Prodyuza wa muziki nchini Kenya, Magix Enga, ametangaza rasmi kuvunjika kwa uhusiano wake na mpenzi wake wa muda mrefu, Ruth Otieno, hatua aliyosema imekuja baada ya wawili hao kukubaliana kwa amani na heshima.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Magix Enga ameeleza kuwa yeye na Ruth wamepitia mambo mengi pamoja, na kutokana na safari hiyo na changamoto walizopitia, ameamua kuchukua hatua ya kusonga mbele bila uwepo wake . Hata hivyo, amesisitiza kuwa hana kinyongo na hatamani mabaya kwa Ruth, akimtakia furaha na upendo anaoustahili katika maisha yake ya baadaye.
Katika ujumbe wake, ameweka wazi kuwa mtoto wao, Starboy Hotani, atasalia kuwa kipaumbele chake cha kwanza, na ataendelea kumpa msaada wa kila aina bila kujali mabadiliko ya kimahusiano. Ameongeza kuwa licha ya kutokuwa pamoja tena, Ruth anaweza kumfikia wakati wowote inapohitajika kwa mambo muhimu yanayomhusu mtoto wao.
Magix Enga amemaliza ujumbe wake kwa kuonyesha shukrani kwa nafasi ambayo Ruth alichukua katika maisha yake huku akisisitiza kuwa wanatarajia kusonga mbele kwa amani na furaha katika njia zao tofauti za maisha.