EDDY KENZO AWAPA SOMO VIJANA KUHUSU NDOA ZA MAPEMA

EDDY KENZO AWAPA SOMO VIJANA KUHUSU NDOA ZA MAPEMA

Bosi wa Big Talent, Msanii Eddy Kenzo amewashauri vijana kujiepusha na ndoa za mapema. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amedai kuwa vijana wanapaswa kueleza nguvu zao kwenye masuala ya kujiboresha kiuchumi kabla ya kuingia kwenye ndoa. “Nawashauri vijana kuchukua muda wao kabla ya kufunga ndoa. Nimekuwepo na nazungumza kutokana na uzoefu,” alisema. Awali Eddy Kenzo alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii Rema Namakula ambaye wamejaliwa kumpata mtoto mmoja lakini wawili hao walikuja wakatengana mwaka 2019 na tangu wakati huo mshindi huyo wa BET hajawahi kuingia kwenye mahusiano mengine.

Read More
 EDDY KENZO AWATAKA WASANII WA UGANDA KUFANYA MUZIKI WAO WA ASILI KANDONGO KAMU

EDDY KENZO AWATAKA WASANII WA UGANDA KUFANYA MUZIKI WAO WA ASILI KANDONGO KAMU

Msanii Eddy Kenzo ametoa changamoto kwa wanamuziki nchini kwao Uganda kuendelea kufanya muziki wao wa asili uitwao Kandogo Kamu. Hitmaker huyo wa “Nsimbudde” amewataka wasanii kufuata nyayo za wakongwe waliokuwa wanafanya mtindo huo wa muziki bila kukataa tamaa, kipindi muziki wa Congo ulikuwa umekita mizizi nchini Uganda miaka ya hapo nyuma. Bosi huyo wa Big Talent amesema wasanii wa Uganda wakiaanza kurekodi nyimbo zenye mahadhi ya Kandongo Kamu wanaweza uwezo mkubwa wa kushindana na wanamuziki wengine duniani Eddy Kenzo kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya tamasha lake la muziki ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 12 mwaka 2022.

Read More
 EDDY KENZO AKATAA KUZUNGUMZIA MPANGO WA KUTOA MATUNZO KWA BINTI YAKE NA REMA NAMAKULA

EDDY KENZO AKATAA KUZUNGUMZIA MPANGO WA KUTOA MATUNZO KWA BINTI YAKE NA REMA NAMAKULA

Bosi wa Big Talent, Msanii Eddy Kenzo hayuko tayari kujibu maswali yoyote kuhusiana na mpango wake wa kutoa matunzo kwa binti yake aliyezaa na msanii Rema Namakula. Akizungumza na Spark TV, Eddy Kenzo ameeleza kuwa haimkalii vizuri kuzungumzia masuala yake ya faragha hadharani huku akisema kwamba anamheshimu sana binti yake, hivyo hapendi watu wakimjadili mtandaoni. Eddy Kenzo ametoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa upande wake wa stori kufuatia hatua ya baby mama wake Rema Namakula kusema kwamba wanashirikiana vyema na mkali huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” kwenye suala la kutoa mahitaji ya msingi kwa binti yao. Utakumbuka Rema Namakula aliachana na Eddy Kenzo mwaka wa 2019 ambapo aliingia kwenye mahusiano mengine na Dakta Hamsa Ssebunya.

