Waandishi wa nyimbo za Bebe Cool ni bandia – King Saha
Mwanamuziki King Saha ameibuka na kuwachana watu wanaomuanndikia Bebe Cool nyimbo kwa kusema kwamba hawana vipaji kwenye masuala ya uandishi. Kwenye mohajiano yake hivi karibuni King Saha amesema Bebe Cool amewekeza mamilioni ya pesa kwa waandishi wa nyimbo ilhali kazi zake zinachuja haraka. Aidha ameenda mbali Zaidi na kujinadi kuwa huwa anaandika nyimbo 5 kwa mwaka na zote zinaisha kuwa kubwa zaidi kwenye tasnia ya Afrika Mashariki. Baadhi ya waandishi wa nyimbo wanaofanya kazi kwa ukaribu na Bebe Cool ni pamoja na Yese Oman Rafiki na Ronnie On Dis One. Utakumbuka Bebe Cool na King Saha hawajakuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu na ugomvi wao ulianza kipindi ambacho Bebe Cool alimshauri hitmaker huyo wa Zakayo aachane na matumizi ya mihadarati kwa kuwa itampoteza kimuziki. Tangu wakati King Saha amekuwa akimrushia vijembe Bebe Cool kila mara anapopata nafasi kwenye mahojiano yake mbali mbali.
Read More