Akothee azua gumzo mtandaoni kwa kutangaza baby shower ya mbwa wake

Akothee azua gumzo mtandaoni kwa kutangaza baby shower ya mbwa wake

Mwimbaji Akothee amezua gumzo mtandaoni kwa kutangaza yupo mbioni kuandaa hafla ya kusherekea mbwa wake wa kike ambaye atajifungua hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema atafanya baby shower ya mbwa wake aitwaye Salome jumapili hiii kwenye hafla ambayo atawaalika marafiki pamoja na wanafamilia ambao kwa njia moja au nyingine wataandamana mbwa wao wa kike na kiume. Post hii hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakitilia shaka uwezo wa kufikiria wa mwanamama huyo huku wengine wakishangaza na hatua ya Akothee kutumia pesa nyingi kumwaandalia mbwa wake baby shower wakati wakenya wanakumbwa na baa la njaa.

Read More
 DR. OFWENEKE AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA AKOTHEE

DR. OFWENEKE AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA AKOTHEE

Mchekeshaji Dr. Ofweneke amekanusha kuwa kwenye bifu na Akothee baada ya kumtaka mwimbaji huyo amlipe shilllingi millioni 1.4 ili awe mshereheshaji(MC) kwenye hafla ya harusi yake. Kwenye mahojiano na Mpasho Ofweneke amesema hana ugomvi na mwanamama huyo wa watoto 5 kama namna watu wanavyohoji kwenye mitandao ya kijamii kwani ni marafiki wakubwa. Mchekeshaji huyo amesema ana imani kuwa Akothee ana uwezo mkubwa wa kumlipa pesa hizo kwani bado wapo kwenye mchakato wa kukamilisha mazungumzo kati yao.

Read More
 AKOTHEE AMJIBU OFWENEKE KWA KUTAKA SHILLINGI MILLIONI 1.4 KUSHEREHESHA HARUSI YAKE

AKOTHEE AMJIBU OFWENEKE KWA KUTAKA SHILLINGI MILLIONI 1.4 KUSHEREHESHA HARUSI YAKE

Msanii Akothee ameshindwa kuficha hisia zake baada ya mchekeshaji Dr. Ofweneka kumtaka alipe shillingi millioni 1.4  kama anahitaji huduma yake kama mshereheshaji kwenye hafla ya harusi yake. Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema mchekeshaji huyo ambaye ni rafiki yake wa karibu amedai  kiasi hicho cha pesa kwa sababu anaolewa na mzungu. Mwanamama huyo ameenda mbali zaidi na kujigamba kuwa hakuna mwanaume wa Kenya ambaye angemtosheleza kimapenzi ndio maana alikimbilia penzi la mzungu. Hata hivyo wakenya wameonekana kumuunga mkono ofweneka kwa hatua ya kumlipisha akothee pesa nyingi wakisema mwimbaji huyo anastahili kutoa kiasi hicho cha pesa kwa kuwa ni tajiri. Kauli ya akothee wakati huu  yupo mbioni kufunga ndoa na mpenzi wake mzungu ambaye alimtambulisha juzi kati na tayari amewataka waandaji wa harusi watume maombi ya kusimamia shughuli yake ya harusi yake.

Read More
 AKOTHEE AKASHIFU UBALOZI WA KENYA NCHINI SAUDIA ARABIA

AKOTHEE AKASHIFU UBALOZI WA KENYA NCHINI SAUDIA ARABIA

Mwanamuziki Akothee ametilia shaka utendakazi wa ubalozi wa Kenya nchini Saudia Arabia kufuatia kuongezeka kwa visa vya wakenya kudhulumiwa na waajiri wao kwenye taifa hilo la bara Asia. Akothee ametoa changamoto kwa serikali ya kenya kuchukua hatua madhubuti kuwaokoa wananchi wake kwa utumwa wanaofanyiwa nchini Saudia, akisema mawakala waliotwikwa jukumu la kuwalinda wakenya dhidi manyanyaso hawafanyi kazi yao ipasavyo. Mwimbaji huyo amesema ni kitendo cha aibu kwa nchi ya kenya kuona wananchi wake wakiteseka ughaibuni wakiwa kwenye harakati za kusaka riziki ambapo ametaka kubuniwe kwa sheria ya kuwazuia watu kusafiri kwenda kufanya kazi nchini Saudia Arabia Hata hivyo ametoa wito kwa mashariki ya kibinadamu kujitokeza na kushinikiza mabadiliko huku akiwaonya wanawake wa Kenya kuchukua tahadhari kabla ya kusafiri nchini Saudia Arabia kutokana na kuongezeka kwa dhuluma dhidi ya wafanyikazi wa nyumbani. Kauli yake imekuja siku chache baada ya serikali kumuokoa Diana Chepkemoi na wasichana wengine 20 waliokuwa wamekwama nchini Saudia Arabia.

