Bahati apewa tuzo ya heshima Youtube

Bahati apewa tuzo ya heshima Youtube

Staa wa muziki nchini Bahati ametunukiwa tuzo ya Golden Plaque na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers millioni moja kwenye channel yake. Bahati ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi. Channel ya youtube ya Bahati  ilifunguliwa rasmi Joined Agosti 7, mwaka 2012 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 193,565,094 huku ikiwa na jumla ya subscribers 1,090, 000. Bahati ni msanii wa pili nchini Kenya kupokea golden Plaque baada ya Otile Brown ambaye alikuw msanii wa kwanza nnchini kufikisha jumla y wafuatiliaji million moja YouTube. Itakumbukwa tuzo ya Golden plaque imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.

Read More
 Bahati athibitisha kufanya kolabo na Nick Minaj

Bahati athibitisha kufanya kolabo na Nick Minaj

Mwanamuziki wa Kenya Bahati amethibitisha kufanya kazi ya pamoja na Rapa kutoka Marekani Nicki Minaj. Bahati ameweka taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram akifichua kuwa wataachia rasmi wimbo wao mwaka 2023. “2023, Bahati na Nicki Minaj imethibitishwa..,” ameandika kupitia Insta stori yake. Baadhi ya Mashabiki wametilia shaka habari hizo ikizingitiwa kuwa mwanamuziki huyo amekuwa akijihusisha sana na kiki kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari. Kwa upande mwingine baadhi wamesema kuwa taarifa ya Bahati kufanya kolabo na Nicki Minaj inaweza kuwa na ukweli kwa sababu amekuwa akifanya kazi kwa bidii kwenye muziki wake. Hata hivyo mashabiki wake sasa wanasubiri kwa hamu 2023 wakiwa na matumaini makubwa kuwa wimbo huo utakuwa mkali zaidi . Nicki Minaj ambaye ni mmoja wa marapa bora zaidi wa kike duniani, kolabo hii na Bahati ikitoka inakuwa ni kolabo yake ya pili kushirikishwa na mwanamuziki toka Afrika baada ya Davido (Nigeria) kwenye wimbo “Holy Ground” uliotoka mwaka 2020.

Read More
 Bahati kufunga ndoa Novemba 30 mwaka huu

Bahati kufunga ndoa Novemba 30 mwaka huu

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Bahati ameashiria kufunga pingu za maisha na mama ya watoto wake Diana B mwishoni mwa mwezi huu. Bahati amedokeza hayo kwa picha ya kupitia ukurasa wake wa Instagram na kisha kuweka ishara ya pete ya ndoa ambayo ameambatanisha na ujumbe unaotaja tarehe 30/11 kufanya jambo la kihistoria. “30TH NOVEMBER 2022 ”, Ameandika. Hata hivyo ujumbe huo umezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wamedai huenda Bahati akahalalisha ndoa yake na Diana B kwa njia ya harusi huku wengine wakihoji ni ujio wa ngoma yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia siku hiyo. Ikumbukwe kwa sasa Bahati anafanya vizuri na singles zake mbili “My Beginning” na “Mambo ya Mhesh Remix” ambayo amemshirikisha Sosuun pamoja na Ssaru.

Read More
 Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Msaniii na  mwanamitandao maarufu kutoka Kenya Diana Marua amefunguka juu ya video iliyosambaa mtandaoni akikiri kuwa alitembea na wanaume wengi kimapenzi kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi. Kupitia ujumbe mrefu aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Diana amesema aliweka wazi suala hilo kwa umma kwa lengo la kuwapa moyo vijana wanaopitia masha magumu. Lakini pia amewahimiza watoto wa kike kutokata tamaa kwenye ndoto zao na badala yake watie bidii kwani muda wao wa kupata mafanikio utafiki. Diana Marua ameongeza kuwa kama balozi mwema katika jamii anapaswa kuzungumzia magumu aliyoyapitia kwenye maisha yake badala ya kuangazia mazuri tu. Diana alichapisha video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii  mwaka 2020 wakati alipokuwa akipokea gari jipya aina Mercedes Benz alilozawadi na mume wake Bahati. Alikumbuka kipindi alikuwa anaishi maisha ya uchochole ambapo alilazimika kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya kupata pesa lakini pia kuendesha magari ambayo hakuwa anaweza kumudu wakati huo. Kwa sasa Diana ana hesabu baraka zake kama Mama ya watoto watano, Mke na mtengeneza maudhui kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 Diana B azua gumzo mtandaoni baada ya video yake akikiri kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kusambaa

