GRAMMY WATANGAZA TAREHE YA TUZO 2023

GRAMMY WATANGAZA TAREHE YA TUZO 2023

Waandaaji wa Tuzo kubwa zaidi za muziki duniani za Grammy, wametangaza rasmi Novemba 15 kuwa ndio siku ambayo watatoa majina na nominations zitakazo patikana katika tuzo hizo. Na hafla ya ugawaji wa tuzo za 65 za Grammy zitafanyika Februari 05 mwaka 2023, mjini Los Angeles ndani ya Crypto Arena. Fahamu, tuzo za Grammy hufanyika kila mwaka nchini Marekani kwa ajili ya kuwatunza wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka uliopita kupitia vipengele mbalimbali kama vile Muimbaji Bora, Mwandishi Bora wa Mashairi, Mtayarishaji Bora wa Muziki, Video Bora ya muziki na zaidi.

Read More
 UONGOZI WA TUZO ZA GRAMMY WATANGAZA TAREHE MPYA YA KUFANYIKA KWA TUZO HIZO KUBWA DUNIANI

UONGOZI WA TUZO ZA GRAMMY WATANGAZA TAREHE MPYA YA KUFANYIKA KWA TUZO HIZO KUBWA DUNIANI

Uongozi wa Tuzo za Grammy umetaja tarehe mpya ya kufanyika hafla ya ugawaji wa Tuzo hizo kwa mwaka 2022 ambapo sasa itafanyika April 3 katika ukumbi wa MGM Grand Jijini Las Vegas nchini Marekani. Awali Tuzo hizo za 64 zilipangwa kufanyika January 31 lakini ziliahirishwa kufuatia tishio la kirusi cha Omicron. Mshereheshaji wa Tuzo za mwaka huu alitajwa kuwa ni mchekeshaji maarufu wa Afrika Kusini, Trevor Noah.

Read More
 TUZO ZA GRAMMY ZAAHIRISHWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO

TUZO ZA GRAMMY ZAAHIRISHWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO

Hafla ya Tuzo za Grammy iliyokuwa ifanyike Januari 31 mwaka huu imeahirishwa kufuatia tishio la kirusi cha Omicron. Waandaaji wa tuzo hizo wametoa taarifa rasmi januari 5 mwaka huu huku tarehe mpya ikiwa bado ni kitendawili. Huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo kwa tuzo hizo kuahirishwa, mwaka jana ziliahirishwa kutoka Januari na kufanyika Machi 14, mwaka wa 2021

Read More
 SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

SAUTI SOL WAPOKEA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA GRAMMY

Kundi maarufu la muziki nchini, Sauti sol limepokea cheti cha utambuzi yaani (Certificate of Recognition) kutoka kwa waandaji wa tuzo za Grammy.   Cheti hicho ni maalum kwa ajili ya ushiriki wao kama watayarishaji kwenye album ya msanii Burna Boy kutoka Nigeria iitwayo “Twice As Tall” ambayo ilishinda tuzo ya Best Global Music Album kwenye tuzo za 63 za Grammy zilizofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.   Sauti sol wameshiriki kwenye uandaaji wa wimbo namba 11 kutoka kwenye album ya “Twice As Tall” uitwao ‘Time Flies’.   Ikumbukwe, Sauti Sol kwa sasa wapo nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yao ya kimuziki baada ya mapumziko ya takribani miaka miwili kutokana na janga la Corona.    

Read More