KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

KING SAHA MBIONI KUFUNGA NDOA MBELE YA HASIMU WAKE BEBE COOL

Inaonekana Ugomvi wanamuziki King Saha na Bebe Cool kutoka uganda hautamalizika hivi karibuni. Hii ni baada ya king saha kuibuka na kumtolea uvivu msanii mwenzake Bebe Cool akidai atafanya harusi mbele ya msanii huyo licha ya kuwa anamzidi kiumri. Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amesema ni aibu kwa mtu kama Bebe Cool kutohalalisha ndoa yake kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa ana umri mkubwa kumshinda. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Zakayo” amesema atafunga harusi hivi karibuni mara baada ya ujenzi wa nyumba yake kukamilika. King Saha amesema licha ya kuwa ana mpango wa kuhalalisha ndoa yake hivi karibuni, hatamweka wazi mke wake kwa umma kwa faida ya amani yake ya akili. “Bebe Cool was singing when I was in P.1. He is a very old man but stuck in the skin of a young man. I’m sure even my wedding will come before his. I will wed my wife immediately after completing my house,” Amesema King Saha Mjengo wa kifahari wa King Saha umekamilika kwa asilimia 80 na nyumba yake hiyo ipo maeneo ya Nakawuka, katika wilaya ya Wakiso nchini Uganda.

Read More
 BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

BEBE COOL AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU BIFU YA KING SAHA NA ALLAN HENDRICK.

Bebe Cool amekuwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka 20 bila kupoa. Ni moja kati ya wasanii wakongwe ambao wakiongea chochote kila mtu kwenye tasnia muziki nchini Uganda anamsikiliza licha ya maisha yake kuandamwa na kashfa nyingi. Msaniii huyo ametoa wito kwa kijana yake Allan Hendrik na King Saha wajitenge na vita vya maneno na badala yake wafanya muziki mzuri Hitmaker huyo wa Gyenvudde amesema wawili hao wanapaswa kuelekeza nguvu zao zote kwenye muziki kwani kutupia maneno makali mtandaoni kutawapoteza kimuziki huku akitoa angalizo kwa King Saha aache kutumia dawa za kulevya. “They have time to be productive because they are still young. They should focus on releasing music, they shouldn’t go after one another. I just want to  King Saha stay away from drugs,” Amesema kwenye mahojiano yake hivi karibuni. Mapema wiki hii , Allan Hendrick alithibitisha kuwa hana ugomvi wowote na King Saha licha ya wimbo wake uitwao  ‘matayo’ kuonekana kumlenga moja kwa moja msanii huyo.

Read More
 BEBE COOL AFUNGUKA MPANGO WA KUMALIZA BIFU YAKE NA BOBI WINE

BEBE COOL AFUNGUKA MPANGO WA KUMALIZA BIFU YAKE NA BOBI WINE

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu suala la kumaliza ugomvi wake na msanii aliyegeukia siasa nchini humo Bobi Wine. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool ameweka wazi matamanio yake ya kuzika tofauti zake na Bobi Wine kwa manufaa ya tasnia ya muziki ya nchini uganda wakiwemo mashabiki na wananchi kwa ujumla. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Genyvudde” amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kuleta amani kwa kupunguza chuki miongoni mwa wafuasi wao. Licha ya kuweka wazi mpango wake huo Bebe Cool amesema hilo litafanyika tu iwapo Bobi Wine atamuomba baba yake msamaha kwa kuvunjia heshima kipindi cha nyuma. Utakumbuka Bebe Cool na Bobi Wine kipindi cha nyuma walikuwa marafiki wakubwa kwenye muziki wao lakini walikuja wakakosana na kila mmoja akaenda kivyake kama msanii wa kujitegemea na tangu wakati huo wamekuwa wakishindana kisiasa, kimuziki na hata kifedha.

