MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA HARMONIZE AWEKA REKODI BOOMPLAY TANZANIA

MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA HARMONIZE AWEKA REKODI BOOMPLAY TANZANIA

Nyota wa muziki nchini Tanzania na mmiliki wa record label ya Konde Gang Harmonize amefanikiwa kufikisha jumla ya streams million 50+ katika mtandao wa boom play music Tanzania. Kwa streams hizo Konde Boy anaungana na wanamuziki wengine wenye zaidi ya streams 50+ katika mtandao huo kama Diamond Platnumz ,Mbosso na Rayvanny ambaye ndiye kinara wa streams Afrika Mashariki. Mpaka sasa mkali huyo wa ngoma ya “Teacher’ ametoa Album mbili ambazo ni Afro East ya mwaka 2020 yenye streams million 2.7 na Highschool ya 2021 yenye streams million 19, na EP moja ‘ inayokwenda kwa jina la Afro Bongo.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

Mwanamuziki wa bongofleva Harmonize ameitangaza rasmi Machi 5, mwaka wa 2022 kuwa tarehe rasmi ambayo tamasha lake ‘Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam. Kwa mujibu wake, tamasha hilo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki. Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini tanzania, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huo kwa siku tatu mfululizo. Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.

Read More
 HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

Mwanamuziki Maarufu nchini Tanzania, Harmonize ameonesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake Alikiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya kwenye tasnia ya Muziki wa Bongofleva. Kupitia ukurasa wake wa instagram, Harmonize alichapisha video fupi iliyokuwa ikicheza wimbo mpya wa Alikiba unaoitwa ‘Utu’ huku akiambatinisha na ujumbe kwamba siku ya kuvisha pete mpenzi wake lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake. “Mtu amwambie mkongwe, mfalme Ali Kiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” Harmonize aliandika. Utakumbuka juzi kati wanamuziki hao walionekana wakisafiri kwenye ndege pamoja jambo ambalo liliteka mazungumzo mtandaoni kwa muda

Read More
 MSANII WA BONGOFLEVA HARMONIZE AKANUSHA KUWA SINGLE

MSANII WA BONGOFLEVA HARMONIZE AKANUSHA KUWA SINGLE

Baada ya kuchukua headlines siku ya jana kwa kuelezea kuwa hana mpenzi mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize ameibuka kukanusha taarifa hizo ambazo zilienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram mkali huyo wa ngoma ya Teacher’ ameandika ujumbe wa kukanusha taarifa hizo ,huku akitaka kuheshimiwa akiambatanisha na emoji za kucheka, jambo ambalo limetafsiriwa kama alikuwa anatafuta kuongelewa (kiki) Januari 22 mwaka huu  Harmonize aliibuka  kupitia mfululizo wa post zake kwenye insta story yake kusema kuwa haamini kama yupo singo tena. Haikuishia hapo alienda mbali na kuandika ujumbe ambao uliohisiwa kumlenga moja kwa moja mchumba wake Briana kwa kusema tuonane nikifikisha umri wa miaka 35 labda nina umri wa miaka. Hata hivyo Harmonize walimwengu kwenye mitandao ya kijamii walihoji kuwa huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu raia wa Australia Briana limevunjika. Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Fridah Kajala.

Read More
 PENZI LA HARMONIZE NA BRIANA LAINGIWA NA UKUNGU,HARMONIZE ATANGAZA KUWA SINGLE

PENZI LA HARMONIZE NA BRIANA LAINGIWA NA UKUNGU,HARMONIZE ATANGAZA KUWA SINGLE

Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu raia wa Australia Briana limevunjika. Kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram harmonize amesema kuwa haamini kama yupo singo tena. Haikuishia hapo ameenda mbali na kuandika ujumbe ambao unahisiwakumlenga moja kwa moja mchumba wake Briana kwa kusema tuonane nikifikisha umri wa miaka 35 labda nina umri wa miaka. Hata hivyo Harmonize hajatoa maelezo zaidi kuhusu kiini cha uhusiano wake na Briana kuvunjika  ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo wa Bongofleva anatengeza  mazingira ya kumzungumziwa Afrika Mahariki kabla ya ujio wa ngoma yake mpya Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Fridah Kajala. Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’

