Ringtone Apoko amchana Eric Omondi kwa kutumia mbwa wake kutafuta umaarufu

Ringtone Apoko amchana Eric Omondi kwa kutumia mbwa wake kutafuta umaarufu

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko amemtolea uvivu Eric Omondi baada ya mchekeshaji huyo kutamba na mbwa wake kwenye uzinduzi wa onesho la Laugh & Jazz mwishoni mwa juma lillopita. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone amedai kuwa Omondi alimuomba mbwa hao kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini. Hitmaker huyo wa “Ombi Langu” amesema licha ya kumsaidia Omondi kufanikisha jambo lake amekerwa na kitendo cha mchekeshaji huyo kumregeshea mbwa wake wakiwa wachafu na wachovu. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemuashia moto Ringtone kwa madai ya kutafuta kiki kupitia jina la Omondi.

Read More
 Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest

Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest

Mwimbaji mkuu wa Sauti Sol Bien-Aime Baraza amempiga marufuku mchekeshaji Eric Omondi kuhudhuria tamasha lijalo la Sol Fest. Katika taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bien ameweka wazi kuwa Omondi hataruhusiwa katika ukumbi wa hafla hiyo kutokana na kitendo chake cha kuwazungumzia vibaya wasanii wa Kenya. Hitmaker huyo wa “Inauma” ameongeza kuwa tayari wameagiza timu yao ya usalama kumzuia Omondi kuingia katika ukumbi wa tamasha lao la kila mwaka. “Eric, mdomo wako mkubwa umekuponza! Usiwalaumu wanamuziki. Hakuna mtu anayetaka kukuona kwenye Sol Fest kwa hivyo tafadhali kaa mbali!!!”, “Timu ya usalama ya Sol fest africa asubuhi ya leo imepokea maagizo makali ya kutoruhusu huyu jamaa na mbwa wake waliokopwa, karibu na ukumbi wa tamasha!.. “Binafsi, nimewasilisha zuio dhidi yake. Kwa hiyo, nawasihi nyote mumuepuke kama majanga!!!, Aliandika Instagram. Hata hivyo, Eric Omondi alijibu kwa kusema kwamba anataka tiketi 20 za VIP na mbwa wake kupewa ulinzi maalum atakapohudhuria Sol Fest Disemba 9 mwaka huu. Onyo hilo la Bien linajiri saa chache baada ya Omondi kusema kwamba atahitaji mbwa wasiopungua 20 ili aweze kuhudhuria Sol Fest kutokana na maisha yake kuwa hatarini. Eric Omondi amekuwa akiwashambulia wasanii wa Kenya kila mara akisema kuwa wamezembea kwenye suala la kutoa nyimbo na kupelekea wasanii wageni kutawala tasnia ya muziki nchini.

Read More
 Mchekeshaji Eric Omondi akanusha madai ya kutomlipa Shakilla

Mchekeshaji Eric Omondi akanusha madai ya kutomlipa Shakilla

Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kumtolipa Shoshalaiti maarufu mtandaoni Shakilla kwa kumshirikisha kwenye kipindi cha wife material. Kwenye mahojiano na Ankali Ray amesema wanawake wote walioshirikishwa kwenye kipindi hicho walilipwa shillingi Ksh. 18,000 kila mmoja akiwemo Shakilla pamoja na Cartoon Comedian. “Nililipa , I swear I paid her . Alilipwa 18 thousand …Shakilla alikua na tabia mbaya sana , alikua ananifuata kwa kila room ,… sijalala na mtu yote.”, Alisema. Kauli ya Omondi imekuja mara baada ya mrembo huyo kumshutumu kuwa alimtumia vibaya kwenye shughuli zake kwa manufaa yake binafsi bila kumlipa chochote. “Eric amenitumia vibaya kwa njia nyingi sana. Hakunilipa wala mtu yeyote aliyeshiriki kipindi cha wife material,” Alisema.

Read More
 Mchekeshaji Eric Omondi avunja kimya chake baada ya mpenzi wake kupoteza ujauzito

Mchekeshaji Eric Omondi avunja kimya chake baada ya mpenzi wake kupoteza ujauzito

Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kutumia suala la mchumba wake kupoteza uja uzito kutafuta kiki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni madai hayo hayana ukweli wowote kwani alikuwa anajaribu kuwapa vijana wenzake changamoto ikitokea wapenzi wao wamejipata kwenye hali ya kuaharibikiwa na uja uzito. Utakumbuka mapema wiki hii Eric Omondi alichapisha video ikimuonyesha mpenzi wake akilia kwa uchungu akiwa hospitalini baada ya uja uzito wake kuaharibika( Miscarriage). Hata hivyo Omondi alipata ukosoaji mkubwa kutoka kwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wakihoji kuwa mchekeshaji huyo alikosea sana kuweka video hiyo mtandaoni.

