Eddy Kenzo ajibu madai ya Bebe Cool kuwa amebebwa na bahati kwenye muziki

Eddy Kenzo ajibu madai ya Bebe Cool kuwa amebebwa na bahati kwenye muziki

Nyota wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo amejibu madai ya Bebe Cool kuwa bahati ndio imembeba kwenye muziki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema Bebe Cool anatumia madai hayo kujifariji huku akidai kuwa bidii ndio imempa mafanikio makubwa kwenye muziki wake kwa miaka 10 na sio bahati kama namna ambavyo Bosi huyo wa Gagamel anavyodai. Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amesema Bebe Cool anapaswa kukubali kuwa ameacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda badala ya kuwahada mashabiki na taarifa za uongo. “Bebe Cool alisema nina bahati kwa sababu alitaka kujifariji. Huwezi kuwa na bahati milele, najua ninachofanya na nimestahili kile nilichonacho. Anapaswa kukubali na kuwaambia watu wake kwamba Kenzo amefanya muziki kwa zaidi ya miaka 10 na anafahamu hilo,” alisema Eddy Kenzo. Kauli ya Eddy Kenzo inakuja mara baada ya Bebe Cool kuachia orodha ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022 ambapo alimtaja Kenzo kama msanii aliyebebwa na bahati kwenye muziki.

Read More
 Bebe Cool Alinisaidia Kupata Mawakili katika kesi dhidi ya Luba Events – Eddy Kenzo

Bebe Cool Alinisaidia Kupata Mawakili katika kesi dhidi ya Luba Events – Eddy Kenzo

Msanii Eddy Kenzo amekiri kwamba Bebe Cool alimsaidia kuondokana na kesi iliyokuwa ikimuandama kutoka kwa Luba Events. Katika mahojiano yake hivi karibuni, Kenzo amesema Bebe Cool alimuunganisha na mawakili walioshughulikia kesi yake dhidi ya promota huyo. “Alinipigia simu na kuniuliza anawezaje kusaidia. Hakutaka kuniona nikiwa kwenye matatizo. Ni rafiki wa kweli,” alisema. Utakumbuka Luba Events alimburuza mwimbaji huyo wa ‘Tweyagale’ mahakamani Novemba mwaka 2022 baada ya tamasha la ‘Eddy Kenzo’ kufanya vizuri, akimtuhumu kuvunja mkataba wa kuandaa Tamasha hilo. Luba alieleza kuwa alipata hasara ya takriban shillingi millioni 9 ambayo aliwekeza katika tamasha hilo mwaka 2020. Kenzo alipigwa marufuku kwa muda kutumbuiza jijini Kampala kabla ya marufuku hiyo kuondolewa na mahakama. Utakumbuka Eddy Kenzo na Bebe Cool walianza kuwa marafiki baada ya Kenzo kuwa karibu na chama cha NRM, mrengo wa kisiasa ambao Bebe Cool anaunga mkono.

Read More
 Eddy Kenzo sio gwiji wa muziki – Bebe Cool

Eddy Kenzo sio gwiji wa muziki – Bebe Cool

Msanii Bebe Cool amedai kwamba Eddy Kenzo hana vigezo vya kuitwa lejendari kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Kwenye mahojiano hivi karibuni amesema hitmaker huyo wa “Nsimbudde” ana mengi ya kufanya kwenye muziki kama kweli anataka kufikia hadhi ya kuitwa nguli. Bosi huyo wa Gagamel anasema Eddy Kenzo ni msanii mwenye bahati tu na anaweza kushinda tuzo ya Grammy mwaka 2023. “Eddy Kenzo ni mwanamuziki mzuri lakini hajavuka mstari wa kuitwa nguli, hata kwa tuzo alizoshinda. Inabidi atie bidii zaidi ili kufikia viwango vya Chameleone, Bobi Wine, na mimi mwenyewe. Sio tu kwa nyimbo na tuzo,” alisema. Utakumbuka juzi kati, Bebe Cool alitoa orodha yake ya kila mwaka ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022. Bebe Cool aliwataja wanamuziki anaoamini wamepata hadhi ya kuitwa malejendari kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda. Kwenye orodha hiyo aliwataja; Jose Chameleone, Bobi Wine, Afrigo Band, na Maddox Sematimba huku akisisitiza kuwa wanaweza kukaa bila kutoa wimbo mkali kwa miaka mingi ijayo kutokana nyimbo zisizochuja walizoziachia miaka ya hapo nyuma.

