ERIC OMONDI AWAPA SOMO WASANII WA KENYA KUJITUMA ZAIDI
Mchekeshaji Eric Omondi amewashauri wasanii kuwa na uthubutu katika kazi zao ili waweze kufikia malengo yao. Akizungumza na Mungai Eve msanii huyo amesema kuwa kupitia sanaa ya ucheshi aliyoifanya kwa muda mrefu amejifunza zaidi kuthamini kile anachokifaanya na kujenga maudhui ambayo yanafurahisha jamii, kitu ambacho kimempa umaarufu zaidi. Katika hatua nyingine Omondi amewasisitiza wasanii kuichukulia sanaa kama kazi nyingine huku akiwataka wajenge tabia ya kuwekeza na kuweka akiba. Hata hivyo amewataka wasanii wanaochipukia kuwa na subira, uvumilivu pamoja na kufanya kazi zenye manufaa na kujenga zaidi jamii zao badala ya kuwa na fikra za kutaka kuwa matajari haraka.
Read More