Read More
 Eric Omondi awaonya mapromota dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni

Eric Omondi awaonya mapromota dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni

Mchekeshaji Eric Omondi amewaonya mapromota wa muziki dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni  kutumbuiza nchini Kenya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi ameapa kupambana na promota  atakayekwenda kinyume na agizo lake kwa kuhakikisha tamasha lake la muziki linasambaratika. Aidha mchekeshaji huyo amesitikishwa na kitendo cha mapromota kujihusisha visa vya kuwatapeli wasanii wa mataifa mengi, jambo ambalo amedai huenda ikachafua taswira ya taifa la kenya kwenye jamii ya kimataifa. “This is MY ORDER to all PROMOTERS in this Country!!! DO NOT!!! and I repeat DO NOT invite anymore Foreign Artists until we have Order. First of all you are killing our own and then secondly you are shaming us Abroad!! DO NOT!!! And if you Try I’ll ensure your EVENT FLOPS!!! TRY ME IDIOTS😡😡😡😡 TRY ME!!!”, Ameandika. Kauli ya Eric Omondi imekuja mara baada ya msanii wa Amapiano kutoka Afrika kusini DJ Chichi kukwama nchini kwa kipindi cha mwezi mmoja kufuatia hatua ya promota aliyempa mwaaliko kushindwa kugharamia mahitaji yake ya msingi.

Read More
 Eric Omondi aapa kukita kambi nje ya bunge kushinikiza mageuzi kwenye muziki wa Kenya

Eric Omondi aapa kukita kambi nje ya bunge kushinikiza mageuzi kwenye muziki wa Kenya

Mchekeshaji Eric Omondi ameapa kwa kauli moja kuwa kabla ya mwaka huu kuisha mswada wake wa kucheza asilimia ya muziki wa Kenya kwenye vyombo vya habari utapatishwa kuwa sheria. Katika mkao na wanahabari Omondi amesema kuanzia wiki ijayo atakita kambi nje ya majengo ya bunge kuhakikisha mswada huo unapitishwa kabla ya rais William Ruto kutia saini na kuwa sheria. Aidha amepuzilia mbali madai ya baadhi ya wasaniii wanaodai kuwa anatumia maswada huo kutafuta kiki kwa kusema kuwa lengo lake kuuu ni kuleta mageuzi kwenye muziki wa Kenya ikiwemo wasanii kupewa kipau mbele kwenye matamasha ya muziki na nyimbo zao kupigwa kwenye vituo vya radio na runinga. Utakumbuka tangu Eric Omondi aanzishe mjadala wa kuleta mageuzi kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya amepata ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu huku wakitamka akome kuingilia masuala ya wanamuziki wakati faini yake ni ucheshi.

Read More
 Eric Omondi amjibu Ringtone kuhusu kazi ya Kshs. 50,000 kwa mwezi

Eric Omondi amjibu Ringtone kuhusu kazi ya Kshs. 50,000 kwa mwezi

Mchekeshaji Eric Omondi ameamua kumjibu Ringtone Apoko mara baada ya mwimbaji huyo kumkejeli kuwa ana mpango wa kumpa kazi ya shillingi Kshs.50,000 kwa mwezi. Kwenye mahojiano na Ankaliray katika kipindi cha Uhondo wa Milele FM, Omondi amesema hawezi kataa ofa ya kuajiriwa na Ringtone ila ana shauku ni wapi haswa mwimbaji huyo atatoa pesa za kumudu mshahara wake ikizingatiwa kuwa kodi ya nyumba anayoishi ni shillingi 45,000 kwa mwezi. Mchekeshaji huyo ameenda mbali na kudai kuwa Ringtone alifurushwa kwenye nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi mtaani Runda miezi sita iliyopita na sasa anaishi kwenye nyumba ya kupanga huko South C viungani mwa jiji la Nairobi. “Mimi kazi sijakataa, ila nyumba hata hana. Kwani hujui stori ya Ringtone. Nyumba ali auctioniwa. Anaishi South C- mi si najua kwake. Analipa aje 50,000 na rent yake ni 45,000.” Alisema Eric Omondi. Kauli ya Eric Omondi inakuja mara baada ya Ringtone kumtolea uvivu akiwa kwenye kipindi cha the Trend ya NTV ambapo alidai kuwa yupo tayari kumlipia mchekeshaji huyo shillingi 50,000 kwa mwezi kama mfanyikazi wake nyumbani ili aweze kumsaidia kufanya usafi kwenye mjengo wake wa kifahari huko mtaani Runda.