Diana B azua gumzo mtandaoni baada ya video yake akikiri kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kusambaa

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wametoa maoni mbali kuhusu video ya Diana Marua akiri hadharani kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya pesa. Diana alichapisha video hiyo mwaka 2020 mtandaoni ambapo alidai kwamba kabla ya kukutana na mume wake Bahati alikuwa anachepuka na wanaume wengi kwa lengo la kukidhi mahitaji yake ya msingi. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi ana umri wa miaka 20 pesa haikuwa shida kwake kwani kila mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano naye alikuwa anamhudumia ipasavyo ikiwemo kumlipia kodi sambamba na kumnunulia chakula na mavazi. “I dated guys for money I had people who used to give me 10k, kuna mtu anakupatia 30k, anakupea 20k, nilikuwa na mtu wa kunifanyai shopping ya nyumba , nilikuwa na mtu wa kuni buyia manguo , unajua All I wanted was to live well..”, Alisema Video hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya ambapo wengi wamehoji kuwa Diana B bado ana tamaa ya pesa na huenda akamkimbia bahati ikitokea amefilisika kiuchumi. Hata hivyo wengine wamesema kuwa watu waache kumhukumu mwanamama huyo wa watoto watatu kwa kuwa amebadili mienendo yake ya zamani ikizingatiwa kuwa ametulia na analea familia ya mwimbaji huyo.

Read More
 Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Seed amefichua kuwa waliamua kumaliza ugomvi wao na Bahati kwa manufaa ya watoto wao. Kwenye mahojiano na World IS, Mr. Seed amesema watoto wao walikuwa wakishambuliwa kila mara kwenye mitandao ya kijamii kutokana na utofauti wao kimuziki, kitendo kilichowalazimu kukutana na kuweka kando uhasama wao ambao ungeathiri ukuaji wa watoto wao katika siku za mbeleni. “Nilikuwa nikiposti picha za mtoto wangu Gold na mashabiki wenye roho chafu walikuwa na mazoea ya kumlinganisha na mtoto wa Bahati Majesty. Hilo pia lilitokea kwa upande wa Bahati na watoto wetu wangeishia kutusiwa,” Alisema. Mr. Seed na Bahati ambao walikuwa marafiki wa karibu, walitofautiana mwaka 2018 baada ya wake zao Diana Marua na Nimo Gachuiri kukosa maelewano katika hafla ya mkesha wa mwaka mpya. Kwa mujibu wa mashuhuda, Diana alipinga wazo la Nimo la kuuza kahawa na vitafunio kwenye sherehe hiyo na aliishia kuwapigia simu polisi kumuondoa Nimo ambaye kwa wakati huo alikuwa mjamzito mzito.

Read More
 Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Bahati akerwa na kitendo cha mashabiki kumuita mheshimiwa

Msanii nyota nchini Bahati amewaonya mashabiki dhidi ya kumuita Mheshimiwa ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu ashindwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu. Kupitia mitandao yake ya kijamii hitmaker huyo wa Adhiambo ameshangazwa na kitendo cha watu kumhusisha na jina hilo kila mara huku akiwataka kutumia jina la Bahati ambalo amekuwa akilitumia kwenye muziki “Sielewi Mbona Bado Watu Wananiita MHESH… Niiteni tuu Bahati Please.” Ameandika Instagram. Lakini pia Bahati amewataka mashabiki kuacha kumhusisha na siasa kwa sababu amerudi kwenye shughuli ya muziki ambayo amekuwa akifanya kwa muda mrefu. “Hii Mambo Ya Mhesh Wekeni Kando…. THE KING IS BACK!!! Tell Me. What Happened While I Was Away???”, Ameongeza. Bahati ambaye alikuwa kimya kwa miezi miwili baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Mambo ya Mhesh” Utakumbuka Bahati alikuwa anawania kiti cha ubunge Mathare kupitia tiketi ya chama cha jubilee lakini alishindwa na mpenzani wake Anthony Oluoch wa chama cha ODM.

Read More
 Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Couple pendwa nchini inayoundwa na wasanii Diana B pamoja na Bahati imetangaza jinsia ya mtoto wao wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni. Katika hafla ya kutambulisha jinsia ya mtoto huyo wawili hao wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kiumemuda wowote kuanzia sasa Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni mkaribisha mtoto wao wa watatu. Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni kwamba huenda Diana B amejifungua kwa siri kutokana na jumbe zenye ukakasi alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.

