Gossip

Mwijaku Akanusha Taarifa za Kuachana na Mke Wake

Mwijaku Akanusha Taarifa za Kuachana na Mke Wake

Mwanamitandao maarufu nchini Tanzania, Mwijaku, amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa ameachana na mke wake.

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari nchini humo, amesisitiza kwamba bado wako pamoja licha ya mke wake kuondoka nyumbani kwa muda.

Mwijaku ambaye anafahamika kama DC wa Instagram, amefafanua kuwa hatua ya mke wake kutohonekana nyumbani haimaanishi kuvunjika kwa ndoa yao, kwani anafahamu aliko na wanawasiliana.

Ameeleza kuwa taarifa zilizoenezwa mtandaoni zimetiwa chumvi, akibainisha kuwa hakuna mgogoro wa mali kati yao kama inavyodaiwa. Kwa mujibu wa Mwijaku, kila mali waliyonayo ina jina la muhusika, na mali pekee wanayomiliki kwa pamoja ni kiwanja.

Kauli ya Mwijaku imekuja kufuatia mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mustakabali wa ndoa yake, na amesisitiza kuwa wanashughulikia mambo yao kwa utulivu pasipo ushawishi wa taarifa za mitandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *