Video ya Khaligraph na Toxic Lyrikali Yazidisha Uvumi wa Kolabo, 

Video ya Khaligraph na Toxic Lyrikali Yazidisha Uvumi wa Kolabo, 

Rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones, amewaacha mashabiki na maswali baada ya kuonekana akizungumza na msanii Toxic Lyrikali wakati wa mazoezi ya Sol Fest. Tukio hilo lilinaswa kwenye video na kusambaa haraka mitandaoni, likichochea uvumi kuwa huenda wawili hao wanapanga kufanya kazi pamoja. Kwenye klipu hiyo, wasanii hao wanaonekana wakisalimiana nyuma ya jukwaa, jambo lililowafanya mashabiki kudhani kuwa huenda kuna mipango mipya ya muziki inayonukia. Hii inakuja licha ya kwamba Toxic Lyrikali aliwahi kukataa ombi la kolabo kutoka kwa Khaligraph hapo awali, akieleza kuwa wakati huo haukuwa sahihi. Hata hivyo, kukutana kwao ghafla katika mazoezi ya Sol Fest kumezua matumaini mapya kuwa msimamo huo huenda umebadilika. Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa yeyote kati yao, mashabiki wanaendelea kuonyesha matumaini makubwa kwamba kukutana kwao unaweza kuwa mwanzo wa kolabo inayosubiriwa kwa muda mrefu.

Read More
 Khaligraph Jones Atangaza Ujio wa Duka Kubwa la Mavazi 2026

Khaligraph Jones Atangaza Ujio wa Duka Kubwa la Mavazi 2026

Rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones, ametangaza kuingia rasmi katika ulimwengu wa fasheni kwa mpango mpya unaotarajiwa kuvutia mashabiki na wadau wa mitindo. Kupitia instastory yake, Rapa huyo amesema kuwa atazindua duka lake la mavazi na bidhaa za ubunifu mwaka 2026, hatua inayotafsiriwa kama mwanzo wa sura mpya katika safari yake ya kisanii na kibiashara. Kwa muda mrefu Khaligraph amekuwa akionekana katika mavazi ya kipekee yanayoendana na taswira yake ya uhodari na ubunifu, na sasa anaonekana kutaka kugeuza muonekano huo kuwa biashara madhubuti. Duka hilo litakuwa na mavazi ya kisasa, bidhaa za chapa yake na makusanyo yatakayoakisi mtindo wake wa kipekee unaojulikana na mashabiki wake. Wadau wa muziki na mitindo wanasema huu ni wakati mwafaka kwa rapa huyo kuchukua hatua hiyo, kwani ushawishi mkubwa mitandaoni vinaweza kulifanya jaribio hili kufanikiw­a kwa kiwango cha kimataifa.

Read More
 Khaligraph Jones Azindua Rasmi Rap Battle ya Wimbo Wake Mpya “Weyuat”

Khaligraph Jones Azindua Rasmi Rap Battle ya Wimbo Wake Mpya “Weyuat”

Msanii nguli wa muziki wa rap nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameanzisha rasmi rap battle ya wimbo wake mpya “Weyuat” baada ya kupata shinikizo kutoka kwa mashabiki wake mitandaoni. Khaligraph amesema awali hakupanga kufanya challenge hiyo, lakini mashabiki wake waliamua kuigeuza kuwa challenge rasmi. Amesema atapakia instrumental ya wimbo huo ili rappers wote wanaohisi wana uwezo waweze kuonyesha kipaji chao kupitia beat hiyo. Pia ameongeza kuwa endapo mambo yataenda vizuri, huenda wakafanya remix maalum ya wimbo huo. Rapper huyo ameahidi kutoa nafasi sawa kwa washiriki wote, akisisitiza kuwa changamoto hiyo ni jukwaa la kuibua vipaji vipya katika muziki wa rap Afrika Mashariki.

Read More
 Khaligraph Jones Adokeza Kolabo Mpya na Msanii Chipukizi Toxic Lyrikali

Khaligraph Jones Adokeza Kolabo Mpya na Msanii Chipukizi Toxic Lyrikali

Mfalme wa rap nchini Kenya, Khaligraph Jones, amedokeza uwezekano wa kufanya kolabo na msanii anayechipukia kwa kasi, Toxic Lyrikali, huku akimsifia kwa kuendelea kushikilia mizizi ya rap nchini humo. Kupitia mazungumzo yaliyowekwa wazi na mdau wa muziki Thithad3, Khaligraph ameonyesha kuvutiwa na kazi ya Toxic, akisema kuwa kwa sasa ndiye anayeshikilia uhalisia wa rap nchini humo. Ameongeza kuwa iwapo watashirikiana kwenye wimbo, itakuwa ni kwa muda muafaka bila presha wala haraka. Iwapo kolabo hiyo itatimia, itakuwa moja ya ushirikiano unaosubiriwa kwa hamu zaidi katika muziki wa hip hop wa Kenya mwaka huu. Toxic Lyrikali, ambaye amekuwa akipata umaarufu kutokana na mtindo wake wa uandishi wa mashairi makali na uhalisia wa mitaani, anaendelea kutajwa kama mmoja wa wasanii wanaochukua nafasi kubwa katika kizazi kipya cha muziki wa hip hop nchini Kenya.

