Kenya yazidi kusonga mbele kuelekea Kombe la Afrika la Wanawake

Kenya yazidi kusonga mbele kuelekea Kombe la Afrika la Wanawake

timu ya taifa ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets, imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Gambia katika mechi ya mkondo wa kwanza wa raundi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake 2026. Mechi hiyo ilichezwa jana kwenye Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, Nairobi. Mechi ya mkondo wa pili itafanyika Jumanne ijayo kwenye Stade Lat Dior jijini Thies, Senegal, kwani Gambia haina uwanja unaokidhi viwango vya CAF. Mshindi wa jumla wa mechi hiyo atapata tiketi ya kufuzu WAFCON 2026, itakayofanyika Morocco kuanzia 17 Machi hadi 3 Aprili mwaka ujao. Rais William Samoei Ruto amewazawadia Starlets shilingi milioni 5 kama motisha ya ushindi huu. Aidha, Rais amewaahidi timu hiyo shilingi milioni 2.5 kwa sare, shilingi milioni 1 kwa kila mchezaji iwapo watashinda kufuzu WAFCON, na shilingi 500,000 kwa kila mchezaji iwapo watafuzu kwa sare. Huu ni ushindi muhimu kwa Starlets, wakijipanga kuendeleza hadhi ya soka la wanawake nchini Kenya na kuendeleza matumaini ya kufuzu fainali za WAFCON mwaka ujao.”

Read More
 Wachezaji kumi na moja wapya waitwa kwenye kikosi cha mwanzo cha Harambee Starlets

Wachezaji kumi na moja wapya waitwa kwenye kikosi cha mwanzo cha Harambee Starlets

Wachezaji kumi na moja wapya wameitwa kwenye kikosi cha mwanzo cha Harambee Starlets ili kuanza maandalizi ya mechi zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake ambapo itamenyana na Tunisia katika mechi ya mikondo miwili kuanzia tarehe ishirini na moja mwezi huu. Kocha mkuu wa Harambee Starlets Bin Odeba amejumuisha kwenye timu hiyo walinda lango Vivian Shionzo wa timu ya Kibera soccer girls na Venda Abongo wa timu ya Kisped Queens katika jitihada za kuboresha kikosi hicho. Safu ya ulinzi ina Elizabeth Ochaka ambaye aliandikisha matokeo bora katika timu ya junior starlet na atajiunga na wachezaji wapya wakiwemo Bernadet Atieno wa Kised Queens Alice Mideri wa Vihega Queza na Tabitha Amoita wa ulinzi Starlets. Wachezaji wengine waliotajwa ni Mary Nthambi wa Kenya polisi na Janet Momo wa Kibera soccer women pamoja na mwenzake Ivona Idagiza miongoni mwa wengine. Timu hiyo itaingia kambini Jumatatu juma lijalo kujiandaa kwa mechi hizo zitakazochezwa tarehe ishirini na moja mwezi huu jijini Nairobi na kisha timu hiyo itasafiri kuelekea Tunisia kwa mechi ya marudiano tarehe ishirini na tano mwezi huu.

Read More