Read More
 BEBE COOL ATIA NENO JUU YA SHEEBAH KUDHALALISHWA KINGONO

BEBE COOL ATIA NENO JUU YA SHEEBAH KUDHALALISHWA KINGONO

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amemshauri msanii mwenzake Sheebah kumburuza mahakamani mwanaume aliyemnyanyasa kingono kwenye moja ya performance yake wikiendi iliyopita. Katika mahojiano yake hivi karibuni Bebe Cool amesema mwanaume aliyemdhalilasha sheebah kijinsia alivuka mipaka, hivyo anapaswa kufunguliwa mashtaka ili iwe funzo kwa wanaowanyanyasa wanawake katika jamii. Hata hivyo, amekataa kumuunga mkono Sheebah kwa madai aliyoyaiibua kwa kuwa shutuma za unyanyasaji wa kijinsia zinaweza tu kuthibitishwa na ushahidi uliowasilishwa kwa mamlaka husika. Kauli ya Bebe Cool imekuja mara baada ya Sheebah Karungi kusimulia kisa kilichowagusa wengi kwa kusema kuwa alinyanyaswa kingono na mtu anayeheshimika katika jamii. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nkwata Bulungi (Bailamos)” alikuwa amepangiwa kutumbuiza kwenye sherehe ya mtu huyo ambaye jina lake halikutajwa lakini kabla hajapanda jukwaani, jamaa huyo alifika kwenye gari lake na kuanza kumpapasa bila ridhaa yake.

Read More
 BEBE COOL ABADILI MAWAZO DHIDI YA CINDY SANYU, AMUUNGA MKONO KUTWAA UONGOZI WA CHAMA CHA UMA

BEBE COOL ABADILI MAWAZO DHIDI YA CINDY SANYU, AMUUNGA MKONO KUTWAA UONGOZI WA CHAMA CHA UMA

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool ametangaza hadharani kumuunga mkono Cindy Sanyu kwenye azma yake ya kuongoza chama cha wanamuziki nchini humo licha ya kumkosoa kipindi cha nyuma. Katika mkao na wanahabari Bebe Cool amesema Cindy ndiye anafaaa kuwasimamia wasanii kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kushawishi wadau wa maendeleo pamoja na serikali kutoa pesa za kufadhilia miradi ya muziki lakini pia anazungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha tofauti na mpnzani wake King Saha. Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema Cindy ni kiongozi dhabiti asiye terereka na changamoto zozote ikizingatiwa kuwa kipindi cha corona alisimama kidete kuwatetea wasanii licha ya viongozi wengi wa wanamuziki nchini Uganda kukimbia majukumu yao. Kauli ya Bebe Cool imekuja mara baada ya kumkosoa cindy sanyu mwezi mmoja uliopita kwa kudai kuwa msanii huyo ana roho ya kulipiza kisasi lakini pia ana uwezo wa kustahimili ukosoaji kutoka kwa wapinzani kwa kuwa ni mtu mwenye hasira. Madai hayo ya Bebe Cool yalimuibua Cindy Sanyu na kusema kwamba ataanza mchakato wa kuwaomba msamaha wasanii wote aliowakosea kipindi cha nyuma kama njia moja ya kupata uungwaji kutoka kwa wanamuziki ambao wanapinga azma yake ya kutwaa uongozi wa urais katika chama cha wanamuziki  nchini Uganda.

Read More
 BEBE COOL AWASUTA VIKALI MAPROMOTA NCHINI UGANDA, ATISHIA KUSUSIA SHOWS ZAO

BEBE COOL AWASUTA VIKALI MAPROMOTA NCHINI UGANDA, ATISHIA KUSUSIA SHOWS ZAO

Mwanamuziki kutoka Uganda Bebe Cool amefunguka na kudai kwamba hatokubali kufanya shows anazolipwa kati ya shillingi laki moja na tatu za Kenya. Hii ni baada ya mapromota wa muziki nchini uganda kuanza kuwalipa wasanii wa nigeria shillingi laki 4 za Kenya kwenye matamasha yao ya muziki. Bebe Cool ameonyesha kusikitishwa na mapromota wa muziki nchini humo wanaoendelea kuwapa kipau mbele wasanii wa Nigeria kwenye matamasha ya muziki. Akizungumza kwenye moja ya perfomance yake, Bebe Cool amewataja mapromota hao kama wanafiki, wasiowatakia wasanii wa Uganda mema. Hitmaker huyo ngoma ya “Gyenvude” ameenda mbali zaidi na kuema kwamba kasumba hiyo huenda ikasambaratisha tasnia ya muziki nchini Uganda. Bebe cool amewataka mapromota wa Nigeria kurudisha fadhila kwa wasanii wa uganda kwa kuanza kuwazingatia kwenye shoo zao kwa faida ya tasnia ya muziki ya nchini hizo mbili. “Msanii wa Uganda anapoachia ngoma kali, mapromota huanza kuua brand lakini huwa wanawafuata sana wasanii wa Nigeria. Lakini mapromota wa Nigeria wanapaswa kurudisha fadhila kwa kucheza muziki wetu,” alisema. Bebe Cool aliendelea kwa kusema “Tulijitahidi sana kujenga hii tasnia. Sasa imekua na watu wanatuangalia. Mapromota wanapaswa kututhamini na kuturuhusu kufurahia matunda ya bidii yetu,”

