Sports news

KOMBE LA DUNIA: Mexico na South Korea Zashinda Mechi ya Ufunguzi

KOMBE LA DUNIA: Mexico na South Korea Zashinda Mechi ya Ufunguzi

Michuano ya Kombe la Dunia ya FIFA 2026 imeanza rasmi jana kwa kishindo, huku wenyeji Mexico pamoja na miamba ya Asia, South Korea, wakiondoka na alama tatu muhimu katika mechi za kwanza za Kundi A zilizopigwa nchini Mexico.

Wenyeji Mexico walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) mbele ya umati mkubwa wa mashabiki.Mshambuliaji Julián Quiñones alifunga bao safi la ufunguzi mapema dakika ya 9 tu ya mchezo. Mkongwe Raúl Jiménez alipachika goli pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 67

Licha ya Afrika Kusini kupambana, matumaini yao yalizorota baada ya wachezaji wao wawili, Sphephelo Sithole na Themba Zwane, kuoneshwa kadi nyekundu. Beki wa Mexico, César Montes, naye alipewa kadi nyekundu mwishoni mwa mechi na kufanya jumla ya kadi nyekundu kuwa tatu.

Katika mchezo mwingine wa Kundi A uliopigwa kwenye Uwanja wa Guadalajara, South Korea ilionyesha ujasiri mkubwa baada ya kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Czech Republic.Czech Republic walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi mnamo dakika ya 58 kupitia kwa Ladislav Krejčí. South Korea wakasawazisha kupitia kwa Hwang In-beom dakika ya 67, kabla ya Oh Hyeon-gyu kupachika bao la ushindi dakika ya 80 na kuwapa South Korea alama tatu muhimu.

Kufuatia matokeo hayo, Mexico wanaongoza Kundi A wakiwa na alama 3 na mtaji wa mabao mawili, wakifuatiwa na South Korea wenye alama 3 na bao moja. Czech Republic inashika nafasi ya tatu huku Afrika Kusini wakiburuza mkia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *