Harmonize amkingia Diamond kwa kukosa show nchini Rwanda
Msanii Harmonize ameonyesha uzalendo kwa kumuombea msamaha msanii mwenzake Diamond Platnumz huko nchini Rwanda kutokana na Diamond kushindwa kufika kwenye show aliyotakiwa aifanye December 23 mwaka jana jijini Kigali, pale BK Arena. Kwenye mahojiano aliyoyafanya na RwandaTV Harmonize mwishoni alikuwa akipewa shukurani ya kufika kwenye kipindi na akatumia nafasi hiyo kuomba msamaha kwa wanyarwanda kwa niaba ya Diamond Platnumz kwa kutokufika kwenye show. Kwenye maelezo yake alisema kuwa hajui tatizo lilikuwa nini lakini kwenye maisha huwezi kujua nini kinatokea hivyo aliwaomba wamsamehe ili tuupeleke muziki wetu wa Afrika Mashariki kwenye hatua inayofuata, japo hakulitaja jina la diamondplatnumz moja kwa moja hali iliyomfanya mtangaazaji kumuuliza ‘Unamaanisha Diamond?” na Harmonize alijibu “yeah yeah”.
Read More