Balenciaga waachana na Kanye West

Balenciaga waachana na Kanye West

Mtandao wa Tmz umeripoti kuwa kampuni ya mitindo na mavazi kutokea Paris, Ufaransa imeamua kuvunja ushirikiano katika uzalishaji wa mavazi kati yao na rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West. “Balenciaga haina mpango wa kuendelea na ushirikiano kati yetu na Kanye West”- Chanzo cha kuaminika kutokea Tmz Chanzo hicho hakijaweka wazi sababu ya kampuni hiyo kuachana na rapa huyo wakati wiki kadhaa zilizopita Kanye alikuwa mmoja wa washiriki katika onyesho kubwa la mavazi ya kampuni hiyo huko jijini Paris.

Read More
 Kanye West amvulia kofi Drake, amuita rapa mkali wa muda wote

Kanye West amvulia kofi Drake, amuita rapa mkali wa muda wote

Rapa Kanye West anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amempa maua yake Drake akiwa hai. Kwenye mahojiano mapya na Drink Champs, Kanye West amefunguka kwamba Drake ni rapa mkubwa na mkali zaidi kwa nyakati zote na hawezi kuomba radhi kwa kauli yake hiyo. Hata hivyo YE amekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu mbali mbali duniani wakidai kuwa rapa huyo amekosa adabu kabisa kutomtaja Kendrick Lamar, Jay Z na Lil Wayne kama The Greatest Rapper Alive. Licha ya kumwagia misifa Drake, Kanye ametema nyongo tena kwa Drizzy kwa kusema kuwa aliwahi kufanya mapenzi na Kris Jenner, Mama mzazi wa Kim Kardashian.

Read More
 Kim Kardashian ahimarisha ulinzi wa watoto wake kutokana na vitisho vya Kanye West

Kim Kardashian ahimarisha ulinzi wa watoto wake kutokana na vitisho vya Kanye West

Mwanamama Kim Kardashian ameripotiwa kuongeza pesa zaidi kwenye ulinzi lakini pia kuimarisha usalama wa watoto wake kufuatia Kanye West kuanika hadharani Jina la shule ambayo watoto wanasoma. Kanye West alijikuta akifunguka hadharani na kutaja Jina la shule hiyo kwenye mfululizo wa post zake kwenye mitandao ya kijamii wakati akipambana kuwajibu wakosoaji wake kwenye sakata la “White Lives Matter” ambalo lilishika vichwa vya habari kwa kuwakera watu weusi duniani kote.

Read More
 Kanye West afungiwa kutumia Instagram na Twitter

Kanye West afungiwa kutumia Instagram na Twitter

Rapa kutoka Marekani Kanye West amefungiwa kutumia mitandao ya kijamii ya Twitter na Instagram baada ya kutuma jumbe za chuki dhidi ya Wayahudi. Mwishoni mwa wiki, Instagram iliwekea vikwazo akaunti ya West baada ya kumshutumu rapa, mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo Sean Combs kwa kudhibitiwa na baadhi ya “Mayahudi wenye nguvu”, bila kutaja ni nani. Majukwa yote mawili yalifuta machapisho yake na kusema kuwa alikiuka kanuni ya uchochezi ukabila ubaguzi wa rangi na chuki za kidini. Matukio hayo yametokea baada ya West kuibua hasira za wanaharakati wa haki za watu weusi kwa kujitokeza katika Wiki ya Mitindo ya Paris akiwa amevalia fulana iliyoandikwa “White Lives Matter”. Katika maneno haya, waliona dhihaka ya kauli mbiu ya vuguvugu la BLM – Black Lives Matter, au “Black Lives Matter.” West, ambaye hivi karibuni alibadili jina na kijiita “Ye”, alikuwa akionyesha mkusanyiko wake wa mavazi huko Paris, ulioonyeshwa na Sela Marley, mwanamitindo mkuu na mjukuu wa Bob Marley

Read More
 KANYE WEST ATOA KAULI TATA KUHUSU KIFO CHA MALKIA ELIZABETH II

KANYE WEST ATOA KAULI TATA KUHUSU KIFO CHA MALKIA ELIZABETH II

Rapa Kanye West ameibuka na tamko lake kwa wananchi wa Jijini London baada ya siku 18 kupita kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II. Kupitia insta story kwenye akaunti yake ya Instagram, YE ameandika “London nafahamu mnavyojisikia, Nilimpoteza Malkia wangu pia.” Tamko hilo limetafsiriwa kwa maana zaidi ya moja na mashabiki mbali mbali, kuna ambao wamesema amefananisha na kifo cha Mama yake mzazi (Donda C. West) huku wengine wakidai amefananisha kifo cha Malkia na kumpoteza mkewe Kim Kardashian ambaye wameachana kwa sasa.

Read More
 KANYE WEST KWENYE HUBA ZITO NA MREMBO KUTOKA AFRIKA KUSINI

KANYE WEST KWENYE HUBA ZITO NA MREMBO KUTOKA AFRIKA KUSINI

Rapa Kanye West ameripotiwa kuwa penzini na mrembo Candice Swanepoel kutoka Afrika Kusini. Wawili hao walionekana pamoja kwenye maonesho ya New York Fashion Week wakiwa kwenye huba zito. Kwa mujibu wa TMZ, YE na Candice walionekana wakicheka na kufurahi pamoja na mchekeshaji Chris Rock huku wakipiga picha na baadaye walipanda gari moja na kuelekea hotelini. Hata hivyo mtandao wa Page Six umeripoti kwamba inaweza kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali ni kiki tu za ku-promote miwani za Yeezy ambazo mrembo huyo ni sura ya bidhaa hizo.

