Video ya Eric Omondi na Mtu Anayefanana naye Yazua Gumzo Mtandaoni

Video ya Eric Omondi na Mtu Anayefanana naye Yazua Gumzo Mtandaoni

Mchekeshaji na Mwanaharakati, Eric Omondi, amewashangaza mashabiki wake baada ya kukutana ana kwa ana na jamaa anayefanana naye kwa kiasi kikubwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric amepakia video akionekana pamoja na kijana huyo wanaofanana kimwonekano, wakiwa wanashiriki matangazo ya kibiashara. Video hiyo imezua gumzo kubwa mtandaoni, mashabiki wengi wakishangaa kufanana kwao kiasi cha wengine kushindwa kutofautisha yupi ni Eric halisi. Mashabiki wamefurahishwa na hatua ya Eric kukutana na pacha wake, huku wengine wakisifu ubunifu wake wa kutumia tukio hilo kama fursa ya kibiashara. Tukio hilo limejiri siku chache tu baada ya Eric kutangaza hadharani kwamba alikuwa akimtafuta kijana huyo anayedaiwa kutoka Githurai, Nairobi, kufuatia video iliyosambaa ikimuonyesha jamaa huyo akionekana kama nakala halisi ya mchekeshaji huyo.

Read More
 Eric Omondi Awataka Wasanii Kusimama na Wananchi Katika Masuala ya Utawala

Eric Omondi Awataka Wasanii Kusimama na Wananchi Katika Masuala ya Utawala

Mchekeshaji na mwanaharakati wa Kenya, Eric Omondi, ametoa wito kwa wasanii kuweka maslahi ya wananchi mbele na kusimama nao katika masuala yanayohusu utawala na mabadiliko ya kijamii. Kupitia video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Omondi amesisitiza kuwa ni wananchi wanaowawezesha wasanii kustawi kwa kuhudhuria matamasha yao na kununua kazi zao, hivyo ni muhimu wasanii nao kuwa upande wa wananchi. Amesema kuwa kuna upepo wa mabadiliko unaovuma barani Afrika ambao utaifagia mifumo kandamizi, na kwamba yeyote atakayejaribu kuukandamiza ataondolewa. Ameongeza kuwa viongozi na wasanii wanapaswa kumtumikia mwananchi kwani vijana wanapigania mustakabali wao, hivyo wasanii hawapaswi kukaa kimya bali waunge mkono harakati hizo. Mchekeshaji huyo ameeleza kuwa hali hiyo ni funzo kwa wasanii barani Afrika kuzingatia sauti ya wananchi badala ya kujiweka karibu na mifumo ya kisiasa inayopingwa na raia. Eric Omondi ametolewa kauli hiyo mara baada ya wananchi nchini Tanzania kupinga kuchaguliwa kwa serikali ya CCM, iliyokuwa ikiungwa mkono na wasanii wengi wakubwa nchini humo.

Read More
 Mwanaume wa Kenya Afichua Alimdanganya Mkewe kwa Mwaka Akijifanya Eric Omondi

Mwanaume wa Kenya Afichua Alimdanganya Mkewe kwa Mwaka Akijifanya Eric Omondi

Mwanaume mwenye sura inayofanana na mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi, amekiri kuwa aliishi katika uhusiano wa kimapenzi kwa mwaka mmoja akijifanya kuwa yeye ndiye mchekeshaji huyo halisi. Kwa mujibu wa mahojiano yaliyosambaa mtandaoni, amesema kuwa alikutana na mwanamke huyo mtandaoni na wakaanza mahusiano, huku akitumia umaarufu wa Eric Omondi kumvutia na kumfanya aamini kuwa anachumbiana na staa huyo. Mwanaume huyo amesema kwa muda wa mwaka mmoja, alidumisha uongo huo kwa kutumia picha na video za Eric Omondi mitandaoni, jambo lililomfanya mwanamke huyo asiwe na shaka. Baada ya muda, ukweli ulifichuka na mpenzi wake kugundua kuwa alikuwa akiishi na mtu tofauti kabisa. Mwanaume huyo amekiri kosa hilo akisema kuwa hakupanga kumuumiza mwanamke huyo, bali alijikuta akizama zaidi katika uongo huo kutokana na hofu ya kumpoteza. Amesema alianza kama mzaha, lakini baadaye mambo yakachukua mwelekeo tofauti.

Read More
 Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Eric Omondi Aanza Harakati za Kumtafuta Jamaa Anayefanana Naye

Mchekeshaji na mwanaharakati, Eric Omondi, ameomba msaada wa kumtafuta kijana anayefanana naye, ambaye video yake imesambaa mtandaoni nchini Kenya. Kupitia kipande cha video alichopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Eric ameeleza kuwa anataka kumpata kijana huyo ili wawe wawili, akitania kwamba mmoja wao anaweza kushiriki kwenye maandamano huku mwingine akiendelea na kazi zake za kawaida. Kijana huyo ambaye anadaiwa kutoka Githurai, Kenya, alipata umaarufu ghafla baada ya video yake kusambaa ambapo alinukuliwa akisema kuwa anatamani kukutana na Eric Omondi. Wafuasi wengi mitandaoni wamekuwa wakimtag Eric kwenye video hiyo wakimtaka atimize ombi hilo. Hadi sasa Eric Omondi hajaweka wazi kama amepata mawasiliano ya kijana huyo, lakini mashabiki wanatarajia kuona mkutano wao, ambao wengi wanaamini utazua kicheko na kufunika mitandao

Read More
 Eric Omondi Asema Kuzaliwa kwa Kenya Mpya Ni Jambo Lisilozuilika

Eric Omondi Asema Kuzaliwa kwa Kenya Mpya Ni Jambo Lisilozuilika

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi amesema kuwa kuzaliwa kwa Kenya mpya ni jambo lisiloweza kuzuilika, akieleza kuwa kizazi kipya kinachojitokeza sasa ni cha Wakenya wasioangalia ukabila, bali umoja na mabadiliko. Kupitia ujumbe wake Instagram, Omondi amesema kuwa “The birth of a new Kenya is inevitable”, akisisitiza kuwa taifa la Kenya linaingia katika kipindi kipya cha mageuzi ya kijamii na kisiasa ambacho kitavunja ukabila, ufisadi, na tamaa ya mali. Eric anaamini kuwa kizazi kipya cha Wakenya kimeamka na kiko tayari kupigania taifa lenye haki, usawa na uwajibikaji. Kwa mujibu wake, mabadiliko haya hayatategemea wanasiasa wa jadi, bali vijana na raia wa kawaida wanaotaka kuona Kenya yenye amani na maendeleo. Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Omondi kuzindua kampeni maalum ya kuhamasisha vijana katika vyuo vikuu kujisajili kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Kampeni hiyo inalenga kuongeza ushiriki wa vijana katika maamuzi ya kisiasa na kuhakikisha sauti yao inasikika kwenye mustakabali wa taifa.

Read More
 Eric Omondi Asema Vijana Ndio Nguzo ya Kutimiza Ndoto ya Raila

Eric Omondi Asema Vijana Ndio Nguzo ya Kutimiza Ndoto ya Raila

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Eric Omondi, ametoa wito kwa vijana wa taifa hilo kusimama pamoja kwa umoja na kuendeleza urithi wa hayati Raila Odinga kwa vitendo. Kupitia ujumbe wake kwa vijana, Eric amesema kuwa wakati taifa la Kenya linaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo, ni jukumu la vijana kutimiza yale yote ambayo Raila alianza lakini hayakukamilika enzi za uhai wake.. Mchekeshaji huyo aliyegeukia uanaharakati, amesema vijana wa Kenya wana fursa kubwa kumaliza kazi hiyo, kwani wao ndio nguvu kuu ya taifa na walikuwa sehemu muhimu ya maono ya Raila kuhusu haki, umoja na maendeleo. Kauli ya Omondi inakuja wakati amekuwa akiendeleza kampeni za kuwarai vijana wa Gen Z kujisajili kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, akisisitiza kuwa ni kupitia kura pekee ndipo vijana wataweza kutimiza maono na ndoto ya Kenya mpya yenye usawa, matumaini na haki kwa wote.

Read More
 Eric Omondi Akanusha Vikali Tuhuma za Kutoa Kafara Shalkidoh

Eric Omondi Akanusha Vikali Tuhuma za Kutoa Kafara Shalkidoh

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi amefunguka kwa uchungu baada ya tuhuma zilizozagaa mtandaoni zikidai kuwa alimtoa kafara msanii Shalkidoh aliyezikwa jana nyumbani kwao kaunti ya Kiambu. Akizungumza kufuatia tetesi hizo, Eric amekanusha vikali madai hayo, akisema ni uvumi wa kupotosha unaolenga kuharibu jina lake na juhudi zake za kusaidia watu. Amesema kuwa hajawahi kujihusisha na mambo ya ushirikina bali anatenda mema kwa nia ya dhati kusaidia jamii. Eric ameongeza kuwa maneno ya watu hayawezi kumkatisha tamaa, na ataendelea kuwasaidia Wakenya wenye uhitaji bila kuogopa maneno ya chuki au fitna. Hata hivyo amesema lengo lake ni kuona vijana wanapata fursa bora za maisha kupitia miradi na kampeni zake za kijamii, akisisitiza kuwa atabaki kuwa sauti ya matumaini kwa waliokata tamaa. Kauli ya Eric Omondi imekuja mara baada ya walimwengu mtandaoni kudai kuwa huenda mchekeshaji huyo alihusika na kifo cha Shalkidoh, ikizingatiwa kuwa pikipiki aliyompa kama msaada ndiyo iliyosababisha ajali iliyomtoa uhai.

Read More
 Eric Omondi Aifariji Familia ya Odinga Kufuatia Kifo cha Raila

Eric Omondi Aifariji Familia ya Odinga Kufuatia Kifo cha Raila

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi amejitokeza kuonyesha heshima na kutoa pole kwa familia ya marehemu Raila Odinga kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa Kenya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eric ameposti video akionekana nyumbani kwa familia ya Odinga eneo la Karen, Nairobi, akimfariji Mama Ida Odinga. Katika video hiyo, alionekana akiwa na uso wa huzuni huku akishikana mikono na Mama Ida katika ishara ya faraja. Eric amesema alimtembelea Mama Ida jana jioni ili kuomboleza pamoja naye na kuwataka Wakenya waendelee kuiweka familia ya Odinga kwenye maombi, akisisitiza kuwa wanahitaji nguvu kubwa katika kipindi hiki kigumu. Kifo cha Raila kimeendelea kugusa nyoyo za Wakenya kutoka nyanja mbalimbali, huku viongozi, wasanii na wananchi wa kawaida wakiendelea kuonyesha huzuni na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Odinga.

Read More
 Eric Omondi Awahimiza Wasanii Kuhudhuria Ibada ya Wafu ya Marehemu Shalkido

Eric Omondi Awahimiza Wasanii Kuhudhuria Ibada ya Wafu ya Marehemu Shalkido

Mchekeshaji na mwanaharakati Eric Omondi ametoa wito kwa wasanii nchini Kenya kuhudhuria ibada ya wafu ya marehemu msanii wa Gengetone Shalkido, itakayofanyika Jumatano tarehe 15, katika kanisa la All Saints Cathedral, Nairobi, kuanzia saa 11:30 asubuhi. Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Eric amewahimiza wasanii wa Kenya kuonyesha umoja na upendo kwa kuhudhuria ibada hiyo, akisema kuwa ni muhimu kwa wasanii kusimama pamoja hasa nyakati za huzuni. Eric ameongeza kuwa ibada hiyo si tu ya kumuaga Shalkido, bali pia ni ishara ya mshikamano katika tasnia ya muziki wa Kenya. amesema wasanii wanapaswa kuacha tofauti zao pembeni na kuungana katika maombi na heshima za mwisho kwa marehemu. Ibada hiyo inatarajiwa kuwaleta pamoja wasanii, wadau wa muziki, na mashabiki wengi watakaoungana kumuaga Shalkido kwa heshima na upendo kabla ya mazishi yake baadaye wiki hii. Ikumbukwe Shalkido, aliyepata umaarufu kupitia kundi la Sailors Gang, alifariki dunia hivi karibuni kufuatia ajali mbaya ya barabarani.

