Burna Boy Alazika Kufuta Shows zake Baada ya Kuugua Ghafla
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Burna Boy, amelazika kufuta shows zake baada ya kuchoka kupita kiasi. Msanii huyo wa muziki wa Afro-fusion ameshare video kupitia Instastory yake ikimuonesha akipatiwa matibabu baada ya kupiga show tatu mfululizo ndani ya masaa 24 bila kupata muda wa kupumzika. Hali hiyo imesababisha kufutwa kwa show yake iliyokuwa imepangwa kufanyika usiku wa leo katika Kia Center, Orlando, ukumbi wenye uwezo wa kubeba takribani watu 20,000. Burna Boy yuko katika mfululizo wa ziara yake ya kimataifa iitwayo “No Sign of Weakness Tour”, ambayo ilianza Novemba 2025 na inatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Mashabiki wake wameonyesha wasiwasi na kumtakia nafuu ya haraka, wakisisitiza umuhimu wa wasanii kupumzika ili kuendelea kutoa burudani bila kuathiri afya zao.
Read More