Read More
 VIDEO YA WIMBO WA KILLY “NI WEWE” YAFUTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

VIDEO YA WIMBO WA KILLY “NI WEWE” YAFUTWA YOUTUBE KWA MADAI YA HAKIMILIKI

Video ya wimbo wa Killy ‘Ni Wewe’ ambao amemshirikisha Harmoninze imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki. Kwa sasa video hiyo haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa Mutisya Munyithya. “This video is no longer available due to a copyrighty claims by Ian Mutisya Munyithya” taarifa ya YouTube inaeleza. Mdundo wa wimbo wa ni wewe wake killy  inafanana kwa kiasi kikubwa na wa wimbo maarufu wa zamani kundi la muziki la Les Wanyika, Sina makosa. Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.

Read More
 HARMONIZE AGEUKIA FANI YA UIGIZAJI, ATANGAZA KUJA NA FILAMU

HARMONIZE AGEUKIA FANI YA UIGIZAJI, ATANGAZA KUJA NA FILAMU

Mwanamuziki na Rais wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kuingia kwenye fani ya uigizaji muda wowote kutoka sasa. Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake Women alichoshirikiana na Otile Brown ameweka wazi hilo kupitia InstaStory yake ambapo ameandika kuwa filamu hiyo kwa mara ya kwanza itaoneshwa kupitia mtandao wa Ceek. Harmonize ameandika “Nimechoka kusubiri filamu yangu ya kwanza. Itakuwa kali sana, tukutane Ceek hivi karibuni jisajili sasa” Kampuni ya Ceek ni kampuni  ambayo inajihusisha na maswala ya burudani kama kurusha matukio ya mubashara mtandaoni, kuandaa matamasha, na kutengeneza headphones.

Read More
 HARMONIZE AANZA MCHAKATO WA KUWA-FOLLOW BACK MASHABIKI ZAKE KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM

HARMONIZE AANZA MCHAKATO WA KUWA-FOLLOW BACK MASHABIKI ZAKE KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM

Baada ya mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize kuwafuta urafiki watu wote ambao alikuwa ame-wafollow katika mtandao wake wa Instagram hatimaye msanii huyo ameanza zoezi la kuwa follow back tena mashabiki na watu waliowahi kumfollow. Ukitembelea ukurasa wa Instagram wa Harmonize utagundua ameongeza idadi ya (Following) kutoka 1 mpaka 283. Utakumbuka mwishoni mwa mwaka wa 2021 mwanamuziki huyo ambaye ni Boss wa Konde Gang aliweza ku Un-follow mashabiki na watu wote walio mfollow na kumfollow mpenzi wake Briana. Kulingana na mahojiano aliyoyafanya mwishoni mwa mwaka 2021 na kipindi cha XXL’ Harmonize  alieleza kuwa aliamua kufanya hivyo ili kupata mapumziko na mpenzi wake.

Read More
 SIJAWAHI KUMTUMA MTU AWAVUNJIE WASANII WENZANGU HESHIMA, ASEMA HARMONIZE

SIJAWAHI KUMTUMA MTU AWAVUNJIE WASANII WENZANGU HESHIMA, ASEMA HARMONIZE

Msanii wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Harmonize amesema hajawai kutuma watu kuzungumza vibaya kuhusu washindani wake. Hitmaker huyo wa “Teacher” amefunguka hayo kwenye kituo kimoja cha radio ambapo ameeleza kuwa haweza kumtuma mtu yeyote kuwashambulia mahasidi wake kwa sababu hakuna kitu chochote wataongeza kwa kazi zake. “Mkiona mtu yeyote anaenda kumzungumzia mtu fulani basi ujue ni maamuzi yake na mimi binafsi siwezi kumtuma mtu yeyote kwa sababu hanisaidii.” alisema Harmonize. Ikumbukwe Harmonize ambaye alifunga mwaka kwa kuachia albamu yake ya pili, High School, hadi sasa lebo yake ina wasanii kama Ibraah, Killy, Cheed, Angella na Young Skales toka Nigeria.