Read More
 Khaligraph Jones Atoa Heshima kwa Hayati Raila Odinga kwa Kuweka Picha zake Ukutani

Khaligraph Jones Atoa Heshima kwa Hayati Raila Odinga kwa Kuweka Picha zake Ukutani

Rapper Khaligraph Jones ameonyesha heshima yake kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Raila Amolo Odinga, kwa kufichua michoro kadhaa (murals) ya kiongozi huyo zilizowekwa ndani ya jumba lake. Katika video iliyosambaa mitandaoni, Khaligraph anaonekana akitembea ndani ya nyumba yake ya kifahari, akionyesha kuta zilizopambwa kwa picha kubwa za Raila Odinga katika mitindo tofauti ya kisanaa. Msanii huyo amesema hatua hiyo ni njia yake ya kuenzi urithi na mchango wa Raila katika siasa na maendeleo ya Kenya, akimtaja kama kiongozi aliyeinua matumaini ya vizazi vingi. Mashabiki wake wengi wamepongeza hatua hiyo, wakisema ni ishara ya heshima na upendo kwa kiongozi ambaye amekuwa na athari kubwa katika historia ya taifa.

Read More
 Rapa Khaligraph Jones,Amlilia Raila Odinga Baada ya Mazishi Bondo

Rapa Khaligraph Jones,Amlilia Raila Odinga Baada ya Mazishi Bondo

Rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonyesha huzuni kubwa kufuatia mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Amolo Odinga yaliyofanyika leo nyumbani kwake eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya. Kupitia Insta stories yake, Rapa huyo amekiri kuumizwa sana na kifo cha kiongozi huyo, akisema kuwa tangu tukio hilo lifanyike amekuwa hana nguvu wala amani ya moyo. Ameongeza kuwa siku ya leo, ambayo ni ya mwisho ya kumpumzisha Odinga, inabeba uzito mkubwa kwa wale waliompenda na kumheshimu. Kwa mujibu wake, amechoka kihisia kutokana na msiba huo na ameitumia siku hii kumtakia Baba pumziko la amani kwa heshima na upendo mkubwa. Khaligraph Jones ni miongoni mwa maelfu ya Wakenya na mashabiki waliomuenzi Raila kama kiongozi mwenye maono, aliyepigania demokrasia na haki za wananchi kwa miongo kadhaa.

Read More
 Rapa Khaligraph Alia Kwa Uchungu Kufuatia Kifo cha Raila

Rapa Khaligraph Alia Kwa Uchungu Kufuatia Kifo cha Raila

Rapa wa Kenya, Khaligraph Jones, ameeleza majonzi makubwa kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga, akisema amebaki bila maneno ya kuelezea machungu anayoyapitia. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Khaligraph amekiri kuguswa sana na taarifa za kifo cha Raila, akieleza kuwa tangu jana amekuwa akihangaika kuamini kilichotokea. Rapa huyo wa ngoma ya “Ting Badi Malo”, amesema kifo hicho kimemwacha akiwa amevunjika moyo kabisa, akiongeza kuwa Raila atabaki kuwa shujaa wake wa milele.. Khaligraph, ambaye amewahi kumtaja Raila kama kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika maisha yake na kwa vijana wengi, amesema urithi wa Baba Raila utaendelea kuishi kupitia vizazi vinavyokuja.

Read More
 Khaligraph Jones Awatolea Uvivu Wakosoaji wa Mavazi Yake

Khaligraph Jones Awatolea Uvivu Wakosoaji wa Mavazi Yake

Mkali wa Rap kutoka Kenya, Khaligraph Jones, amewatolea uvivu wakosoaji wanaobeza mtindo wake wa mavazi, akisema yeye si mtu wa kuvaa kiholela kama wanavyodhani. Kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, rapa huyo ameonyesha wardrobe yake yenye mavazi ya aina mbalimbali, akibainisha kuwa kila vazi analolichagua linaendana na tukio au wakati husika. Khaligraph amesema kuwa watu wengi wanaomkosoa hawajui gharama ya mavazi anayovaa, kwani mengi ni ya thamani kubwa na yanawakilisha hadhi yake kama msanii wa kimataifa. Papa Jones ameongeza kuwa mtindo wake wa mavazi ni sehemu ya utambulisho wake katika muziki na kwamba anapenda kuonyesha ubunifu na umaridadi bila kuiga mtu yeyote.