Read More
 KANYE WEST MBIONI KUNUNUA KAMPUNI YA VIATU

KANYE WEST MBIONI KUNUNUA KAMPUNI YA VIATU

Rapa Kanye West amesema kuwa ana mpango wa kununua Kampuni kubwa ya viatu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram YE ameuliza kuwa kama kuna kampuni yoyote kubwa ya viatu itapendezwa na ombi lake ifanye mawasiliano nae. Kanye West amesisitiza kuwa anahitaji kununua Chapa kubwa kama alivyofanya James Salter kununua kampuni ya REEBOK. Mbali na hilo rapa huyo amesema kuwa alijaribu kuzungumza na Kampuni ya JB MORGAN lakini haijawezekana kupata dili kwani wana mkataba na kampuni ya ADIDAS.

Read More
 KESI YA KANYE WEST KUMPIGA SHABIKI NGUMI YAFUTWA

KESI YA KANYE WEST KUMPIGA SHABIKI NGUMI YAFUTWA

Rapa Kanye West hatashitakiwa kwa kumpiga ngumi shabiki mmoja ambaye alikuja kwa ajili ya kutaka kupiga picha nae, mwezi Januari mwaka huu. Tukio hilo lilitokea Jijini Los Angeles ambapo shabiki huyo alidai kwamba baada ya kumuomba YE kupiga nae picha, walijikuta wakijibazana na ghafla rapa huyo alishuka kwenye gari na kumpiga ngumi mbili, moja kichwani na nyingine shingoni ambapo alianguka chini. Idara ya Polisi imechunguza shauri hilo ambalo linabeba hukumu ya miezi 6 Jela, na taarifa mpya ni kuwa wamekuta hakuna ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Kanye West.

Read More
 KANYE WEST AMTANIA PET DAVIDSON KWA KUACHANA KIM KARDASHIAN

KANYE WEST AMTANIA PET DAVIDSON KWA KUACHANA KIM KARDASHIAN

Rapa kutoka Marekani Kanye West amerejea Instagram na kumtolea uvivu Pete Davidson ambaye hivi karibuni ametajwa kuachana na Kim Kardashian. YE ameibuka na mfano wa taarifa kwenye gazeti la The New York Times ikidai Pete “Skete” Davidson kama ambavyo humtania, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 28. Hii imekuja baada ya Mtangazaji huyo na Mchekeshaji kuripotiwa kubwagana na Kim Kardashian baada ya penzi lao kudumu kwa miezi 9. YE aliingia kwenye mvutano wa mitandaoni na Pete baada ya kuingia penzini na Kim baada tu ya ndoa yao kuingia doa jeusi.

Read More
 AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

AMBER ROSE AFUNGUKA SAKATA LA KANYE WEST NA NICKI MINAJ KUPITIA WIMBO WA MONSTER

Verse ya Nicki Minaj kwenye ngoma ya Kanye West “Monster” ya mwaka 2010 ilikuwa ya moto sana ingawa YE hajawahi kufurahishwa na mauaji ya mrembo huyo kwenye ngoma hiyo. Sasa Amber Rose ambaye ndiye alimleta Nicki Minaj studio kuifanya verse hiyo, amerudi tena na kufunguka mengi kuhusu sakata hilo. Kwenye mahojiano yake na Podcast ya (Higher Learning) Amber amesema Kanye West aliwahi kumtamkia wazi kuwa, kwanini umeniletea mtu ambaye amekuja kuniua kwenye ngoma yangu? YE: “How the f*ck did you bring in a b*tch that killed me on my own song?” Amesema. Utakumbuka mwanamitindo na mwigizaji kutoka Marekani Amber Rose aliwahi kukaririwa mwaka 2018 akisema YE alibaki kidogo aifute verse hiyo.

Read More
 KANYE WEST AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA NYINGINE

KANYE WEST AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA NYINGINE

Rappa Kanye West ameingia tena kwenye headlines baada ya kushtakiwa mahakamani na kampuni ya Phantom Labs. Kanye ameshtakiwa na Phantom Labs kampuni ya uandaaji matamasha kwa madai ya kutolipa $7.1m ambayo ni malipo ya matamasha matatu. Inaelezwa licha ya kupokea barua nyingi za kukumbushwa kutoka kwa Phantom, Kanye West na timu yake wameendelea kwa njia isiyoeleweka kuinyima malipo kampuni hiyo. Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Kampuni ya “David Casavant Archive” ya kukodisha mavazi ilifungulia mashtaka mahakamani akidaiwa kukosa kurejesha mavazi aliyokodisha yenye thamani ya $400K.

Read More
 KANYE WEST KUFUNGUA DUKA LA KUSAMBAZA BIDHAA ZA YEEZY

KANYE WEST KUFUNGUA DUKA LA KUSAMBAZA BIDHAA ZA YEEZY

Imeripotiwa kuwa rappa Kanye West yupo mbioni kufungua duka lake la kusambaza bidhaa zake za “YEEZY”. Kwa mujibu wa TMZ, Kanye na timu yake ya sheria tayari wamehitimisha alama yao ya biashara ya “YZYSPLY” itakayotumika kwenye duka lake. Kanye ambaye ameanzia kutoa huduma ya usambazaji wa bidhaa zake kupitia online (tovuti), sasa hivi inatanuliwa kwa ufunguzi wa duka rasmi litakalokuwa linafanya huduma hiyo.

Read More