Buruklyn Boyz Yatunukiwa Gold Kupitia Album ya East Mpaka London

Buruklyn Boyz Yatunukiwa Gold Kupitia Album ya East Mpaka London

Kundi la muziki la Buruklyn Boyz limeandika historia mpya baada ya albamu yao East Mpaka London kutunukiwa hadhi ya Gold Certification kufuatia kuvuka zaidi ya streams milioni 30 kwenye majukwaa mbalimbali ya kidijitali. Kupitia ujumbe waliouchapisha mtandaoni, Buruklyn Boyz wamewashukuru mashabiki wao kwa mchango mkubwa walioonyesha tangu mwanzo wa safari yao ya muziki. Albamu ya East Mpaka London iliachia rasm Mei 20 mwaka wa 2022 na ilikuwa albamu yao ya kwanza (debut album). Mradi huo ulijumuisha nyimbo 15, zikiwemo Pree, Dream Ya Kutoka Kwa Block, Catalyst, Usikam Hii Section, Blicky, Niskize na Coins. Albamu hiyo pia iliwashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Maya Amolo, Silverstone Barz, Big Yasa na Younglouie58, jambo lililoongeza utofauti wa sauti na ubunifu ndani ya mradi huo. Mafanikio ya kupata Gold Certification yanaendelea kuthibitisha nafasi ya Buruklyn Boyz kama moja ya makundi yaliyochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa muziki wa drill nchini Kenya na Afrika Mashariki.

Read More
 Buruklyn Wakanusha Kufanya Kazi na Toxic Lyrikali

Buruklyn Wakanusha Kufanya Kazi na Toxic Lyrikali

Mabingwa wa miondoko ya Drill kutoka Nairobi, Buruklyn Boyz, wameingilia kati na kuzima tetesi zilizoanza kusambaa kwa kasi mtandaoni zikidai kuwa kundi hilo linapika mradi mpya wa muziki na hasimu wao rapa Toxic Lyrikali. Kupitia kurasa zao rasmi, Buruklyn Boyz wamekanusha vikali taarifa hizo na kudai kuwa hawana akaunti yoyote rasmi ya Facebook. Wamesema kuwa yeyote anayotumia jina lao kwenye jukwaa hilo ni tapeli anayepotosha mashabiki wao kwa taarifa za uongo. Hata hivyo wasanii hao wametoa onyo kwa wafuasi wao kutokubali kudanganywa na akaunti feki (parody accounts) na kuwataka kufuatilia taarifa rasmi kupitia vyanzo vyao vilivyothibitishwa pekee. Kauli hiyo imekuja kama pigo kwa mashabiki waliokuwa na shauku ya kuona kama bifu kati ya wasanii wa Buruklyn Boyz na rapa Toxic Lyrikali lingeweza kumalizwa kwa kazi ya pamoja.

Read More
 BURUKLYN BOYZ WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA “EAST MPAKA LONDON”

BURUKLYN BOYZ WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA “EAST MPAKA LONDON”

Kundi la muziki nchini Kenya, Buruklyn Boyz  limeachia rasmi Album yao mpya inayokwenda kwa jina la East Mpaka London.. Album hiyo ambayo ina jumla ya mikwaju 16 ya moto  ina kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Young Louie, Maya Amolo na Silverstone Barz. East Mpaka London Album  ina nyimbo kama Pree, Blicky, Coins,Ex, Delete, Taliban na  inapatikana exclusive kupitia digital platforms mbalimbali za kupakua na kusikilizia muziki duniani ikiwemo,Youtube, Apple Music na Spotify. Album hii ni ya kwanza kwa wasanii wa Buruklyn Boyz tangu waanze safari yao ya muziki miaka mitatu iliyopita. Buruklyn Boyz ni kundi la muziki wa Drilll ambalo linaundwa na wasanii Mr. Right pamoja na Ajay na lilipata umaarufu nchini mwaka wa 2019 lilipoachia singo yao ya kwanza iitwayo “Durag na Slice.”

Read More