BIEN WA SAUTI SOL AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

BIEN WA SAUTI SOL AKANUSHA KUWA KWENYE UGOMVI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

Msanii wa Sauti Sol, Bien amefunguka na kudai kuwa hana ugomvi wowote na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja kama namna baadhi ya watu wanavyochukulia mtandaoni. Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Bien amesema kile ambacho anakishinikiza kama kundi la Sauti Sol  malipo yao wimbo wa Extravangaza ambao ulitumiwa na muungano huo kwenye shughuli zao kisiasa bila ridhaa yao. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mbwe Mbwe” amesema mawakili wapo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Azimio la Umoja kutatua utata unaozingira wimbo wao  wa extra vangaza huku akidokeza kwamba huenda wakalipa shillingi billioni moja za kenya kwa kuharibiwa brand yao ya muziki. Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Ezekiel Mutua kuitaka bendi ya Sauti Sol kuacha kushiriki vita vya mtandaoni na muungano wa Azimio la Umoja na badala yake watumie njia ya mazungumzo kutatua tofauti zao kudai haki yao kwani jambo hilo huenda likaathiri muziki wao. Utakumbuka baada ya Sauti Sol kutishia kuufungulia muungano wa Azimio la Umoja kesi kwa kuitumia wimbo wa Extravaganza kwenye kampeini zao bila ridhaa yao, walipoteza takriban subscribers 2,000 kwenye mtandao wa Youtube na kuifanya channel yao kushuka kutoka subscribers elfu 905 hadi 904.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AUCHANA MUUNGANO WA KISIASA NCHINI KENYA AZIMIO LA UMOJA

BIEN WA SAUTI SOL AUCHANA MUUNGANO WA KISIASA NCHINI KENYA AZIMIO LA UMOJA

Mwanakikundi wa Sauti Sol, Bien ameamua kurusha jiwe gizani kwenda kwa uongozi wa Azimio la Umoja unaongozwa na Raila Odinga baada ya bendi hiyo kupoteza jumla ya subscribers 2.000 kwenye mtandao wa youtube ndani ya kipindi cha masaa 48. Kupitia Mtandao wa Instagram Bien, ameandika ujumbe wa kimafumbo ambao umetafsiriwa na wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuwa bendi hiyo inaegemea upande wa mrengo wa Kenya Kwanza unaongozwa na Naibu wa Rais Dakta William Ruto wakati huu taifa inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9. “Time will reveal. Wale wanashuka washuke saa hii. Stage yao imefika.” Ameandika Instagram. Chapisho hilo kutoka kwa Bien imeibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya kwenye mitandao ya kijamii, ambapo wengi wamewataka wasaani hao bendi hiyo kujitenga na masuala ya siasa na badala yake wawekeze nguvu zao kwenye suala la kutoa muziki mzuri. Channel ya Youtube ya Sauti Sol ambayo ilikuwa na subscribers elfu 903 kwa sasa ina jumla ya subscribers elfu 903. Jumatatu wiki hii bendi ya Sauti Sol ilitishia kuushtaki Muungano wa Azimio la Umoja kwa kutumia wimbo wao “Extravaganza” bila ridhaa yao kwenye kampeni zao ambapo siku hiyo walikuwa wakimtambulisha Mgombea mwenza wa Raila Odinga, Bi. Martha Karua. Utakumbuka mwaka wa 2021 Sauti Sol walikuwa baadhi ya wasanii Kenya waliojitokeza hadharani na kupinga mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia Mpango wa Maridhiano BBI ambao ulikuwa unaongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AKIRI KUWAHI KUTAKA KUIVUNJA NDOA YAKE NA MKEWE CHIKI KISA MSONGO WA MAWAZO

BIEN WA SAUTI SOL AKIRI KUWAHI KUTAKA KUIVUNJA NDOA YAKE NA MKEWE CHIKI KISA MSONGO WA MAWAZO

Mwanakikundi wa bendi ya Sauti Sol, Bien Barasa ameendelea kutoa ushuhuda wa ndani kuhusu maisha yake, amefunguka kwamba aliwahi kutaka kuivunja ndoa yake. Kwenye podcast ya Bald Box msanii huyo amesema kwamba mwaka wake wa kwanza kwenye ndoa nusra ampe talaka mke wake Chiki kuruka baada ya kupitia wakati mgumu kipindi cha korona. Hitmaker huyo wa ngoma ya “MbweMbwe” amesema alipatwa na msongo wa mawazo kipindi cha korona baada ya shughuli za kimuziki za bendi ya Sauti Sol kusambaratika lakini alikuja akapata afueni alipopata ushauri nasaha kutoka kwa mwanasaikolojia. Utakumbuka Bien Aime Barasa na mkewe Chiki Kuruka ambaye ni dancer, mwalimu wa mazoezi ya mwili na mtangazaji wa redio walifunga ndoa miaka miwili iliyopita.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL MBIONI KUKAMILISHA COLLABO YAKE NA KUNDI LA ETHICS

