Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Eddy Kenzo sio mwanamuziki bora Uganda – Ragga Dee

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Ragga Dee amemkataa Bosi wa Big Talent, Eddy Kenzo. Hii  ni  baada ya watu kuhoji kuwa Eddy Kenzo ndiye mwanamuziki bora nchini humo kufuatia kuteuliwa kwake kwenye tuzo za Grammy mwaka 2023. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ragga Dee amesema kuna wasanii wengi nchini Uganda ambao wana vipaji kumzidi Kenzo, hivyo kwa upande wake haamini kama hitmaker huyo “Nsimbudde” hapaswi kupewa taji la mwanamuziki bora nchini humo. “Eddy Kenzo ni msanii mzuri sana, hata hivyo, sio mwanamuziki bora nchini Uganda. Kuna wasanii wengine wazuri wa Karamoja na mikoa mbalimbali ambao hatuwajui,” alisema. Ikumbukwe kipindi cha nyuma Kenzo alisema kwamba hajali maneno ya watu wanaodai kuwa yeye ni msanii bora nchini uganda, ila jambo analozingatia kwenye muziki wake ni kufanya kazi zenye ubora. Wasanii kadhaa ikiwemo Gravity Omutujju na Roden Y Kabako wanamtaja Eddy Kenzo kama mwanamuziki bora nchini Uganda.

Read More
 Wanamuziki wa Uganda wataendelea kushinda tuzo za kimataifa- Bebe Cool

Wanamuziki wa Uganda wataendelea kushinda tuzo za kimataifa- Bebe Cool

Bosi wa Gagamel, Msanii Bebe Cool ana imani kuwa wasanii wa Uganda wataendelea kung’aa kimataifa kupitia muziki wao. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Bebe Cool amebainisha kuwa kuteuliwa kwa Eddy Kenzo kwenye tuzo za Grammy 2023 itawafungulia wasanii wengi nchini humo milango ya kushiriki tuzo kubwa duniani. Ikumbukwe kipindi cha nyuma Bebe Cool alikuwa kwenye ugomvi (bifu) na Eddy Kenzo mara baada ya hitmaker huyo wa “Nsimbudde” kukimbia na msanii wake Rema Namakula ambaye alikuwa chini ya Gagamel Entertainment. Lakini wawili hao walikuja wakaweka kando tofauti zao kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini Uganda.

Read More
 Usalama wa Eddy Kenzo waimarishwa- Asema Promota Balaam Barugahara

Usalama wa Eddy Kenzo waimarishwa- Asema Promota Balaam Barugahara

Promota Balaam Barugahara amethibitisha kuwa usalama wa mwanamuziki Eddy Kenzo umeimarishwa baada ya kutishiwa maisha na watu wasiojulikana. Kwenye mahojiano yake, promota huyo amesema njama ya wanaopanga kumtoa uhai Kenzo haitafaulu kamwe ikizingatiwa kuwa msanii huyo tayari ana walinzi wengi waliojihami na silaha kali za moto. Baalam ameongeza kuwa njama hiyo inaweza tu kufanikiwa iwapo watesi wake watatumia njia ya uchawi. “Wale wanaotaka kumuua Kenzo wanaweza tu kufanikiwa kupitia uchawi. Ameimarisha usalama wake na walinzi wenye uzoefu,” Balaam alisema kwenye mahojiano na YouTuber mmoja nchini Uganda. Mapema wiki hii, Kenzo alifichua kuwa anapokea jumbe za kumtishia maisha ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka Waganda kumuombea.

Read More
 Eddy Kenzo amkingia kifua Museveni baada ya wafuasi wa NUP kumtishia maisha

Eddy Kenzo amkingia kifua Museveni baada ya wafuasi wa NUP kumtishia maisha

Msanii Eddy Kenzo amehapa kwamba hatokuja kumvunjia heshima Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa lengo la kuwafurahisha wapinzani wake. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kenzo ambaye juzi kati aliteuliwa kuwania tuzo ya Grammy 2023 kupitia kipengele cha Best Global Perfomance, amekiri kuwa  Museveni ni mwokozi wake kwani alikuwa mtu wa msaada kwake kipindi cha korona alipofungiwa nchini Ivory Coast. “I will never abuse Museveni to make his opponents happy. That is what they want but his my saviour. He saved me during the pandemic,” alisema. Kauli yake imekuja mara baada ya wafuasi wa chama cha NUP inayoongozwa na Bobi Wine kumkashifu kwa hatua ya kujihusisha na viongozi wakuu serikalini kwenye tamasha lake lilomalizika wikiendi iliyopita huko Kololo Airstrip. Utakumbuka mapema wiki hii Eddy Kenzo alidai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya watu wasiojulikana kuanza kumtolea vitisho vya kumuangamizi.