Read More
 Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Bosi wa label ya Gagamel, Msanii Bebe Cool anasema alikuwa amemtabiria mema Spice Diana kipindi anatoka kimuziki miaka minane iliyopita. Bebe Cool amesema alikuwa anajua mrembo huyo atakuwa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Uganda bila usaidizi wowote wa staa mkubwa nchini humo. Aidha amefafanua sababu za kukataa kufanya kolabo na Spice Diana kwa kusema kuwa ilikuwa njia ya kumpa changamoto aendelee kuipambania brand yake hadi atakapoachia wimbo mkali kama msanii wa kujitegemea. “Miaka minane iliyopita, Spice Diana na meneja wake walikuja kwangu wakiomba kolabo. Tulikutana kwenye baa moja mjini Ntinda. Nilimwambia afanye kazi kwa bidii hadi atakapoachia wimbo mkali bila usaidizi wa mtu yeyote,” Bebe Cool alielezea. Hata hivyo anaamini ikitokea wamefanya kazi ya pamoja na Spice Diana watafaidi wote kwa kuwa mrembo huyo ameacha alama kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kutokana na nyimbo ambazo amekuwa akiaziachia katika miaka ya karibuni.

Read More
 Waandishi wa nyimbo za Bebe Cool ni bandia – King Saha

Waandishi wa nyimbo za Bebe Cool ni bandia – King Saha

Mwanamuziki King Saha ameibuka na kuwachana watu wanaomuanndikia Bebe Cool nyimbo kwa kusema kwamba hawana vipaji kwenye masuala ya uandishi. Kwenye mohajiano yake hivi karibuni King Saha amesema Bebe Cool amewekeza mamilioni ya pesa kwa waandishi wa nyimbo ilhali kazi zake zinachuja haraka. Aidha ameenda mbali Zaidi na kujinadi kuwa huwa anaandika nyimbo 5 kwa mwaka na zote zinaisha kuwa kubwa zaidi kwenye tasnia ya Afrika Mashariki. Baadhi ya waandishi wa nyimbo wanaofanya kazi kwa ukaribu na Bebe Cool ni  pamoja na Yese Oman Rafiki na Ronnie On Dis One. Utakumbuka Bebe Cool na King Saha hawajakuwa na maelewano mazuri kwa muda mrefu na ugomvi wao ulianza kipindi ambacho Bebe Cool alimshauri hitmaker huyo wa Zakayo aachane na matumizi ya mihadarati kwa kuwa itampoteza kimuziki. Tangu wakati King Saha amekuwa akimrushia vijembe Bebe Cool kila mara anapopata nafasi kwenye mahojiano yake mbali mbali.

Read More
 Mwimbaji wa Marekani Matt B adokeza kufanya kolabo na Bebe Cool

Mwimbaji wa Marekani Matt B adokeza kufanya kolabo na Bebe Cool

Msanii kutoka  Marekani Matt B amefichua mpango wa kufanya kazi  ya pamoja na wasanii wa Uganda. Kupiti ukurasa wake wa Instagram amemtaja Bebe Cool kama mmoja wa wasanii ambao huenda akafanya nao kazi ambapo alienda mbali zaidi na kuwauliza mashabiki namna wimbo wao utakavyosikika masikioni mwao. “Nilipata nafasi ya kukutana na Bebe Cool ilikuwa heshima. Nashangaa namna wimbo wa Bebe Cool na Matt B utasikika,” aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Utakumbuka Matt B ni moja kati ya wasanii walioteuliwa kushiriki tuzo za Grammy 2023 kupitia Wimbo wake na Eddy Kenzo “Gimme Love”. Wawili hao waliotajwa kuwania kipengele cha Best Global Music Performance wanatarajiwa kuchuana na wasanii Burna Boy, Rocky Dawuni na Blvk H3ro, na Bayethe Wouter Kellerman, Zakes Bantwini na Nomcebo Zikode.

Read More
 Gravity Omutujju Ajibu Madai ya Bebe Cool Kwamba Haogi

Gravity Omutujju Ajibu Madai ya Bebe Cool Kwamba Haogi

Rapa Gravity Omutujju amejibu madai ya Bebe Cool kuwa anapaswa kuoga kila mara ili aweze kufikia kiwango chake cha maisha. Hii ni baada ya Omutujju kumtaka bosi huyo wa Gagamel kustaafu muziki na kuwapa nafasi vijana wachanga waendeleze gurudumu la kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa. Sasa kupitia mitandao yake ya kijamiii rapa huyo amesema kuwa yeye huwa anazingatia sana masuala ya usafi kwa kuoga kila siku, hivyo Bebe Cool hapaswi kutumia suala hilo kuficha ukweli kwamba anatakiwa kustaafu muziki. “Tunaoga na kuvaa vizuri, kwa kweli hata tunanukia vizuri. Unaogopa uhalisia na mabadiliko. #kizazi kipya kinatawala duniani kote,” Gravity alichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.