Read More
 HARMONIZE AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA MKATABA WA COUNTRY BOY KUMALIZIKA KONDE MUSIC WORLDWIDE

HARMONIZE AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA MKATABA WA COUNTRY BOY KUMALIZIKA KONDE MUSIC WORLDWIDE

Siku chache baada ya Lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide kutangaza kumalizika kwa mkataba baina yao na msanii Country Boy, mmiliki wa lebol hiyo Harmonize ametoa neno. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, Harmonize amemshukuru Country Boy kwa uwepo wake ndani ya Konde Music Worldwide katika kipindi cha miaka miwili, lakini pia amemtakia kila la kheri na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano kwenye kazi zake. Uongozi wa lebo ya Konde Music Worldwide ukiongozwa na harmonize  walifanya party maalumu ya kumuaga msanii Country Boy ambaye alimaliza mkataba na lebo hiyo January 08, mwaka wa 2022. Party hiyo ilifanyika nyumbani kwa Harmonize na kuudhuriwa na Young Lunya, Harmonize, Ibraah, Meneja wa Harmonize, Choppa na wasaniii wengine kibao. Country Boy  alisainiwa Konde Music Worldwide September 11, mwaka 2020 na kuachia kazi kadha ikiwemo EP yake “The Father EP” lakini pia hits kibao kama Baby, Say, BABA na nyingine nyingi.

Read More
 PRODYUZA BONGA KUFANYA KAZI TENA NA HARMONIZE BAADA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO

PRODYUZA BONGA KUFANYA KAZI TENA NA HARMONIZE BAADA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO

Mtayarishaji wa muziki wa Bongofleva maarufu kama Prodyuza Bonga ambaye alihusika kukamilisha hit song ya ‘Never Give Up’ ya Harmonize ameeleza kufanya tena kazi na mwanamuziki huyo mmiliki wa record label ya Konde Gang baada ya kutofanya naye kazi kwa muda mrefu kufuatia kutofautiana. Mtayarishaji huyo amefunguka hayo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram akijibu moja ya maswali ya mashabiki waliotaka kujua kama atafanya kazi tena na Konde Gang, na kujibu kuwa tayari zipo kazi nyingi sana. Lakini pia kwenye post nyingine ameweka wazi kwamba atafanya kazi na Harmonize kwa makubaliano ya mkataba. Mapema mwaka jana Prodyuza Bonga alitangaza kuacha kufanya kazi na msanii huyo kwa madai ya kutolipwa na kutotimiziwa baadhi ya ahadi ikiwemo kununuliwa gari baada ya wimbo wa “Never Give Up” kufanya vizuri.

Read More
 HARMONIZE NA OTILE BROWN WAINGIA LOCATION KUTAYARISHA VIDEO YA WIMBO WAO

HARMONIZE NA OTILE BROWN WAINGIA LOCATION KUTAYARISHA VIDEO YA WIMBO WAO

Msanii wa Bongofleva Harmonize na Otile Brown wameingia location kuitayarisha video ya wimbo wao ambao unahisiwa huenda ukapatikana kwenye EP yao ya pamoja. Harmonize amethibitisha hilo kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram kwa kushare misururu ya picha wakiwa chimbo na mkali huyo kutoka Kenya jambo ambalo limewaaminisha mashabiki muziki mzuri Afrika Mashariki kuwa wawili hao wapo kwenye maandalizi ya video ya wimbo wa pamoja. Kupitia post hiyo Harmonize hajaweka wazi nini hasa wanapika na Otile Brown ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahoji huenda Otile Brown akawa mmoja wa wasanii atakaotumbuiza Disemba 31 mwaka huu kwenye listening party ya album yake ya High Schoolhuko Palm Village, Mikocheni, Dar e Salaam. Juzi kati Otile Brown alisifia uwezo wa Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza ambapo alisema msanii huyo wa Bongofleva alifanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakuwa tayari kusikia kazi hiyo Itakumbukwa Harmonize  akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.

Read More