Msanii na mjasiriamali kutoka Tanzania, Shilole, amenusurika katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Malagarasi, mkoani Kigoma, alipokuwa safarini akirejea Dodoma akitokea Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Cleyton Chipando maarufu Baba Levo, Shilole alikuwa akitumia gari aina ya Toyota Alphard lililogonga ng’ombe barabarani, hali iliyopelekea ajali hiyo kutokea.
Mbunge huyo ameeleza kuwa Shilole kwa sasa anaendelea kupata matibabu mkoani Tabora, huku juhudi zikiendelea kuhakikisha anapatiwa huduma zote muhimu za kitabibu.
Shilole alikuwa miongoni mwa watu waliofanikisha shughuli ya Pilau Day iliyoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia mgahawa wake wa Shishi Food, ikiwa ni sehemu ya sherehe za Mwaka Mpya zilizofanyika mjini Kigoma.