Read More
 Eddy Kenzo ashtakiwa na Promota kwa kukiuka mkataba wa kufanya tamasha la muziki

Eddy Kenzo ashtakiwa na Promota kwa kukiuka mkataba wa kufanya tamasha la muziki

Mwanamuziki Eddy Kenzo ameburuzwa mahakamani kwa kufanya tamasha la muziki wikiendi iliyopita bila kumhusisha promota muziki nchini humo Luba Events. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Luba amewasilisha kesi mahakamani kumzuia msanii huyo haziweze kufanya matamasha ya muziki nchi Uganda hadi pale uamuzi wa kesi yake itakapotolewa. Promota huyo amedai kuwa alisaini mkataba wa kufanya onesho la muziki na Eddy Kenzo mwaka 2020 ambapo alienda mbali zaidi na kumlipa Ksh 3.9 millioni lakini wakati janga la Corona lilizuka walilazimika kuahirisha onesho lao. Luba amesema licha ya kumuandika Eddy Kenzo barua ya kumuonya asifanye tamasha hilo la muziki bila kumshirikisha, msanii huyo alikwenda kinyume na agizo lake na kufanya tamsha hilo mwenyewe. Hata hivyo amedai kuwa jaribio la kutatua sakata lake na Eddy Kenzo halikuzaa matunda, jambo ambalo lilimlazimu kumfungulia kesi mahakamani. Ikumbukwe Luba Events alikuwa miongoni mwa mapromota wa muziki waliofidiwa na serikali ya Uganda kwa hasara waliyopata wakati wa janga la Corona baada ya matamasha ya muziki kusitishwa ghafla.

Read More
 Eddy Kenzo aandika historia Afrika Mashariki, Atajwa kuwania tuzo za Grammy.

Eddy Kenzo aandika historia Afrika Mashariki, Atajwa kuwania tuzo za Grammy.

Mwanamuziki wa nchini Uganda Eddy Kenzo ametajwa kuwania Tuzo za Grammy mwaka 2023 ambapo ametajwa katika kipengele cha Best Global Music Performance na wimbo wake ‘Gimme Love’ aliomshirikisha Matt B. Eddy Kenzo anakuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania Tuzo hizo kubwa na maarufu duniani. Aliwahi pia kuwa msanii pekee aliyeshinda Tuzo ya BET kwa Afrika Mashariki kabla ya Rayvanny kuinyakua pia mwaka 2017. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Februari 05, mwaka 2023.

Read More
 Bebe Cool ampa Eddy Kenzo maua yake akiwa angali hai kuelekea Tamasha lake Novemba 12

Bebe Cool ampa Eddy Kenzo maua yake akiwa angali hai kuelekea Tamasha lake Novemba 12

Msanii mkongwe kwenye muziki Bebe Cool ameamua kumpa maua yake Eddy Kenzo akiwa angali hai licha ya watu kuhisi kuwa ana bifu (ugomvi) na Bosi huyo wa Big Talent. Mkali huyo ngoma ya “Boss Lady” ametoa wito kwa mashabiki wa muziki mzuri kujitokeza na kuhudhuria tamasha la msanii huyo Novemba 12 huko Kololo Airstrip huku akithibitisha kuwa atakuwa moja kati ya wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo. Ikumbukwe miaka kadhaa iliyopita Eddy Kenzo alimualika Bebe Cool kwenye tamasha lake la muziki katika hoteli ya Serena viungani mwa Jiji la Kampala na kupitia tamasha hilo ndipo alimaliza bifu yake na Bobi Wine.

Read More
 Eddy Kenzo akanusha kuwa muumini wa dhehebu la Illuminati

Eddy Kenzo akanusha kuwa muumini wa dhehebu la Illuminati

Msanii nyota kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo amenyosha maelezo kuhusu madai ya kutumia ishara ya illuminati kwenye video ya wimbo wake “Semyekozo”.. Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema alama alizozitumia kwenye video ya wimbo huo haihusiani kabisa na nguvu za kishetani kama baadhi ya walimwemgu walivyohoji mtandaoni kwani ni ishara ya kawaida ambayo watu hutumia kwenye maisha ya kila siku mitaani. Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amewataka watu waache kuwa na fikra za kishamba kwa kuwahusisha watu wenye mafanikio na nguvu za giza huku akisema kuwa chimbuko la illuminati limetokana na makundi ya watu matajiri duniani na sio madhehebu ya kishetani kama wengi wanavyodhani. Utakumbuka miaka kadhaa iliyopita baada ya Eddy Kenzo kutusua kimataifa, walimwengu walihoji kuwa huenda utajiri na mafanikio yake kisanaa imetokana na hatua yake kuingia ubia wa kufanya kazi na dhehebu la illuminati.

