Sports news

Harambee Stars Kuchuana na Senegal Leo Kwenye Mchezo wa Kirafiki

Harambee Stars Kuchuana na Senegal Leo Kwenye Mchezo wa Kirafiki

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, itakutana na Senegal leo jioni katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa katika Uwanja wa Mardan hapa Uturuki.

Mchuano huu utakuwa wa pili wa kirafiki wa kimataifa kwa Stars mwezi huu, baada ya kufungwa bao moja kwa nunge na Equatorial Guinea Ijumaa iliyopita. Historia inaonyesha kuwa timu hizo zimekutana mara nne, ambapo Senegal imeandikisha ushindi mara tatu na kutoka sare mara moja. Mechi ya mwisho ya Harambe Stars dhidi ya Senegal ilikuwa mwaka 2019 katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ambapo Stars ilipoteza mabao matatu kwa nunge.

Mechi ya leo itakuwa fursa muhimu kwa Stars kujipima nguvu dhidi ya wapinzani wao wenye viwango vya juu huku ikijinoa kabla ya mechi zijazo za ushindani. Kocha na wachezaji wanatarajiwa kutumia mchezo huu kuimarisha mikakati na kuimarisha mawasiliano uwanjani kabla ya mashindano makubwa yajayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *