Akothee Aachia Rasmi EP Yake Mpya

Akothee Aachia Rasmi EP Yake Mpya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina “Tatu Bora”, kazi ambayo imeimbwa kwa lugha ya Dholuo. Tatu Bora EP ina jumla ya ngoma tatu kali, ambazo zote amezifanya bila kolabo na msanii yeyote, ikiwa ni hatua inayoonyesha ubunifu na ubora wake binafsi. Nyimbo zilizopo ndani ya EP hiyo ni Bi Mos, Tururu, na Koyo, na zinapatikana exclusive katika majukwaa yote ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni. Kupitia ujumbe wake kwa mashabiki, Akothee ameeleza kuwa ameachia kazi hii kama zawadi kwa wafuasi wake na kama msukumo kwa wanawake, akisisitiza kuwa katika ulimwengu wa ndoa na changamoto zake, muziki unaweza kuwa tiba na faraja. “Tatu Za Bora EP” ni kazi ya kwanza kutoka kwa Akothee tangu atoke hospitalini ambako alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya tumbo.

Read More
 Akothee Atoka Hospitalini Baada ya Matatizo ya Tumbo

Akothee Atoka Hospitalini Baada ya Matatizo ya Tumbo

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo, Akothee, ameibuka na taarifa njema kwa mashabiki wake baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini kufuatia kulazwa kwa muda kutokana na matatizo ya tumbo. Akizungumza mara baada ya kutoka hospitalini, Akothee ametoa shukrani za dhati kwa wote waliomuombea apone haraka na waliomtumia salamu za faraja wakati wa kipindi hicho kigumu. Ameeleza kuwa maombi na upendo wa mashabiki wake yamempa nguvu na matumaini makubwa ya kupona. Hata hivyo, amewashangaza wengi baada ya kufichua kuwa kulikuwa na baadhi ya watu waliotumia mitandao ya kijamii kumtakia mabaya, akiwemo wanaodaiwa kumtakia kifo. Amesema tukio hilo halikumvunja moyo, bali limempa sababu zaidi ya kuthamini wale wanaomuunga mkono kwa dhati. Akothee alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kukumbwa na matatizo ya tumbo yaliyomfanya kupata maumivu makali. Kwa sasa, anasema afya yake imeimarika na ameanza kuendelea vyema chini ya uangalizi wa madaktari.

Read More
 Akothee Akimbizwa Hospitalini Baada ya Maumivu Makali ya Tumbo

Akothee Akimbizwa Hospitalini Baada ya Maumivu Makali ya Tumbo

Mwanamuziki kutoka Kenya, Akothee, amefichua tukio la kutisha alilopitia alfajiri ya jana baada ya kuanguka chooni kutokana na maumivu makali ya tumbo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amesema kuwa hali hiyo ilianza usiku wa manane baada ya kushuhudia video ya kutisha ya msichana aliyekuwa nyumbani kwake. Amesema tukio hilo lilimshtua kiasi cha kumsababishia maumivu makali, kutapika, kuharisha, na hisia za woga ambazo zilimfanya kushindwa hata kulala. Akothee ameeleza kuwa maumivu yalimfanya kulala ndani ya choo kwa kujaribu kupunguza hali hiyo. Amesema kufikia saa tisa asubuhi, nguvu zake zilimwishia na akaanguka sakafuni huku akijaribu kufika chumbani kwa watoto wake akiwa analia kwa maumivu makali. Mwanamama huyo amesema watoto wake walimpata akiwa amelala chooni na mara moja walimkimbiza hospitalini kupitia kitengo cha dharura. Amedai familia yake ilikabiliana na changamoto ya kupokea matibabu haraka baada ya muuguzi kuonyesha ukatili na kutokuwa na huruma. Hata hivyo Akothee amesema baada ya jitihada hizo, hatimaye alipatiwa matibabu na sasa anaendelea kupona, ingawa tukio hilo limemuacha akiwa na hofu kubwa.

Read More
 Msanii Akothee Afunguka Kuhusu Mipango Yake ya Mazishi

Msanii Akothee Afunguka Kuhusu Mipango Yake ya Mazishi

Mwanamuziki kutoka Kenya, Akothee, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutoa tamko jipya kuhusu mipango yake ya mazishi. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, ameeleza kuwa hataki chakula chochote kipikwe siku ya mazishi yake, akisisitiza kuwa watu wanaohudhuria wanapaswa kubeba chakula chao kutoka nyumbani badala ya kutegemea familia yake. Akothee amehoji ni vipi watu wanaweza kumudu kula kwenye mazishi, akiongeza kuwa yeyote anayetaka kula siku hiyo anapaswa kuchangia gharama mapema na kula nyumbani kwao. Mwanamama huyo, amesema wazi kuwa hafurahishwi na utamaduni wa baadhi ya watu kutumia mazishi kama fursa ya kula na kunywa badala ya kutoa heshima kwa marehemu. Kauli yake inakuja siku chache baada ya kueleza kuwa atakapoaga dunia angependa kuzikwa ndani ya saa 48, bila kujali mahali atakapofia, akisisitiza kuwa hataki mchakato wa mazishi wake ucheleweshwe.

Read More
 Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Akothee Aeleza Namna Magonjwa Yalivyobadilisha Maisha Yake

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Akothee, amefunguka kuhusu mabadiliko makubwa kwenye maisha yake baada ya kugunduliwa na matatizo ya kiafya yakiwemo mashambulizi makali ya kichwa (migraine), damu kuganda, na fibroids. Kupitia ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Anasema hali hizo zimemlazimisha kupunguza kasi na kubadili mtazamo wake kuhusu maana ya nguvu na maisha. Akothee amesema changamoto hizo zimemfundisha kuwa nguvu ya kweli si kupambana kila wakati, bali ni kujipa nafasi ya kupumzika na kupona. Ameeleza kuwa sasa anaheshimu mwili wake zaidi, anaepuka presha zisizo za lazima, na kutilia mkazo amani na utulivu kama tiba yake kuu. Aidha, amewatia moyo wanawake wengine wanaopitia changamoto za kiafya kimyakimya, akisema hawapaswi kuona hali hizo kama udhaifu, bali kama safari ya mabadiliko na ukuaji.. Ameongeza kuwa sasa anaheshimu zaidi mwili wake na kuepuka presha zisizo za lazima. Kwa ucheshi wake wa kawaida, Akothee ametaniana na wafuasi wake akisema wanaweza kumuita “Fibroids, Migraines, Bloodclot Akoth Kokeyo,” huku akisisitiza kwamba upendo wa kweli ni ule unaoonyeshwa mtu akiwa hai, na kwamba huu ni wakati wake wa kuthamini utulivu.

Read More
 Akothee Akosoa Vikali Wanaodhihaki Maumbile ya Raila Odinga Junior

Akothee Akosoa Vikali Wanaodhihaki Maumbile ya Raila Odinga Junior

Msanii kutoka Kenya, Akothee, ameonyesha masikitiko makubwa kufuatia dhihaka zinazomlenga Raila Odinga Junior, mwana wa hayati Raila Amolo Odinga, baada ya picha na video kusambaa mitandaoni zikionyesha baadhi ya watu wakicheka maumbile yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amelaani vikali tabia ya baadhi ya watu kutumia mitandao vibaya kwa kumkejeli Junior kutokana na maumbile yake. Amesema kizazi cha sasa kimepoteza utu, heshima na huruma, na kwamba baadhi ya vijana wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kutokana na malezi duni. Msanii huyo amesema kuwa matendo kama hayo yakiachwa bila kudhibitiwa yanaweza kuchochea unyanyasaji hata kwa watu wenye ulemavu mitaani. Amesisitiza kuwa vijana wanaohusika lazima wachukuliwe hatua za kisheria ili wajifunze kuishi kwa heshima na utu katika jamii. Aidha, Akothee amemtumia ujumbe wa faraja Raila Junior, akimtaja kama shujaa anayestahili upendo na heshima kutoka kwa Wakenya. Pia amempongeza Mama Ida Odinga kwa uvumilivu wake na kuahidi kupigania heshima ya familia hiyo, akisema yuko tayari kushughulikia suala hilo kwa ukaribu. Kauli ya Akothee imezua mjadala mkubwa mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa kusimama kidete dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni.

Read More
 Akothee Asema Hawezi Kuolewa na Mwanaume wa SDA

Akothee Asema Hawezi Kuolewa na Mwanaume wa SDA

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, amezua mjadala mitandaoni baada ya kutoa matamshi yenye utata kuhusu wanaume wa Kanisa la Waadventista (SDA). Kupitia video aliyoiposti kwenye mitandao yake kijamii, amesema kuwa hawezi kamwe kuolewa na mwanaume kutoka kanisa hilo kwa kuwa wanaume wengi wa SDA ni wakali na wenye masharti mengi kuhusu maisha ya kila siku, jambo analoliona haliendani na mtindo wake wa maisha. Mwanamama huyo ameongeza kuwa hawezi kuishi kwenye ndoa inayomnyima uhuru wa kufurahia maisha, akitaja mambo kama kunywa mvinyo na kula nyama kuwa sehemu ya starehe anazopenda. Hata hivyo amesema kuwa licha ya yeye mwenyewe kuwa Mwaadventista, bado hawezi kumpendekeza mtu kuolewa na wanaume kutoka dhehebu hilo.

Read More
 Akothee Aandika Ujumbe wa Tumaini kwa Mashabiki

Akothee Aandika Ujumbe wa Tumaini kwa Mashabiki

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu wa Kenya, Akothee, ameandika ujumbe wa matumaini kwa mashabiki kupitia ukurasa wake wa Instagram akisimulia safari yake ya maisha iliyojaa changamoto na mafanikio yaliyotokana na bidii, nidhamu, na imani. Katika ujumbe huo, Akothee amekiri kuwa hakuwahi kuaminiwa na watu wengi alipokuwa akikua. Amesema kwamba hata katika mambo madogo kama masomo na ndoa yake ya awali kijijini, watu hawakuona mustakabali mkubwa kwake. Ameongeza kuwa licha ya wenzake kumzidi kwa hatua, aliendelea kuwashangilia kwa moyo mkunjufu na kusherehekea mafanikio yao bila wivu. Amesema kuwa sasa anajivunia kuona maisha yake yakiwa kwenye mstari, si kwa sababu kila kitu kiko sawa, bali amejifunza nidhamu na uthabitii unaomwezesha kukabiliana na changamoto za kila siku. Mwanamama huyo amesisitiza kuwa uvumilivu umemjenga, neema imembeba, na imani yake kwa Mungu imekuwa nguzo kuu ya mafanikio yake. Hata hivyo amehitimisha ujumbe wake kwa kueleza kuwa Mungu wake ni Mungu wa kuishi, akiwatia moyo mashabiki wake kutokata tamaa licha ya magumu wanayopitia.

Read More
 Akothee Amkingia Kifua Azziad Dhidi ya Wakosoaji wa Mitandaoni

Akothee Amkingia Kifua Azziad Dhidi ya Wakosoaji wa Mitandaoni

Mwanamuziki, Akothee, amejitokeza kumtetea TikTok queen na mtangazaji Azziad Nasenya baada ya kuvamiwa mitandaoni kwa madai ya kuishi maisha ya kuigiza. Kupitia waraka wake Instagram, Akothee ameeleza kuwa anampenda na kumheshimu Azziad kwa kuwa na ndoto kubwa na kuonesha ujasiri wa kukimbizana na maisha. Amesisitiza kuwa hatua ya mrembo huyo kupata mkopo wa millioni 25 za Kenya na kununua nyumba akiwa na umri wa miaka 25 ni jambo la kupongezwa na si kulaumiwa, kwani ni nadra vijana kufanikisha mambo makubwa wakiwa na umri mdogo. Amesema kuwa wakati vijana wa rika la Azziad leo wanajitahidi kujenga maisha yao, wengi wa kizazi kilichomtangulia walihangaika na changamoto kubwa kama ndoa zilizoshindikana, kulea watoto peke yao na hata kutokuwa na akaunti ya benki wala ajira. Kwa maoni yake, hatua ya Azziad kuwekeza katika nyumba ni mfano bora wa kuchukua jukumu la maisha yake mapema. Akothee pia amekosoa wanaume wanaoendelea kumsema vibaya Azziad mitandaoni ilhali wao bado wanashindwa hata kumudu mikopo midogo. Kwa mtazamo wake, badala ya kumkosoa, Wakenya kwa jumla wana nafasi ya kujifunza kutoka kwake. Hata hivyo amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa Azziad ni msichana mwenye ndoto kubwa, anayeendelea kujijenga na kuwa chanzo cha msukumo kwa vijana wengi, na kwamba jamii inapaswa kusherehekea ujasiri wake badala ya kumshusha

Read More
 Akothee Alazwa Hospitalini Baada ya Kuteseka kwa Miezi Miwili

Akothee Alazwa Hospitalini Baada ya Kuteseka kwa Miezi Miwili

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini, Esther Akoth maarufu kama Akothee, amefichua kuwa amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali kwa zaidi ya miezi miwili na hatimaye amelazwa hospitalini tangu Jumatatu wiki hii. Kupitia waraka mrefu kwenye Instagram, Akothee alieleza kuwa maisha yake yamekuwa ya faragha kiasi kwamba mashabiki wake hawakujua hali yake ya kiafya hadi alipoamua kufunguka. Alisema alijisukuma kupita kiasi licha ya kubeba maumivu kwa zaidi ya miezi miwili. Shida hiyo ilijitokeza zaidi wakati wa mtihani wa pili ambapo ghafla akili yake iliganda, karatasi ya mtihani ikaonekana kumlemea na akaanza kuhisi kichefuchefu. Akiwa Homa Bay, alikiri kuwa alitegemea dawa za kupunguza maumivu na za kulegeza misuli ili kuendelea na majukumu yake, akiwemo kumalizia ratiba aliyokuwa ameahidi mashabiki wake. Hata hivyo, alipata shambulio jingine kali wakati alipotarajia kuruhusiwa kuondoka hospitalini, hali iliyomlazimu kuendelea kupata uangalizi wa karibu. Ujumbe wake umeonyesha ni kwa namna gani alijitolea kukamilisha majukumu yake licha ya hali ngumu ya kiafya, jambo lililoibua mjadala mkubwa kuhusu shinikizo la kazi na athari zake kwa wasanii na viongozi wa kijamii. Mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi kumtakia nafuu ya haraka, huku wakimsifu kwa ujasiri wa kuendelea kusimama imara licha ya changamoto alizopitia.

Read More
 Akothee Avunja Ukimya Baada ya Kukosolewa Kuhusu Mavazi

Akothee Avunja Ukimya Baada ya Kukosolewa Kuhusu Mavazi

Mwanamuziki wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee, amejibu vikali ukosoaji unaoendelea mitandaoni kuhusiana na mavazi aliyovaa katika tukio la hivi karibuni huko Homa Bay. Kupitia mitandao ya kijamii, Akothee alisisitiza kuwa hana jukumu la kuwa mfano wa kuigwa kwa mtu yeyote na kwamba anapaswa kuachiwa aishi maisha yake kwa namna anayoona inafaa. Akothee alisema licha ya mashambulizi ya maneno anayopokea, bado ataendelea kushiriki katika matukio anayoalikwa na kufanya maonyesho kwa mtindo wake wa kipekee. Mwanamuziki huyo ameendelea kusisitiza kuwa maamuzi yake ya kisanii na binafsi hayapaswi kupimwa kwa kipimo cha maadili ya mtu mwingine, akiwataka wakosoaji waache kumfuatilia kwa matarajio yasiyoendana na mtindo wake wa maisha. Kauli ya Akothee imeibua mjadala mitandaoni, ambapo wafuasi wake wamegawanyika kati ya wanaomuunga mkono kwa kusimamia haki yake ya kujieleza na wale wanaoamini kuwa umma una haki ya kumkosoa kutokana na hadhi yake kama msanii maarufu. Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya picha na video za Akothee akiwa katika vazi lililoibua hisia kali kusambaa mitandaoni, na kusababisha mjadala mkubwa kuhusu mipaka ya uhuru wa msanii na matarajio ya jamii

Read More
 Mashabiki Wamkemea Akothee kwa Kudharau Kazi ya Fundi

Mashabiki Wamkemea Akothee kwa Kudharau Kazi ya Fundi

Msanii nyota wa Kenya, Akothee, amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoa kauli kali iliyotafsiriwa kama dharau kwa fundi aliyemtengenezea meza. Kauli yake kwamba meza hiyo “inafanana na jeneza”, imechukuliwa na mashabiki kama ya kudhalilisha na kukosa heshima kwa mafundi wanaojituma kujitafutia riziki. Mashabiki waliitaja kauli hiyo kuwa ya kuumiza na kukosa utu, wakimtaka msanii huyo kuheshimu bidii ya mafundi wanaojituma licha ya changamoto. “Hata kama hukupenda kazi, si lazima kumdhalilisha mtu. Huo ni ukatili,” aliandika shabiki mmoja. Wengine walimtaka Akothee kutumia umaarufu wake kuhamasisha heshima kwa watoa huduma wa kawaida badala ya kuwavunjia hadhi hadharani. Pia, walihimiza mawasiliano ya moja kwa moja na ya staha kama njia bora ya kushughulikia changamoto za kibiashara. “Umaarufu haumpi mtu ruhusa ya kumshusha mwingine hadharani. Wafanyakazi wa mikono wanastahili heshima pia,” aliongeza mwingine Hadi sasa, Akothee hajatoa tamko lingine zaidi ya kauli yake ya TikTok, huku mjadala ukiendelea kushika kasi mitandaoni na wengi wakimtaka azingatie lugha na heshima anapotoa mrejesho kwa umma. Mzozo huo ulianza baada ya fundi seremala kumuanika Akothee kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa hajalipwa salio la kazi yake, licha ya kumkabidhi meza aliyokuwa ameagiza. Katika kujibu kupitia TikTok Live, Akothee alidai tayari alimlipa fundi huyo asilimia 80 ya malipo lakini kazi aliyopokea haikukidhi matarajio yake. “Nilimlipa 80%, lakini kazi si ya kiwango nilichotaka. Aichukue tu, hiyo meza inafanana na jeneza,” alisema Akothee mbele ya mashabiki wake mtandaoni.

Read More