Read More
 “Niko tayari kumuajiri na kumlipa  Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

“Niko tayari kumuajiri na kumlipa Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko ameendelea kumuwashia moto mchekeshaji Eric Omondi baada ya kudai kuwa yuko tayari kumuajiri kama mfanyikazi wake wa nyumbani. Kwenye mahojiano na The Trend Ringtone amesema atamlipa Omondi shillingi millioni 50,000 kwa mwezi kwa kuwa amekuwa akiigiza kuishi maisha ya kifahari mtandaoni ambayo kwa mujibu wake hawezi kumudu. Katika hatua nyingine amemtolea uvivu mchekeshaji huyo kwa kusema kuwa hana kipaji cha ucheshi kwani amekuwa akitumia muda wake mwingi kukosoa shughuli za watu ili azungumziwe mtandaoni. Ringtone Apoko ambaye amekuwa akijinasibu kuwa msanii tajiri nchini Kenya, kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Ombi Langu” akiwa amewashirikisha wasanii wa kundi la Zabron Singers kutoka nchini Tanzania.

Read More
 Eric Omondi akanusha kutumia mjadala wa kufufua muziki wa Kenya kujitafutia umaarufu

Eric Omondi akanusha kutumia mjadala wa kufufua muziki wa Kenya kujitafutia umaarufu

Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kutumia mjadala wa kuifufua muziki wa Kenya kujitafutia umaarufu. Akipiga stori na podcast ya Captain Nyota Omondi amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ana umaarufu mkubwa kuliko msanii yeyote hapa nchini huku akisisitiza kuwa anatumia ushawishi alionao kwa sasa kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Kenya ambao kwa mujibu wake umeshuka kwa asilimia kubwa. Mchekeshaji huyo amesema wasanii wa Kenya hawana ubunifu kwenye uandaaji wa video zao za muziki kwa kuwa wameshindwa kutofautisha kati ya kuwa wabunifu na kiki, jambo ambalo amedai limewapelekea baadhi ya kuachia muziki usiokuwa na ubora. Hata hivyo amewataka wasanii kujifunza kutoka kwa wasanii wa Nigeria na Tanzania ambao mara nyingi uwekeza pesa nyingi kwenye utayarishaji wa kazi zao kama njia moja wapo ya kuongeza nakshi kwenye nyimbo zao.

Read More
 Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Msanii wa Sauti Sol, Bien amemtolea uvivu mchekeshaji Eric Omondi kwa kukosoa wasanii wa kenya kutokana na kuzembea kuachia nyimbo. Kupitia ukurasa wake wa instagram bien amemtaka Omondi akome kuwashinikiza wasanii wa Kenya waachie muziki mzuri wakati uchekeshaji umemshinda. Mkali huyo wa ngoma ya “Inauma” amemtaka Omondi kuwekeza nguvu zake kwenye suala la kufufua tasnia ya ucheshi ambayo kwa mujibu wake imepoteza mwelekeo. Hata hivyo mashabiki wameonekana kumuunga mkono Bien huku wengine wakimtaka msanii huyo akubali ukweli muziki wa kenya umeshuka kwa kuwa wasanii hawatoi nyimbo nzuri ikilinganishwa na wasanii wa mataifa mengi. Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Eric Omondi kushangazwa na hatua ya wasanii wa Kenya kushindwa kuingiza nyimbo nyingi kwenye chati ya muziki ya Apple Music ambayo imetawaliwa na wasanii wa Nigeria.

Read More
 ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

Mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amekoshwa na kile kinachoendelea mtandaoni kati ya msanii Willy Paul na Jovial. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amewapongeza wawili hao kwa hatua ya kuhalalisha mahusiano mtandaoni kitendo ambacho amehoji ni ubunifu wa hali ya juu wa kutengeneza matukio yatakayowasaidia kutangaza muziki wao mtandaoni. Mchekeshaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake. Hata hivyo amewapa changamoto wasanii kuwa wabunifu ili kutengeneza maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao na kupitia njia hiyo wataweza kushinda na wasanii wa kimataifa.

Read More
 ERIC OMONDI ATOA SOMO KWA WANAUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

ERIC OMONDI ATOA SOMO KWA WANAUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

Mchekeshaji Eric Omondi amewashauri wanaume kutokumbatia mpango wa uzazi wa kukata mishipa ya uzazi maarufu kama Vasectomy. Kwenye mahojiano na mpasho Omondi amesema hakubaliani na njia hiyo ya upangaji uzazi kwa kuwa inamzuia mwanaume kutekeleza wajibu wake wa kujaza dunia kwa kuzaa watoto wengi kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu. Utakumbuka juzi kati msanii Bien wa Sauti Sol alikiri hadharani kuwa yupo tayari kumsaidia mke wake kupanga uzazi kwa njia ya kukata mshipa wake wa uzazi maarufu kama Vasectomy kwani wanaume wengi katika nchi za kiafrika wamewaachia akina mama jukumu hilo.

Read More