Read More
 Bebe Cool afunguka sababu za kutofanya tamasha la muziki mwaka 2022

Bebe Cool afunguka sababu za kutofanya tamasha la muziki mwaka 2022

Msaniii mkongwe Bebe Cool amefunguka sababu za kutofanya tamasha la muziki mwaka 2022 kama wasanii wenzake. Kwenye mahojiano yake amekiri kupata changamoto ya kifedha kwa kuwa amekuwa akiwalipia karo watoto wenye uhitaji katika jamii maeneo mbali mbali nchini uganda. Hitmaker huyo wa “Gyevude” amesema watoto wengi kutoka familia zisozijiweza wanamtegemea hivyo hawezi kuwaacha wakitabiaka. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa sababu za Bebe Cool kutoandaa tamasha lake la muziki hazina mashiko kwa kuwa hajaachia wimbo wowote mkali.

Read More
 Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amemjibu Gravity Omutujju baada ya rapa huyo kumshauri astaafu muziki kwa kuwa ana umri mkubwa. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Bebe Cool amemtaka rapa huyo kumlipa pesa kama anatamani aache muziki. Utakumbuka baada ya Gravity kupata mapokezi kwenye show yake miezi kadhaa huko Cricket Oval, Lugogo aliibuka na kuwachana wasanii bebe cool jose chameleone na Bobi wine akiwashauri wageukia masuala ya kilimo na kuachia wasanii kizazi kipya kuendelea na muziki. Alienda mbali zaidi na kutoa orodha ya wanamuziki bora nchini Uganda na kuwaacha nje wasanii hao watatu.

Read More
 Wanamuziki wa Uganda wataendelea kushinda tuzo za kimataifa- Bebe Cool

Wanamuziki wa Uganda wataendelea kushinda tuzo za kimataifa- Bebe Cool

Bosi wa Gagamel, Msanii Bebe Cool ana imani kuwa wasanii wa Uganda wataendelea kung’aa kimataifa kupitia muziki wao. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Bebe Cool amebainisha kuwa kuteuliwa kwa Eddy Kenzo kwenye tuzo za Grammy 2023 itawafungulia wasanii wengi nchini humo milango ya kushiriki tuzo kubwa duniani. Ikumbukwe kipindi cha nyuma Bebe Cool alikuwa kwenye ugomvi (bifu) na Eddy Kenzo mara baada ya hitmaker huyo wa “Nsimbudde” kukimbia na msanii wake Rema Namakula ambaye alikuwa chini ya Gagamel Entertainment. Lakini wawili hao walikuja wakaweka kando tofauti zao kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini Uganda.

Read More
 Bebe Cool achoshwa na wasanii wa Nigeria kutumbuiza nchini Uganda

Bebe Cool achoshwa na wasanii wa Nigeria kutumbuiza nchini Uganda

Msanii mkongwe nchini Uganda Bebe Cool amechoshwa na hatua ya wasaniii wa Nigeria kutumbuiza nchini humo kila wiki. Bebe cool amesema kitendo hicho imewafanya wasaniii wa Nigeria kujiona kuwa wana mashabiki wengi kuwashinda wasanii wa ndani huku akiwataka mashabiki kuwaonyesha upendo wasanii wa Uganda pindi wanapofanya matamasha kama njia ya kuwapa changamoto mapromota muziki kuwazingatia kwenye maonyesha yao. “We are tired of Nigerian artists coming here and acting as though they have more fans here. I implore everyone who has supported Kenzo to also come for Jose Chameleone’s concert dubbed “Gwanga Mujje” next year at Cricket Oval,” Alisema Bebe Cool. Bosi huyo wa Gagamel ametoa kauli hiyo alipokuwa anawarai mashabiki kumuunga mkono msanii jose chameolene kipindi hiki yupo kwenye maandalizi ya onesho lake ambalo litafanyika mapema mwaka 2023. Ikumbukwe ndani ya mwaka huu wasanii kumi kutoka Nigeria tayari wametumbuiza nchini Uganda akiwemo Tiwa Savage, Rema, Ruger, na wengine wengi.

Read More
 Bebe Cool ampa Eddy Kenzo maua yake akiwa angali hai kuelekea Tamasha lake Novemba 12

Bebe Cool ampa Eddy Kenzo maua yake akiwa angali hai kuelekea Tamasha lake Novemba 12

Msanii mkongwe kwenye muziki Bebe Cool ameamua kumpa maua yake Eddy Kenzo akiwa angali hai licha ya watu kuhisi kuwa ana bifu (ugomvi) na Bosi huyo wa Big Talent. Mkali huyo ngoma ya “Boss Lady” ametoa wito kwa mashabiki wa muziki mzuri kujitokeza na kuhudhuria tamasha la msanii huyo Novemba 12 huko Kololo Airstrip huku akithibitisha kuwa atakuwa moja kati ya wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo. Ikumbukwe miaka kadhaa iliyopita Eddy Kenzo alimualika Bebe Cool kwenye tamasha lake la muziki katika hoteli ya Serena viungani mwa Jiji la Kampala na kupitia tamasha hilo ndipo alimaliza bifu yake na Bobi Wine.

Read More