Read More
 Eddy Kenzo amtabiria mema Gravity Omutujju licha ya watu kumshambulia mtandaoni

Eddy Kenzo amtabiria mema Gravity Omutujju licha ya watu kumshambulia mtandaoni

Mwanamuziki Eddy Kenzo amemtabiria mema rapa Gravitty Omutujju kwa kusema kuwa atapata mafanikio makubwa kwenye muziki wake licha ya watu kumpiga vita kila mara kwenye shughuli zake. Kwemye mahojiano yakw hivi karibuni Kenzo amesema omutujju hatoshushwa kisanaa na baadhi ya watu wanaojaribu kumshambulia mtandaoni kwani ni moja kati ya watu ambao wamepitia maisha ya taabu.. “Nilimtoa Gravity kutoka mitaa ya banda. Alikuwa analala chumba kimoja na mama yake mzazi pamoja na dada yake. Ana ujasiri kwa kile anachokifanya najua atafika mbali, hivyo hakuna mtu ambaye atamshusha kisanaa mapema, ana moyo mugumu wa kupigana na matatizo”, Alisema. Eddy Kenzo ambaye alimtoa kimuziki Rapa Gravityy Omutujju chini ya lebo yake ya muziki ya Big Talent, anatarajiwa kufanya tamasha lake la muziki Novemba 9 mwaka huu huko Kololo Airstrip nchini Uganda.

Read More
 Eddy Kenzo akumbwa na msala mwingine baada ya kifo cha kaka yake, Mande

Eddy Kenzo akumbwa na msala mwingine baada ya kifo cha kaka yake, Mande

Msanii Eddy Kenzo amepata pigo nyingine baada ya dada yake kumpoteza binti yake mwenye umri wa miaka siku chache baada ya kumzika kaka yao. Duru zikuaminika zinasema binti huyo alifariki kifo cha kawaida akiwa shuleni akijitayarisha kukalia mtihani wake wa PLE. Shinah alipatikana amefariki kwa beni ya shule amezikwa huko Kanyuga, Kassawo, Kifumpa nchini Uganda. Chanzo cha kifo chake hakijajulikana ila maafisa wa usalama wanaendelea na uchunguzi kubaini ni nini hasa kilikumkutana msichana huyo. Utakumbuka mwisho mwa wiki kaka ya Eddy Kenzo alifariki baada ya kupata majeraha mabaya kichwani alipopigwa na jamaa mmoja kwenye moja ya night club huko nchini Uganda.

Read More
 Eddy Kenzo awaonya Waislamu kutofuta Tattoo kwenye mwili wake pindi atakapofariki

Eddy Kenzo awaonya Waislamu kutofuta Tattoo kwenye mwili wake pindi atakapofariki

Hitmaker wa “Nsimbudde”, Msanii Eddy kenzo ni kama ameanza kujipanga na safari yake ya mwisho/ kifo chake baada ya kutoa maagizo ya kutaka kuzikwa na Tatoo. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema licha ya kwamba alikenda kinyume na imani ya kiislamu kwa kuchora tatoo, watu watakaompuzisha kwenye nyumba yake ya milele wasijaribu kufuta tatoo yeyote kwenye mwili wake pindi atakapofariki duniani. “Muslims should not cut off or remove my tattoos after my death, I will be very mad at them. That is my choice and I will have to deal with my creator when I am gone,” Alisema Eddy Kenzo. Eddy kenzo ni moja kati ya wasanii walio na tatu nyingi kwenye mwili mwake nchini Uganda licha ya imani ya kiislamu kukatazaa waumini wake kuchora miili yao kwani inakwenda kinyume na uumbaji wa mwenyezi Mungu.

Read More
 Eddy Kenzo afunguka sababu za wasanii wa Uganda kutoachia nyimbo za kizalendo

Eddy Kenzo afunguka sababu za wasanii wa Uganda kutoachia nyimbo za kizalendo

Hitmaker wa “Nsimbudde”, Msanii Eddy Kenzo ametoa changamoto kwa serikali ya Uganda kuwawezesha wasanii wa ndani kifedha ili waweze kurekodi nyimbo za kizalendo. Kwenye mahojiano na Tawfiq Media Ug Kenzo amesema wasanii wengi wanaogopa kuachia nyimbo za kizalendo kwa sababu aina hiyo ya muziki haina soko. Mshindi huyo wa BET amesisitiza kuwa wasanii wengi wanafanya muziki kama biashara na ndio maana wengi wao wanawekeza kwenye muziki ambao unawaingizia kipato. Kauli ya Eddy Kenzo imekuja mara baada ya kuulizwa mbona wasanii wengi nchini Uganda hawatoi nyimbo za kizalendo katika miaka ya hivi karibuni.

Read More