen Z, akisema kuwa angalau wao wanaonyesha viwango vya juu vya heshima na ustaarabu linapokuja suala la kuwasiliana na wanawake.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Huddah kufunguka kupitia Insta story yake kuhusu tukio alilodai lilimtokea katika moja ya hoteli ya kifahari jijini Nairobi, ambapo mwanaume alimfuata kwa njia aliyoiita isiyo na heshima, na kujaribu kumtongoza bila staha.