Read More
 EDDY KENZO AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

EDDY KENZO AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

Msanii Eddy Kenzo amewahimiza wasanii wenzake nchini Uganda kutowaingilia wasanii wa Nigeria ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye soko la muziki duniani. Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema muziki wa nigeria umepata mapokezi mazuri kwa sababu ni wakati wao kung’ara huku akiwataka wasanii wa uganda kutia bidii kwenye kazi zao kwani kuna kipindi muziki wao pia utafanya vizuri duniani akitolea mfano muziki wa Congo na Jamaica ambao umepotea kwa sasa licha ya kupata mapokezi makubwa miaka ya hapo nyuma. “They are trending in the whole world because that’s how their music is performing. It’s just their season, and we shall also get ours. Even Congolese and Jamaicans dominated our airways years back but they are no more,” Alisema. Hitmker huyo wa “Follow” amesema wasanii wa nigeria wamewekeza pesa nyingi kwenye muziki wao kiasi cha kuwa na mawakala nchini uganda ambao wanawalipa madeejay kucheza nyimbo zao. “Nigerians invest so much money in their music and promotion. They have agents here and they pay deejays to play their music,” Aliongeza. Hata hivyo amesema wasanii hao wanapaswa kulipwa pesa nyingi kwenye shows zao kwa sabababu wametumia pesa nyingi kutengeneza brand zao za muziki tofauti na wasanii wa Uganda.

Read More
 EDDY KENZO AWALAUMU WASANII WAKONGWE KWA KUIGAWANYA TASNIA YA MUZIKI UGANDA

EDDY KENZO AWALAUMU WASANII WAKONGWE KWA KUIGAWANYA TASNIA YA MUZIKI UGANDA

Mwanamuziki Eddy Kenzo amewalaumu wasanii wakongwe kwa migawanyiko inayohushudiwa kwa sasa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Mwimbaji huyo ambaye ni mshindi wa Tuzo ya BET mwaka wa 2015 anaamini wanamuziki wakongwe wameshindwa kuwaleta wasanii pamoja jambo ambalo limepelekea wasanii wa kizazi kipya kujigawa kwenye makundi mbali mbali. Lakini pia amesema viongozi wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA) hawana budi kuweka kando maslahi yao binafsi na kufanya kazi kuelekea ustawi wa wanamuziki wote. “Nina tatizo na chama, nadhani hakiko kwenye njia sahihi. Imezua mgawanyiko miongoni mwa wanamuziki katika tasnia hii. Viongozi lazima wazingatie kufanya kazi kwa manufaa ya wanamuziki wote,” aeleza. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” amethibitisha kuwa hatashiriki katika uchaguzi ujao wa UMA.

Read More
 EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

EDDY KENZO AAPA KUMALIZA UGOMVI WA KING SAHA NA BEBE COOL

Staa wa muziki nchini Uganda,Eddy Kenzo amefichua kuwa ugomvi unaoendelea kati ya Bebe Cool na King Saha unamchukiza. Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amesema wasaniii wanapaswa kuacha kutupiana maneno makali mtandaoni na badala yake waungane kwa ajili kuupeleka muziki wà Uganda kimataifa. “I hate the negativity in this industry. I don’t like artists who fight each other. We don’t need a divided industry. We need to grow first and conquer the international market,” Amesema Eddy kenzo ameahidi kuwaleta pamoja King Saha na Bebe Cool ambao wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu kwa kuwa ni marafiki zake. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” ameeleza kuwa tasnia ya muziki nchini Uganda bado ni changa hivyo wasanii wanapaswa kuelekeza nguvu zao kubuni njia za kuingiza kipato na kutoa muziki mzuri badala kupigana vita. “I will work to unite the two because I speak to both. Artists ought to know our industry is still young, we should unite and fight brokenness instead of fighting one another,”  Ameongeza King Saha na Bebe Cool wamekuwa kwenye ugomvi tangu bebe cool amshauri aachane na matumizi ya dawa za kulevya la sivyo atapotea kimuziki. King Saha alikasirisha na kauli hiyo ambapo amekuwa akimchana Bebe Cool kwenye mahojiano mbali mbali na hata akaachia disstrack iitwayo Zakayo ambayo inalenga bossi huyo wa Gagamel. Eddy Kenzo kipindi cha nyuma alikuwa kwenye ugomvi na Bebe Cool lakini baadae wakakuja wakamaliza tofauti zao ambapo kwa sasa wana uhusiano mzuri wa kufanya kazi pamoja.        

