Mfanyabiashara na staa wa mitandao ya kijamii, Zari Hassan, ametangaza rasmi kuachana na mume wake baada ya kuwa pamoja kwa takriban miaka mitano.
Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Zari amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kutengana kutokana na tofauti ambazo hawawezi kuzitatua, maarufu kama irreconcilable differences.
Zari amesema kuwa licha ya kuachana, hakuna chuki wala kinyongo kati yao. Amesisitiza kuwa wanathamini muda walioutumia pamoja, kumbukumbu walizozitengeneza na sapoti waliyopeana katika kipindi chote cha mahusiano yao.
Aidha, wawili hao wameeleza kuwa wataendelea kuwa marafiki wenye kuheshimiana na kuelewana, huku kila mmoja akimtakia mwenzake mafanikio, furaha na kila la heri katika maisha yajayo.
Kwa sasa, wala Zari wala Shakib hawajatoa maelezo zaidi kuhusu chanzo halisi cha tofauti zilizopelekea kuvunjika kwa mahusiano yao.