Read More
 Eric Omondi Azindua Ziara ya Vyuo Vikuu Kuhamasisha Gen Z Kujisajili Kama Wapiga Kura

Eric Omondi Azindua Ziara ya Vyuo Vikuu Kuhamasisha Gen Z Kujisajili Kama Wapiga Kura

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii kutoka Kenya Eric Omondi ameanzisha rasmi kampeni ya kitaifa yenye lengo la kuhamasisha vijana wa kizazi cha Gen Z kujisajili kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Kupitia hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Pwani, Kaunti ya Kilifi, Eric amesema kuwa kampeni hiyo ni ya kihistoria kwa taifa la Kenya kwani inaashiria mwanzo wa safari ya kuleta mabadiliko ya kisiasa kupitia ushiriki wa vijana. Omondi ameeleza kuwa kampeni hiyo inalenga kutembelea vyuo vikuu vyote nchini humo ili kuhakikisha vijana wanatumia haki yao ya kidemokrasia kwa kujisajili na kushiriki katika uchaguzi. Mchekeshaji huyo, amesisitiza kuwa ni wakati wa vijana kuamka na kubeba jukumu la kuunda taifa jipya kupitia kura zao, akiahidi kutembelea kila pembe ya Kenya ili kuhakikisha “Kenya Mpya” inajengwa na vijana wenye ari ya mabadiliko. Eric Omondi, ambaye kwa miezi ya hivi karibuni amekuwa akijitokeza kama sauti ya vijana katika masuala ya kijamii na kiuchumi, amesema anaamini kuwa nguvu ya vijana ndiyo nguzo kuu ya mabadiliko nchini humo.

Read More
 Shalkido Apata Msaada Kutoka kwa Eric Omondi

Shalkido Apata Msaada Kutoka kwa Eric Omondi

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi ameonyesha moyo wa kusaidia baada ya kujitokeza kumsaidia msanii wa Gengetone, Shalkido, ambaye hivi karibuni alifichua kuwa maisha yamekuwa magumu kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya familia yake. Mchekeshaji huyo amemkabidhi Shalkido pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya nyumbani ikiwemo unga, sukari na mafuta ya kupikia. Kupitia msaada huo, Eric amesema lengo lake ni kuhakikisha msanii huyo anapata fursa ya kujiinua na kujitegemea tena. Shalkido, anayejulikana zaidi kupitia kundi la Sailors, amepokea msaada huo kwa furaha na shukrani, akisema utampa nafasi ya kurudia katika mstari sahihi wa kujikimu kimaisha. Kitendo cha Eric kimepongezwa na mashabiki wengi mitandaoni wakimtaja kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine na jamii kwa ujumla.

Read More
 Eric Omondi Aanzisha Msako wa Familia Iliyofukuzwa na Mume

Eric Omondi Aanzisha Msako wa Familia Iliyofukuzwa na Mume

Mchekeshaji na mwanaharakati wa kijamii Eric Omondi ameanzisha msako wa kuipata familia iliyoonekana kwenye video ikifukuzwa na mume wake. Video hiyo, ambayo imesambaa sana mtandaoni, inamuonyesha mwanaume akimtoa mke wake na watoto nje ya nyumba huku akionekana kuwa na msimamo mkali wa kutowakubali tena. Omondi alipakia video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii na kueleza wasiwasi wake juu ya namna familia hiyo ilivyodhalilishwa hadharani. Ameeleza kuwa lengo lake kuu kwa sasa ni kuwatafuta ili kuhakikisha wanapata msaada wa haraka na kurejeshewa heshima yao kama binadamu. Kupitia wakfu wake wa Sisi kwa Sisi, Omondi amekuwa akijitolea kusaidia Wakenya wanaopitia changamoto mbalimbali. Wakfu huo tayari umesaidia wagonjwa kulipiwa gharama za hospitali, wanafunzi kupata karo, pamoja na familia zisizo na makazi kupata hifadhi ya muda.  Wachambuzi wanasema hatua ya Omondi inaashiria jinsi watu mashuhuri wanavyoweza kutumia majukwaa yao kushughulikia changamoto za kijamii ambazo mara nyingi hupuuziwa. Wamepongeza hatua yake wakieleza kuwa ni mfano wa kutumia umaarufu kwa njia ya kijamii yenye manufaa. Kwa sasa, jitihada zinaendelea kuhakikisha familia hiyo inapatikana, huku mashirika ya kijamii na mashabiki wa Omondi mitandaoni wakiahidi kushirikiana ili kuharakisha msaada.

Read More