Read More
 EDDY KENZO AJUTIA KUMPIGA SHABIKI NA MIC, AOMBA RADHI

EDDY KENZO AJUTIA KUMPIGA SHABIKI NA MIC, AOMBA RADHI

Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Kenzo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kufeli kudhibiti hasira yake kwenye onesho lake huko Bwera, Kasese. Kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Kenzo anaonekana akimrushia shabiki kipaza sauti kwa madai ya kumwagia kinywaji akiwa jukwaani. Kenzo amesema kinywaji hicho kilikuwa kimechanganywa na kilevi na harufu yake mbaya ndio ilimfanywa akapandwa na hasira. Licha ya kuwa alisema kwamba hajutii kitendo cha kumpiga shabiki na kipaza sauti, msanii huyo ameamua kuwaomba radhi mashabiki zake akisema kuwa anajutia maamuzi aliyoyachukua ikizingatiwa kuwa yeye ni kioo cha jamii. “My fans expect better from me. I know and I regret my actions. I think this guy was sent by people who want to taint my image, but it’s fine. I forgive him,” says Eddy Kenzo. Utamkumuka Septemba mwaka wa 2014 Kenzo alimshushia kichapo cha mbwa mtangazaji wa Dembe FM Isaac Katende maarufu kama Kasuku kwenye mkao na wanahabari huko Centenary Park kwa madai ya kumzungumzia vibaya.

Read More
 EDDY KENZO AVUNJA KIMYA JUU YA KUMPIGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI

EDDY KENZO AVUNJA KIMYA JUU YA KUMPIGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI

Mwanamuziki Edrisa Musuuza maarufu  Eddy Kenzo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya kumtwanga shabiki na kipaza sauti kwenye moja onesho lake juzi kati. Akizungumza kuhusu tukio hilo Eddy Kenzo amesema hakufurahishwa na kitendo cha shabiki kumwagia pombe akiwa jukwaani jambo ambalo lilimkasirisha na akajipata amemrushia kapaza sauti kwani kinywaji hicho kilikuwa kinatoa harufu mbaya. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” ametejitea namna ambavyo alichukulia tukio hilo kwa kusema kwamba hapendi kabisa kuvunjiwa heshima kwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao wanapenda sana amani. Utamkumuka Septemba mwaka wa 2014 Kenzo alimshushia kichapo cha mbwa mtangazaji wa Dembe FM Isaac Katende maarufu kama Kasuku kwenye mkao na wanahabari huko Centenary Park kwa madai ya kumzungumzia vibaya.

Read More
 EDDY KENZO AMTWANGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI HADI AKAPOTEZA FAHAMU.

EDDY KENZO AMTWANGA SHABIKI NA KIPAZA SAUTI HADI AKAPOTEZA FAHAMU.

Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Kenzo ameingia kwenye vichwa vya habari Afrika Mashariki mara baada ya kuripotiwa kumtwanga na kipaza sauti shabiki yake mmoja kwenye moja ya show yake juzi kati. Inasemekana kuwa nguvu ya kipaza hiyo ilitosha kumuangusha chini shabiki huyo ambaye alibamiza kichwa chini baada ya kuanguka na kulala kabla ya walinzi wa Eddy Kenzo kumkamata na kumtupa nje ya ukumbi ambao msanii huyo alikuwa akitoa burudani. Inadaiwa kuwa chanzo cha purukushani hiyo ni baada ya shabiki huyo kumwagia kinywaji Eddy Kenzo alipokuwa jukwaani akitumbuiza wimbo wake wa Enjoyment, kitendo ambacho kilimkasirisha msanii huyo ambaye yupo kwenye ziara ya kimuziki na kuamua kumrushia kipaza sauti. Utakumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Eddy Kenzo kujipata kwenye msala kama huo, amewahi pia kumzaba makofi mtangazaji mmoja wa redio nchini Uganda baada ya kumharibia jina kwa kusema kwamba Eddy Kenzo sio msanii mwenye kipaji kwani aliandikiwa wimbo wake uitwao Syemkozi na prodyuza aitwaye Ronnie, madai ambayo mwanamuziki huyo alikanusha vikali.

