BAHATI AMSHAURI MUNA LOVE ASIBADILI DINI KUTOKA UKRISTO KWENDA UISLAMU
Baada ya Muigizaji na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania Muna Love kuweka wazi matamanio yake ya kubadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Staa wa muziki nchini Bahati ameonekana kutofautiana kimawazo na mrembo huyo. Kupitia comment aliyoachia kwenye post ya Muna Love kwenye mtandao wa Instagram Bahati amemshauri mrembo huyo abaki katika dini yake ya Ukristo kwa kudai kuwa njia ya wokovu ina mambo mengi. Kauli ya Bahati imekuja siku moja baada ya Ali Kiba kuahidi kuhakikisha kuwa mrembo huyo ana stirika katika dini ya Uislamu ambapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa atashirikiana nae vyema katika kumbadili endapo atakuwa tayari kufanya hivyo. Ikumbukwe kuwa miaka kadhaa nyuma Muna Love alitangaza kuokoka na kuwa Mlokole ambapo amekuwa akitumia nafasi hiyo pia kuwashawishi watu wengine kuingia katika dini yake hiyo.
Read More