Read More
 BEBE COOL APINGA AZMA YA CINDY SANYU KUWAONGOZA WASANII  WA UGANDA KWA MARA YA PILI

BEBE COOL APINGA AZMA YA CINDY SANYU KUWAONGOZA WASANII WA UGANDA KWA MARA YA PILI

Mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amedai kwamba Cindy Sanyu hapaswi kupigiwa kura kama rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo kutokana na mienendo yake isiyoridhisha. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amesema Cindy ameshindwa kuwaunganisha wasanii nchini uganda lakini pia hapendi kukosolewa kwenye utendakazi wake. Bosi huyo wa Gagamel amedai kwamba cindy ni kiongozi dikteta kitu ambacho  amesema sio kizuri kwa kiongozi kuwa nayo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gyenvudde” amesema Cindy anapotofauti na mtu kimawazo, mtu huyo anakuwa adui wake, hivyo hapaswi kupewa nafasi nyingine ya kuwaongoza wasaniii wa uganda kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni. Hata hivyo ameonekana kumchagua Cindy kuwa rais wa muungano wa wasanii nchini uganda badala ya king saha ambaye kwa mujibu wake ni mvuta bangi. Utakambuka kwenye kinyanganyiro cha kuwania wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda wasanii watatu peke ndio wametia nia ya kugombea wadhfa huo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni. Wasanii hao ni pamoja na Daddy Andre, King Saha na Cindy Sanyu ambaye ndiye rais wa sasa wa muungano wa wasanii nchini Uganda.

Read More
 KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

KING SAHA AMJIBU BEBE COOL KWA KEJELI BAADA YA KUPINGA AZMA YAKE YA KUWA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha amejibu madai yaliyoibuliwa na Bebe Cool kuwa hana vigezo vya kuuongoza muungano wa wasanii nchini humo kutokana na kuathirika pakubwa na matumizi ya dawa za kulevya. Kupitia mitandao yake ya kijamii King Saha ameshare video ya Bebe Cool akimzungumzia vibaya na kuweka caption ya kumshukuru kwa kejeli huku akisema kwamba endapo atachaguliwa kama rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda atamhudumia msanii huyo bila ubaguzi licha ya kumpinga vikali kwenye azma yake ya kuwa kiongozi wa wasanii. King saha ambaye juzi kati alitangaza kuwania wadhfa wa urais kwenye muungano wa wanamuziki nchini uganda anatarajiwa kuchuana na rais wa sasa wa muungano huo Cindy Sanyu kwenye uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya ambao utafanyika hivi karibuni. Tayari aliyekuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda Ykee Benda ameunga mkono azma ya King Saha kuwa rais wa muungano huo kwa kusema kwamba anastahili wadhfa huo licha ya kutokuwa maadili mema kama baadhi ya watu wanavyosema mitandaoni.