Read More
 EDDY KENZO ALAMBA SHAVU YA UBALOZI UGANDA WILDLIFE AUTHORITY (UWA)

EDDY KENZO ALAMBA SHAVU YA UBALOZI UGANDA WILDLIFE AUTHORITY (UWA)

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo ameingia ubia wa kufanya kazi na Mamlaka ya Wanyama pori nchini Uganda UWA kwa ajili ya kutangaza mbuga za wanyama kimataifa Eddy Kenzo amelamba dili hilo nono wiki moja iliyopita na  sasa anaendelea na harakati za kuaandaa maudhui  yatakayotumiwa kutangaza utalii nchini Uganda duniani. Utakumbuka kipindi cha nyuma Eddy Kenzo amefanya kazi kama balozi wa utalii nchini Uganda na Kenya mtawalia. Eddy kenzo ni moja kati ya wasanii wanaotangaza muziki wa Uganda na Afrika Mashariki kimataifa shukran kwa wimbo wake Sitya Loss ambayo ilimfungulia milango mwaka wa 2014.

Read More
 EDDY KENZO AMSHIKA MKONO CLEVER J BAADA YA KUTOSWA NA NDUGU ZAKE

EDDY KENZO AMSHIKA MKONO CLEVER J BAADA YA KUTOSWA NA NDUGU ZAKE

Staa wa muziki kutoka Uganda Eddy Kenzo ameamua kumsaidia msanii mwenzake Clever J baada ya ndugu zake kumtelekeza. Eddy kenzo ambaye juzi kati alitumbuiza pamoja na Clever J kwenye show ya Comedy Gate, aliamua kumpa msanii huyo pesa zote alizopewa na mashabiki kama njia ya kumsaidia kijikwamua kimaisha. Hatua hiyo ya Eddy kenzo wengi wametafsiri kama kejeli kwa ndugu zake Chameleone na Pallaso ambao wamekuwa wakitumia jina la Clever J kujipatia pesa. Clever J anatarajiwa pia kutumbuiza kwenye tamasha la Eddy Kenzo mwezi Novemba mwaka huu kama njia ya kujipatia kipato ya kujiendeleza kimaisha.

Read More
 EDDY KENZO AFUNGUKA JUU YA KUWANIA URAIS WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

EDDY KENZO AFUNGUKA JUU YA KUWANIA URAIS WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA UMA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo ana wafuasi wengi ambao wanamwamini katika muziki wake. Mwimbaji huyo amefichua kuwa aliwakatisha tamaa wasanii waliomtaka ajitoze kwenye uongozi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA. Akizungumza katika mahojiano na runinga moja nchini humo, bosi huyo wa Big Talent ameeleza kuwa wasanii tofauti walimsihi kugombea wadhfa wa urais katika chama hicho kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni lakini alikataa. Hitmaker huyo wa ngoma “Nsimbudde” anaamini kuwa anaweza kuwatumikia wanamuziki wenzake hata bila kupewa nafasi yoyote katika tasnia ya muziki nchini uganda. “Nilifuatwa na wanamuziki wengi wakiniomba nigombee urais wa UMA lakini nilikataa, si lazima niwe ofisini ni watumikie, mimi si mwanachama kiherehere wa UMA lakini naunga mkono Chama hicho na kuitakia mema,” alisema. . Mapema wiki hii, Eddy Kenzo alimuidhinisha Msanii mwenzake King Saha kugombea urais wa cha cha UMA ambacho pia kinang’ang’aniwa na rais wa sasa chama hicho Cindy Sanyu.

Read More