Read More
 AKOTHEE AWAKOSOA WANAWAKE WASIOWAPOSTI WAPENZI WAO MTANDONI

AKOTHEE AWAKOSOA WANAWAKE WASIOWAPOSTI WAPENZI WAO MTANDONI

Mwanamuziki asiyeishiwa na vituko kila leo nchini Akothee amezua ngumzo mtandaoni mara baada ya kudai kwamba wanawake wengi ambao hawaposti wapenzi wao kwenye mitandao ya kijamii wapo kwenye mahusiano mengine. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Akothee amesema wanawake sampuli hiyo wanashiriki vitendo vya usaliti kwa kutoka kimapenzi na wanaume tofauti ambao mara nyingi huwatimizia mahitaji yao ya msingi, jambo amedai limewafanya kusahau kuwaonyesha upendo wapenzi wao. Hata hivyo ujumbe huo wa Akothee umezua hisia kinzani kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo baadhi wamekubaliana nae huku wengine wakionekana kushangazwa na kauli ya mwanamama huyo ambaye amekuwa kwenye mahusiano mengi ya kimapenzi na wanaume mbali mbali. Kauli ya Akothee inakuja siku chache mara baada ya kumtambulisha mpenzi wake mzungu na kudai kuwa yuko tayari kufunga nae ndoa kwa kuwa ameshapata furaha ambayo amekuwa akitafuta kwa muda mrefu.

Read More
 AKOTHEE ADOKEZA MPANGO KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE MPYA

AKOTHEE ADOKEZA MPANGO KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE MPYA

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu nchini, Akothee anayafurahia sana mahusiano yake mapya na hivi karibuni huenda tukashuhudia akifunga ndoa na mpenzi wake mzungu. Siku chache tu baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya, mama huyo wa watoto watano sasa amebainisha kuwa baada ya kuhangaika miaka mingi akitafuta mapenzi, hatimaye amempata mwenzi wa maisha. “Sikujua kijiji changu kingeweza kuwa Paradiso, Mfalme alikuwa akikosekana, sasa naweza kusema maisha yangu yamekamilika na niko tayari kutulia, niko tayari kuwa mke mtiifu,” amesema Akothee. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliambatanisha ujumbe huo na picha inayomuonyesha akiwa amekumbatiwa na mpenzi wake mpya na kutangaza kwamba walikuwa wakielekea katika mbuga ya wanyama ya Ruma kwa ajili ya kutalii.

Read More
 AKOTHEE AKANUSHA KUSHIRIKI BIASHARA YA ULANGUZI WA BINADAMU

AKOTHEE AKANUSHA KUSHIRIKI BIASHARA YA ULANGUZI WA BINADAMU

Staa wa muziki nchini Akothee amekanusha vikali tuhuma za kujihusisha na biashara ya ulanguzi wa binadamu. Hii ni baada ya walimwengu kwenye mitandao kuibua madai kuwa anamiliki kampuni inayosajili watoto wa kike nchini na kisha kuwatafutia kazi kwenye nchi za miliki ya kiarabu. Kupitia mfululizo wa Instastory mama huyo wa watoto 5 amepuzilia mbali madai hayo huku akiwataka wanaotilia shaka utajiri wake kufanya utafiti kwanza kabla ya kuzungumzia vibaya. Hitmaker huyo wa “Abebo” amewakejeli wanaodai kuwa utajiri wake umetokana na biashara ya ulanguzi wa binadamu, kwa kusema kuwa wamtumie vyombo vya usalama zimtie nguvuni badala ya kupiga kelele mtandaoni.. “Send DCI to come and arrest me. Aacha kupiga kelele social media. Yes, you are very right, there is no money in music,” Ameandika. Kauli ya Akothee imekuja mara baada ya wakenya kuzua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii kufuatia visa vya wasichana kudhulumiwa na waajiri wao kuongezeka katika nchini za kiarabu.

Read More
 AKOTHEE AWAPA SOMO WANAUME MTANDAONI

AKOTHEE AWAPA SOMO WANAUME MTANDAONI

Staa wa muziki nchini Akothee amewataka wanaume kuacha kumtumia jumbe tamu za kimahaba kwenye mitandao kwa nia ya kumtongoza. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mama huyo wa watoto watano ameweka wazi kuwa hawezi kuanguka kwenye mtego wa mapenzi ya mitandaoni kwa kuwa anapendelea kukutana na mtu ana kwa ana. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sweet Love” amedokeza kuwa hofu yake ya mambo ya mitandaoni imetokana na matukio ya nyuma yaliyoishia kuuvunja moyo wake. Hata hivyo amekiri kuwa yeye ni mwathiriwa wa unafiki ulio kwenye mitandao ya kijamii kwani amewahi kukutana na watu wengi waongo.