BIEN WA SAUTI SOL MBIONI KUKAMILISHA COLLABO YAKE NA KUNDI LA ETHICS

Member wa Sauti Sol Bien na wasanii wa kundi la muziki wa gengetone Ethics Entertainment wameingia studio kwa ajili ya kuandaa kazi yao ya pamoja. Kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii wasanii hao wameonekana kuwa katika jukumu la kushirikiana kuandaa wimbo katika mazingira ya Studio wakivibe na mdundo wa kazi yao mpya. Video hiyo imewaacha mashabiki na maswali mengi kama kweli wawili hao wapo kwenye maandalizi ya kazi yao mpya au walikuwa kwenye starehe zao. Hata hivyo iwapo Bien na wasanii wa Ethics Entertainment wataachia collabo yao itakuwa ni kazi yao ya kwanza ikizingatiwa kuwa hawajawahi kufanya kazi ya pamoja.

Read More
 BIEN BARAZA WA SAUTI SOL ATANGAZA KUACHA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

BIEN BARAZA WA SAUTI SOL ATANGAZA KUACHA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

Mwanamuziki mahiri wa kundi maarufu la muziki kutoka nchini Kenya ‘Sauti Sol’ Bien-Aime Baraza ametangaza kubadilisha mfumo wa matumizi yake ya mitandao ya kijamii, kutokana na kile alichodai kuwa mitandao hiyo ni sawa na sehemu ya sumu. Bien ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kubainisha dhamira yake ya kuacha mitandao baada ya kutafakari maisha yake kwa muda mrefu. “Baada ya kujitazama kwa muda mrefu kwenye kioo, nimeamua kubadili njia zangu. Mtandao ni mahali pa sumu sana na ninataka tu kuchukua hatua, Kuna tabia nyingi ambazo nilizichukua na mwaka huu naziacha, Nataka tu kupumzika na kurudi nyuma,” alisema. Hitmaker huyo wa “Mbwe Mbwe” amesema kuwa anajua mchakato wa mabadiliko hautakuwa rahisi, lakini amejipanga kwa safari ndefu inayokuja na kukiri kufikia hatua ya kuacha hata matumizi ya vileo. Kufuatia uamuzi wa nyota huyo, aliungwa mkono na watu mbali mbali licha ya kuwepo kwa waliompinga kiasi cha kubashiri kuwa hatoweza kutekeleza mpango hu .

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA  KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

BIEN WA SAUTI SOL ATOA OFA KWA YEYOTE ATAKAYEMREJESHEA SIMU YAKE ILIYOIBIWA

Member wa Sauti Sol, Bien ameahidi kutoa ofa ya shillingi elfu 50 kama zawadi kwa yeyote atakayemrudishia simu yake ambayo juzi kati iliibiwa katika ukumbi wa burudani wa Carnivore kwenye onesho la NRG Wave Concert. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bien ameandika ujumbe wa masikitiko kwa kusema kwamba aliibiwa simu aina ya Infinix Note 11 Pro na vifunguo vya gari aina ya Porsche Cayenne ambapo amedai kuwa simu yake ilikuwa na data muhimu ya album mpya ya Sauti Sol ambayo inatarajiwa kuingia sokkoni mwezi Aprili mwaka huu. Hitmaker huyo wa “Mbwe Mbwe” ameenda mbali zaidi na  kutania kuwa hangekaa vibaya watu wangemuibia hata mke wake Chiki Kuruka huku akisisitiza kutoa zawadi ya shillingi elfu 50 kwa yeyote atakayemrudhishia simu pamoja na vifunguo vya gari. Sanjari na hilo msanii Ndovu Kuu amethibitisha kuibiwa simu kwenye onesho la NRG Wave Concert lilofanyika katika ukumbi wa Carnivore ambapo pia ameahidi kutoa zawadi kwa yeyote atakayemregeshea simu yake.

Read More
 ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

Mchekeshaji Eric Omondi ameingia kwenye headlines baada ya kutaka kuzichapa na member wa Sauti Sol, Bien baraza usiku wa kuamkia Januari mosi katika onesho la Konshens Jijini Nairobi. Chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Omondi kushinikiza kundi la Sauti Sol watumbuize wa mwisho katika orodha ya wasanii kama njia ya kuwapa heshima. Làkini Pia Bien katika moja ya interview amenukuliwa akisema muda wanaopewa kuperfom kama kundi la Sauti Sol katika tamasha haijawahi kuwa tatizo kwao, iwapo atakuwa wasanii wa kwanza au wa mwisho katika orodha ya wasanii. Ikumbukwe kwa muda  sasa eric omondi amekuwa akipaza sauti juu ya wasanii wa kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki. Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.

Read More