Entertainment

Shay Diva atupwa Jela miaka 4 kwa kughusisha stakabadhi ya gari

Shay Diva atupwa Jela miaka 4 kwa kughusisha stakabadhi ya gari

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Shay Diva amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela au faini ya ksh 200,000 baada ya kupatikana na hatia ya kumuibia aliyekuwa mpenzi wake PJ Dodhia Kumar gairi aina ya Toyota Land cruiser V8.

Mahakama ya Kitale ilimpata na hatia ya kuingia kwenye akaunti ya TIMs/NTSA ya bwenyenye PJ Dodhia Kumar na kuhamisha umiliki wa gari hilo kwake bila kufuata taratibu stahiki za umiliki.

Shay Diva aliomba kupunguziwa hukumu kali aliyopewa na mahakama akidai kuwa yeye ndiye anategemewa na familia yake ikizingatiwa kuwa anamhudumia mama yake mgonjwa na ndugu zake wanne.

Ikumbukwe Mwanamuziki huyo alishtakiwa baada ya familia yake kubaini kuwa Shay Diva alikuwa amechukua gari hilo kwa njia ya utata, waliahamua kufungulia mashtaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *