AKOTHEE AFUNGUKA NAMNA TUHUMA ZA ILLUMINATI ZILIVYOATHIRI BINTI YAKE KIMASOMO.

AKOTHEE AFUNGUKA NAMNA TUHUMA ZA ILLUMINATI ZILIVYOATHIRI BINTI YAKE KIMASOMO.

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Esther Akoth maarufu Akothee amefunguka sababu zilizompelekea binti yake Prudence Otieno aka Fancy Makadia kusomea shule mbali mbali nchini. Kulingana na mwimbaji huyo Fancy alituhumiwa kuwa ni mshirika dhehebu la kishetani la illuminati akiwa shule ya upili ya wasichana ya Ulanda jambo ambalo lilimlazimu kumhamisha kwenye shule ghali zaidi nchini Kenya, ⁣Braeburn Group of International Schools. Hitmaker huyo wa ngoma ya Abebo amesema tuhuma hizo zilimuathiri binti yake kisaikolajia kiasi cha kutofanya vizuri kimasomo kwani kila mara alihisi kutengwa na wanafunzi wenzake. Hata hivyo amesema anashukuru Mungu binti yake Prudence alikamilisha masomo yake ya kidato cha nne katika shule ya Braeburn Group of International Schools na akajiunga na chuo kikuu nchini Ufaransa kusomea shahada ya masuala ya utalii na usimamizi. Kwa sasa, Makadia yupo nchini France ambako yupo mbioni kukamilisha mtihani wake wa mwisho wiki hii ambao utatoa nafasi kwake kukamilisha masomo yake. Mei mwaka wa 2019 Akothee alidai kuwa alimpeleka binti yake kwenye moja ya chuo kikuu ghali zaidi huko Paris, Ufaransa ambapo alienda mbali zaidi na kufichua kwamba alilipa takriban shilllingi millioni 2.2 za Kenya baada ya binti yake kujiunga na chuo hicho.

Read More
 AKOTHEE AWEKA WAZI KIASI CHA PESA ANAYOTOZA KWA SHOW MOJA

AKOTHEE AWEKA WAZI KIASI CHA PESA ANAYOTOZA KWA SHOW MOJA

Msanii nyota Akothee ameamua kutaja kiasi cha pesa anacholipisha kwa show zake  iwapo utahitaji kufanya kazi nae. Katika mahojiano yake hivi karibuni Akothee ametangaza kuongeza pesa anazozilipisha kwa show moja kutoka shillingi millioni 1.5 hadi 2.3 za Kenya. Akothee ambaye anafanya vizuri na album yake mpya iitwayo Akothee the lioness amesema amechukua hatua hiyo kutokana na bidii anayoweka kila siku kwenye shughuli zake za muziki kwani amekuwa akiwekeza pesa nyingi kutoa muziki mzuri. Katika hatua nyingine amenyoosha maelezo maelezo kuhusu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks kwa kusema kwamba aliachana na jamaa huyo mwezi disemba mwaka jana baada ya uhusiano kuingiwa na ukungu. Akothee amesema hayo alipokuwa anawasilisha mapendekezo ya kuwasaidia wasanii kupata shows na nyimbo zao kuchezwa kwenye vyombo vya habari katika chama cha hakimiliki na muziki na hakimiliki nchini MCSK

Read More
 PENZI LA AKOTHEE NA NELLY OAKS LAFIKIA KIKOMO

PENZI LA AKOTHEE NA NELLY OAKS LAFIKIA KIKOMO

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amewaacha wafuasi wake na maswali mengi baada ya kukiri hadharani kuchoshwa na mapenzi. Kupitia ukarasa wake Instagram Akothee amethibitisha kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Nelly Oaks huku akisema kwamba hatoweka wazi sababu za kuachana na mpenzi wake huyo . Msanii huyo amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake zote kwenye muziki huku akiwataka wanablogu kutomuuliza maswali kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutochukulia kwa uzito taarifa hiyo kwa kuwa mwanamama huyo amekuwa na mazoea ya kutangaza kuachana na Nelly Oaks mara kwa mara lakini baadae wanafuafua penzi lao.

Read More
 AKOTHEE AZINDUA RASMI KITABU CHAKE

AKOTHEE AZINDUA RASMI KITABU CHAKE

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini, Akothee amezindua rasmi kitabu chake ambacho amekipa jina la “Akothee Quotes”. Akothee Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Hilo ambapo amesema kwamba kitabu hicho kinaelezea namna ya kufanikiwa kwenye maisha katika nyanja mbalimbali. Kwenye kitabu hicho ambacho kinapatikana kwenye maduka kadhaa ya kuuza vitabu nchini, Akothee amesimulia kuhusu maisha yake kama mtu maarufu na maisha yake binafsi. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Abebo” anajiunga na orodha ya Mastaa ambao tayari wameandika vitabu vyao kama Janet Mbugua, Lupita Nyong’o, Polycarp Otieno wa Sauti Sol, Robert Burale na Nganga.

Read More
 AKOTHEE AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

AKOTHEE AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki maarufu nchini Akothee ameachia rasmi Album yake mpya inayokwenda kwa jina la Sibuor Madhako. Sibuor Madhako Album ina jumla ya ngoma 8 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Tony Nyadundo na Kamanu. Album hiyo ina nyimbo kama Siponsa, Expensive Baby, Mpenzi, Nisimamie, Abebo, Dende Nyom, Nkoro Nditu na Mapenzi Chonyi. Akizungumza kwenye uzinduzi wa Album hiyo, Akothee amesema ameachia album hiyo kwa ajili ya kuwapa moyo waliokata tamaa maishani lakini pia kwa singles mothers wote ambao wanapambana kuwalea wanao bila usaidizi wa mtu yeyote. Sibuor Madhako ni Album ya kwanza kwa mtu mzima Akothee tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa Youtube.

Read More
 AKOTHEE MBIONI KUZINDUA KITABU CHAKE

AKOTHEE MBIONI KUZINDUA KITABU CHAKE

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini, Akothee anatarajiwa kuzindua kitabu chake  ambacho amekipa jina la “Akothee Quotes”. Akothee Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Hilo ambapo amesema kwamba kitabu hicho kinaelezea namna ya kufanikiwa kwenye maisha katika nyanja mbalimbali. Kwenye kitabu hicho ambacho kitazinduliwa rasmi  Juni 4, mwaka huu katika hoteli ya Eka Hotel, Akothee amesimulia kuhusu maisha yake kama mtu maarufu na maisha yake binafsi. Hata hivyo ametoa wito kwa mashabiki kukaa mkao kula kununua kitabu cha Akothee Quotes huku akisema sehemu ambayo anaipenda kwenye kitabu hicho  ni ile ambayo inazungumzia maisha ya malezi ya watoto.

Read More
 AKOTHEE AWATOLEA UVIVU WANAOFURAHIA ANGUKO LAKE

AKOTHEE AWATOLEA UVIVU WANAOFURAHIA ANGUKO LAKE

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amekanusha madai ya kuachana na mpenzi wake Nelly Oaks mara baada ya kuandika ujumbe uliotafsiriwa na wengi kuwa huenda penzi lao limefikia kikomo. Kupitia instagram Akothee ameshangazwa na kitendo cha watu kufurahia anguko lake huku akidai kwamba chapisho lake lilikuwa mzaha. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kutofurahishwa na hatua ya Akothee kuwadanganya wafuasi wake huku wengine wakidai kuwa msanii huyo anatafuta  mazingira ya kuzungumziwa na wanablogu.

Read More
 AKOTHEE AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO

AKOTHEE AKIRI KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO

Mwanamuziki maarufu nchini Akothee amefunguka safari ya kupambana na msongo wa mawazo ikiwa ni siku chache imepita baada ya kufikisha umri wa miaka 41. Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee ameeleza kuwa amekuwa aking’ang’ana na msongo wa mawazo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita huku akiwahimiza wanaokumbana matatizo hayo ya afya ya akili kujitokeza na kuzungumzia hali zao kwa watu wao karibu ili waweze kupata usaidizi. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sweet Love” ametoa angalizo kwa jamii kutochukulia matatizo ya afya ya akili kwa mzaha huku akisema kwa sasa anafurahia jinsi hali yake ya afya ya akili inazidi kuhimarika. Utakumbuka Mwezi Septemba mwaka wa 2021 Mwimbaji huyo alitasanua kuwa amekuwa akipambana na hofu ya kuwa mtu maarufu ambapo alienda mbali zaidi na kukiri kuwa ilifika pahali alianza kuwaepuka mashabiki zake kiasi cha kujuta kuwa na umaarufu.

Read More
 AKOTHEE ALAMBA SHAVU YA UBALOZI UNGA LIMITED

AKOTHEE ALAMBA SHAVU YA UBALOZI UNGA LIMITED

Staa wa muziki nchini Akothee amelamba dili nono la kuwa balozi wa kampuni ya Unga Limited ambayo inazalisha unga wa ugali,uji na ngano. Akothee ametengaza habari njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Unga limited. Lakini pia ameishikuru uongozi wa kampuni ya Unga limited kwa kutambua nguvu yake na kuhamua kumpatia dili hilo ambalo litamjengea heshima. Hata hivyo kampuni ya Unga Limited imesema imeingia ubia kufanya kazi na Akothee kwa sababu ya ubunifu, bidii pamoja na ushawishi wake kwenye jamii huku ikisema kwamba wana imani msanii huyo ataingozea kampuni hiyo wateja wengi zaidi. Akothee sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Unga limited kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongeza mauzo ya unga hiyo ya ugali, uji na ngano.

Read More
 AKOTHEE AJUTA KUWAWEKA WANAE MITANDAONI

AKOTHEE AJUTA KUWAWEKA WANAE MITANDAONI

Staa wa muziki na mfanyabiashara kutoka Kenya, mwanamama Akothee amejutia maamuzi yake ya kuwaweka watoto wake mitandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti chati yake ya mtandao wa WhatsApp (screenshot) na mmoja wa watoto wake ambaye anamuomba afute akaunti yake ya Instagram. “Hili ni kosa ambalo nitaishi nikijutia, kuleta wanangu kwenye mitandao iliyojaa wachawi na uchawi kutoka kona zote za ulimwengu. Mimi nilidhani ni kitu kizuri kuonyesha maisha yangu kama njia ya kutia wengine moyo lakini wapi!” ameandika Akothee. Akothee ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao “Nkoro Ndito” ametoa ushauri kwa wazazi wengine wasipende kuwaweke watoto wao mitandaoni huku akisema kwamba hili limesababisha aondoe uhusiano wake wa kimapenzi mitandaoni. “Tayari ninahisi joto na itabidi nitafute njia ya kujisamehe kwa kuumiza familia yangu.” alimalizia Akothee ukupitia ukurasa wake wa Instagram.

Read More
 AKOTHEE ARUDI SHULE KUPATA SHAHADA

AKOTHEE ARUDI SHULE KUPATA SHAHADA

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee ameweka wazi kwamba amerejea shuleni kuendeleza masomo yake ili kupata shahada. Mama huyo wa watoto watano amesema anatia bidii kubwa masomoni ili kumfanya mama yake ajivunie kumzaa mtoto kama yeye. “Nilipotakiwa kuwa shuleni, niliamua kuwa mke, sasa badala ya kuwa mke, niko shuleni nikiwa na umri mkubwa maisha, haya maisha hayawi sawa kabisa” amesema. “Lakini lazima nipate Shahada yangu kwa sababu ya mama yangu ili afurahie kuwa na kofia hiyo nyumbani kwake,” amesema Akothee kupitia ukurasa wake wa Instagram. Utakumbuka Akothee anataka kuwa miongoni mwa wasanii matajiri sana nchini Kenya ambapo utajiri wake unakadiriwa kufikia Dola10 Milioni

Read More
 AKOTHEE KUANZA ZIARA YAKE YA KIMUZIKI JULAI MWAKA 2022

AKOTHEE KUANZA ZIARA YAKE YA KIMUZIKI JULAI MWAKA 2022

Staa wa muziki nchini Akothee ametangaza kuanza kwa ziara yake ya kimuziki mwezi Julai mwaka wa 2022 Barani Ulaya na Marekani Akothee ameipa ziara hiyo jina la Akothee World Tour ambayo itaanza Julai 2, mwaka wa 2022 huko Munich nchini Ujerumani. Ziara hiyo inatarajiwa kupita kwenye miji mbalimbali ikiwemo Stuttgart, Ujerumani tarehe 30 Julai, na Jonkoping, Sweden Julai 30 mwaka wa 2022. Tour hiyo pia inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Marekani,Dubai, Nigeria, Tanzania, Uganda, Kenya, na Afrika Kusini ila Akothee ameahidi kuweka wazi tarehe rasmi ambayo ataanza ziara yake hiyo kwenye nchi hizo.

Read More