Read More
 Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Ringtone afunguka sababu za kuwaponda Willy Paul na Bahati

Hitmaker wa Ombi Langu, Ringtone Apoko amefunguka sababu ya kuwakosoa wasanii Willy Paul na Bahati kila mara kwenye majukwaa mbali mbali. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema wawili hao walimvunjia heshima mwenyezi Mungu kwa kutumia vibaya kiwanda cha muziki wa injili kwa ajili ya kujilimbikizia mali na kisha wakageukia muziki wa kidunia. Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo cha Willy Paul na Bahati kutumia njia haramu kuchuma mali wanayomiliki kwa sasa imewaponza kisanaa kiasi cha kutopata mafanikio kwenye muziki wao. Katika hatua nyingine Ringtone ametetea utajiri wake kwa kusema kuwa ana vyanzo vingi halali vinavyomuinguzia kipato huku akikanusha tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya ulanguzi wa pesa kwani inakwenda kinyume na maandiko matakatifu.

Read More
 Bahati amkataa Raila Odinga, akiri uchaguzi mkuu nchini Kenya ulikumbwa na dosari

Bahati amkataa Raila Odinga, akiri uchaguzi mkuu nchini Kenya ulikumbwa na dosari

Staa wa muziki nchini Bahati amefunguka sababu za kudinda kuchukua kazi ambayo kinara wa Azimio Raila Odinga aliahidi kumpa pindi atakapotua uongozi wa nchi kwenye uchaguzi uliokamilika. Bahati amesema alijua kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ungekumbwa na dosari na ndio maana akaendelea na azma yake ya kuwania ubunge Mathare licha ya kushurutishwa kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho. Katika hatua nyingine Hitmaker huyo wa “”Adhiambo anaamini kuna siku jamii ya Kamba itamtoa rais ambaye ataongoza taifa la Kenya licha ya Odinga kumtumia vibaya Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa na nyota ya kuiongoza jamii hiyo. Hata hivyo Bahati ambaye amesisitiza kuwa atakuwa kwenye kinyanganyiro cha urais mwaka 2037 amejinasibu kuwa hajutii kitendo cha kukosa ubunge Mathare kwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao wapo ndani ya serikali.

Read More
 Ringtone aanika siri za Bahati, Adai yupo mbioni kuja na EP mpya

Ringtone aanika siri za Bahati, Adai yupo mbioni kuja na EP mpya

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko amefunguka tusiyoyajua kuhusu ukimya wa Bahati kwa kusema kwamba amekuwa chimbo akiandaa EP yake mpya. Kulingana na Ringtone hatua ya Bahati kufuta kila kitu kwenye ukurasa wake wa Instagram ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya ujio wa EP hiyo ambayo ina jumla ya nyimbo 6. Katika hatua nyingine Ringtone amewataka mashabiki kumweka Bahati kwa maombi kwa sababu mkali huyo wa ngoma ya “Adhiambo” amekuwa na msongo wa mawazo tangu ashindwe kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare. Bahati amekuwa kimya baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kukamilika nchini Kenya, jambo ambalo liliwaacha mashabiki zake na maswali mengi kiasi cha kutaka kufahamu ni nini hasa kimemsibu msanii huyo.

Read More
 BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUFUTA KILA KITU INSTAGRAM

BAHATI AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUFUTA KILA KITU INSTAGRAM

Staa wa muziki nchini Bahati amefuta picha na video zake kwenye mtandao wa Instagram, hatua iliyohisiwa ni ujio wake mpya. Hatua hii ya Bahati imevuta hisia za baadhi ya mashabiki ikihisiwa kuwa huenda akaachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kukaa kimya tangu apoteze kiti cha ubunge mathare kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika nchini kenya. Uamuzi wa Bahati hakujali hata picha alizopiga na mke wake, Diana B huku upande mwingine ikihisiwa kuwa pengine kuna kingine kisichohusiana na ujio wa kazi kutoka kwake. Utakumbuka juzi kati Bahati alifunguka kuwa familia yake ipo njia panda ambapo aliwataka mashabiki kumweka kwenye maombi pamoja na mke wake Diana ambaye alikuwa mbioni kujifungua.

Read More