Read More
 AKOTHEE MBIONI KUFUNGUA SHULE YA WATOTO WENYE UHITAJI KATIKA JAMII

AKOTHEE MBIONI KUFUNGUA SHULE YA WATOTO WENYE UHITAJI KATIKA JAMII

Msanii na mfanyabiashara maarufu nchini Akothee, ametangaza kuwa anajenga shule ambayo watoto wanaotoka katika familia maskini wataweza kusoma bila malipo. Akothee ameweka wazi taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa alitoa ekari 7 za ardhi kupitia wakfu wake, Akothee Foundation kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo aliyoipa jina la Akothee Foundation Academy. Mwanamama huyo amewahimiza mashabiki zake ambao kwa njia moja au nyingine wangependa kuwa sehemu ya kufanikisha ndoto zake zitimie wamtafute. Kando na kutoa elimu bure, wanafunzi hao pia watapewa sare, kifungua kinywa na chakula cha mchana shuleni. “Akothee Foundation Academy. Kutoa elimu bure kwa wasiojiweza. Wanafunzi wataoga shuleni, watavaa shuleni, watakula na kupata kifungua kinywa na chakula cha mchana shuleni bila malipo,” Akothee alisema.   Aliongeza, “Mwaka jana nilitoa ekari 7 za Ardhi kwa AKOTHEE FOUNDATION. Akothee foundation Academy kwenye Bodi. Nikizungumza, nafanya. Hii ndio ndoto kuu inayonisababishia kukosa usingizi usiku. Mapambano tarehe 10 Januari 2023… Ninapomaliza mradi sasa naweza kupumzika kwa amani. ”

Read More
 AKOTHEE AWAPO SOMO MASHABIKI, ACHENI KUWAIGA WATU MAARUFU MITANDAONI

AKOTHEE AWAPO SOMO MASHABIKI, ACHENI KUWAIGA WATU MAARUFU MITANDAONI

Mwanamuziki Akothee amewataka mashabiki zake kuacha kujilinganisha na watu maarufu mtandaoni na badala yake watie bidii ili waweze kutimiza mafanikio yao. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Akothee amesema mastaa wengi huwa hawachapishi  matatizo yao kwenye mitandao ya kijamii No one shows off their struggle, everyone wants to look like success itself. Akothee is one real deal, what you see is what you get. Be careful whom you follow, do they motivate, inspire you, or do they choke you with lies and make you feel like, you are not living?” ameandika Hitmaker huyo wa Sweet love amesema kila mtu ni mpangaji wa maisha yake na kile ambacho mtu anakifanya kwa sasa inaashiria mafanikio au anguko lake katika siku za mbele. “My friend, you must work hard. To have good things, the good life comes with sacrifices, not with iPhone, filters, and backgrounds. You can never earn a penny for being famous. Most people are just famous for being famous with zero investments, and zero earnings. Think fame can only take you to big hotels, free intimacy and free foods. Ask celebs.” Ameongeza Akothee ambaye yupo nchini Ufaransa kwa ajili ya tour yake ya kimuziki, ameongeza kuwa mitandao ya kijamii inaweza kumfanya mtu akapatwa na msongo wa mawazo

Read More
 AKOTHEE AWAPA SOMO MASHABIKI,AWATAKA WAJIPE KIPAUMBELE MAISHANI

AKOTHEE AWAPA SOMO MASHABIKI,AWATAKA WAJIPE KIPAUMBELE MAISHANI

Staa wa muziki nchini Esther Akoth, maarufu Akothee amewashauri mashabiki zake kujiamini kuwa wanaweza pata amani bila usaidizi wa mtu yeyote. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya Oyoyo ameshea picha yake ya mwaka wa 2018 na kusema kwamba kipindi hicho alikuwa anapitia wakati mgumu katika maisha yake. Akothee amesema ilibidi afanye baadhi ya mabadiliko katika maisha yake kwa ajili ya kujiweka sawa kutokana na msongo wa mawazo ikiwemo kuwapiga msasa watu waliokuwa karibu naye kipindi hicho. Hata hivyo Akothee amewataka mashabiki zake wawe wabahili na wajiweke kipau mbele katika maisha yao kwa kujijali sana.

Read More
 AKOTHEE MBIONI KUJIPANDIKIZA MBEGU YA KIUME KUFANIKISHA NDOTO YA KUPATA MTOTO.

AKOTHEE MBIONI KUJIPANDIKIZA MBEGU YA KIUME KUFANIKISHA NDOTO YA KUPATA MTOTO.

Msanii wa muziki nchini Akothee amedokeza mpango wa kupata mimba kwa njia ya kisanyasi ili kukata kiu yake ya kutamani mtoto. Akothee ambaye ana umri wa miaka 39 amesema kwa sasa ana mpango wa kumtafuta mpenzi, hivyo ameamua kutumia njia ya kupandikazi mbegu za kiume hospitalini ili mwisho wa siku apate mimba. Akothee yupo kwenye ziara ya kimuziki nchini ufaransa na watoto wake watano amesema watu wasishangaa au kumuuliza baba wa mtoto wake pindi watakapomuona akiwa mjamzito hivi karibuni. “I have something for kids. I miss something and I don’t want to get pregnant at 45. Since looks like a partner won’t be possible soon. I will be going for Artificial Insemination here in France. So when you see me pregnant don’t ask me who the father is. All I want is my own baby with No drama,. Cheers and good night,” Akothee ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo amewashauri watu kwenye jamii kujihusisha au kufanya mambo yanayowafurahisha duniani kwa kuwa maisha ni yao. “Do what you want to do in this life, Its your life,” Amesema.

Read More