Read More
 BEBE COOL AFUNGUKA KUHUSU KUSTAAFU MUZIKI

BEBE COOL AFUNGUKA KUHUSU KUSTAAFU MUZIKI

Mwanamuziki kutoka Uganda Bebe Cool amefunguka na kudai kwamba hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni kwani ana miaka 20 ya kufanya hivyo. Kwenye moja ya onesho lake huko Kawempe Bebe Cool amesema ndio mwanzo anaanza safari yake ya muziki hivyo mashabiki watarajie muziki mzuri kutoka kwake. “Majuzi niliambia Chameleone kuwa nina mpango wa kustaafu muziki miaka 20 ijayo na akaanza kuachia muziki maana alikuwa amelaza damu.”..Amesema Bebe Cool Bebe Cool ambaye ana umri wa miaka 40 ametoa changamoto kwa wasanii wachanga kutia bidii kwenye kazi zao maana wasanii wakongwe hawana mpango wa kuacha muziki. Utakumbuka Bebe Cool ni  mmoja kati ya wasanii wakongwe kwenye muziki nchini Uganda kwani amekuwa kwenye game ya muziki kwa takriban miongo miwili.

Read More
 BEBE COOL ATHIBITISHA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BABY MAMA WAKE ZUENA KARIMI

BEBE COOL ATHIBITISHA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BABY MAMA WAKE ZUENA KARIMI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amekuwa akiahidi kufanya harusi na mke wake Zuena Karimi kwa muda, na namna mambo yanavyoenda ni kama tutashuhudia harusi kubwa kati ya mastaa hao mwaka huu. Kwenye moja ya onesho lake huko Mukono nchini Uganda Bebe Cool amethibitisha kuwa ndani ya mwaka huu ana mpango wa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Zuena Karimi. Bosi huyo wa Gagamel amewaambia mashabiki zake kuwa harusi ambayo anaenda kuifanya mwaka huu itavunja historia nchini Uganda. Ni hatua ambayo imepokelewa kwa ukubwa na wafuasi wake wengi kwenye mitandao ya kijamii wakisema kwamba wanangoja harusi hiyo kwa hamu harusi ya wawili hao. Utakumbuka Bebe Cool ni msanii pekee ambaye hajafanya harusi ya kanisani kando na mahasimu wake wa jadi Jose Chameleone na Bobi Wine.

Read More
 BEBE COOL AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU ISHU YA KUTOMSAPOTI ALLAN HENDRICK

BEBE COOL AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU ISHU YA KUTOMSAPOTI ALLAN HENDRICK

Staa wa muziki nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu ishu ya kutomsaidia mwanae Allan Hendrick kutunaua wigo wa muziki wake licha ya kuwa na ushawishi mkubwa Afrika Mashariki. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amekanusha madai ya kumtelekeza Allan Hendrick kwenye muziki wake huku akisema amekuwa na ukaribu na mwanae huyo kwa muda akimpa ushauri wa namna ya kuboresha muziki wake na kubaki kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu bila kuchuja. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Gyenvudde” amesisitiza kuwa anaweza kuinua muziki wa Allan Hendrick bila hata kumpa kollabo tofauti na namna watu wamekuwa wakimshinikiza kwenye mitandao ya kijamii. Kauli ya Bebe Cool imekuja siku cha baada ya Chameleone kumwagia sifa Hendrick kwa kipaji chake cha muziki ambapo alienda mbali zaidi na kuahidi kufufua muziki wake ambao umekuwa ukisuasua katika siku za hivi karibuni.

Read More
 BEB COOL MBIONI KUWAFUNGULIA MASHTAKA WANAOMPAKA TOPE NCHINI UGANDA

BEB COOL MBIONI KUWAFUNGULIA MASHTAKA WANAOMPAKA TOPE NCHINI UGANDA

Mwanamuziki Moses Ssali maarufu Bebe Cool ni mmoja wa wasanii waliokosolewa zaidi nchini Uganda, lakini huenda wanaomchafulia jina wakijipata hatiani hivi karibuni. Katika mahojiano ya hivi  karibuni na MwanaYouTube wa eneo hilo, bosi huyo wa Gagamel ameeleza kuwa ameanza kukusanya ushahidi dhidi ya wanahabari ambao wamekuwa wakimpaka tope kwa tuhuma za uongo. “Nimejenga brand yangu kwa muda mrefu sana na kwa mwandishi yeyote wa habari kuja kuniongelea upuuzi, nawaahidi nitawapa funzo. Ninakusanya ushahidi, na watalipa,” alisema. Hata hivyo Bebe Cool amesema washukiwa wakuu ni watangazaji wa redio na TV ambao wamekuwa wakitoa maoni hasi dhidi yake.

Read More