Read More
 Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Msanii nyota wa hip hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonekana kuguswa na kauli za mtangazaji Rapcha the Sayantist, aliyemshutumu vikali kwa kudai kuwa muziki wake na maisha yake yote ni ya kuigiza. Katika kujibu lawama hizo, Khaligraph ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa mtindo wa utani, akionekana kugeuza matusi hayo kuwa fursa ya kumsaidia Rapcha kupata umaarufu zaidi. Amesisitiza kuwa kutajwa kwake ni njia rahisi ya kupata kiki, na akaenda mbali kwa kuwahimiza mashabiki wake wamfuate Rapcha mitandaoni. Pia ametoa dondoo kwamba anajiandaa kuachia freestyle mpya, hatua ambayo mashabiki wameihusisha na majibu ya muziki kwa ukosoaji aliopewa. Mashabiki mitandaoni wamegawanyika, baadhi wakiona kuwa Khaligraph ameonyesha busara kwa kutochukua mambo kwa hasira, huku wengine wakimtuhumu Rapcha kwa kutumia lugha ya matusi na kushusha heshima ya moja ya wasanii wakubwa zaidi wa hip hop Afrika Mashariki. Hayo yote yameibuka mara baada ya Rapcha kwenye moja ya Podcast kudai kuwa kila kitu kuhusu Khaligraph ni cha kubuni kuanzia lafudhi yake, madai ya kutoka Kayole, mtindo wa mavazi hadi muziki anaoutoa.

Read More
 Jaketi la Khaligraph Lapigwa Mnada kwa Dola 100

Jaketi la Khaligraph Lapigwa Mnada kwa Dola 100

Jamaa mmoja nchini Kenya ameibua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa anauza jaketi alilopewa na Rapa Khaligraph Jones, wakati wa onyesho lililofanyika Machakos. Kwa mujibu wa jamaa huyo, jaketi hilo ni zawadi ya moja kwa moja kutoka kwa Papa Jones. Hata hivyo, amesema sasa amelazimika kuliuza kwa bei ya dola 100 (takribani KSh 13,000) akieleza kuwa ana mahitaji ya kifedha. Taarifa hiyo imezua maoni tofauti mitandaoni. Baadhi ya mashabiki wameshangazwa na uamuzi wa kuuza zawadi ya msanii mkubwa kama Khaligraph, huku wengine wakisisitiza kuwa mara tu zawadi inapotolewa, mwenye kupokea ana uhuru wa kuamua atalifanyia nini. Mpaka sasa, Khaligraph Jones hajaweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo, na kuacha mashabiki wakijiuliza kama kweli jaketi hilo ni la ukweli au ni mbinu ya kutafuta kiki.

Read More
 Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonyesha ubunifu na ujasiri kwa kugeuza kejeli alizopokea kutoka kwa rapa Octopizzo kuwa fursa ya biashara. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Khaligraph alizindua Limited Edition OG Omollo Custom Sweatpants, hatua iliyowaacha mashabiki wake wakimpongeza kwa uamuzi wa kipekee. Khaligraph ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Confuse” amehitimisha ujumbe wake kwa kutumia hashtag maarufu #respecttheogs, ishara ya kuendeleza msimamo wake wa kudumisha heshima na ushawishi katika anga ya muziki wa rap nchini humo. Uamuzi huo ulionekana kama jibu la moja kwa moja kwa kejeli kutoka kwa rapa mwenzake, Octopizzo, ambaye alinukuliwa akisema “Kuna rapper flani huvaa sweatpants from January to December na timber ya yellow.” Badala ya kuchukua maneno hayo kwa njia hasi, Khaligraph aliuchukua mtindo huo na kuubadilisha kuwa bidhaa ya kibiashara, hatua iliyotafsiriwa na mashabiki kama “clap back” ya kishujaa. Mashabiki wengi walimsifu kwa ubunifu huo, wakisema ni mfano bora wa jinsi msanii anaweza kutumia ukosoaji kujinufaisha.

Read More
 Khaligraph Jones Atamani Kununua Tena Subaru Yake ya Zamani

Khaligraph Jones Atamani Kununua Tena Subaru Yake ya Zamani

Rapa Khaligraph Jones, ametangaza kuwa anatamani kununua tena gari lake la zamani aina ya Subaru Forester ambalo liliwahi kuwa sehemu ya maisha yake kabla ya kupata umaarufu mkubwa. Khaligraph ameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa anataka kulipata tena Subaru hilo, akiwataka mashabiki wanaofahamu lilipo kumjulisha. Hatua hiyo imezua hisia tofauti mitandaoni, wengi wakikumbuka jinsi gari hilo lilivyokuwa sehemu ya safari yake ya muziki kabla ya kupata mafanikio makubwa Tangazo hili linakuja wiki chache baada ya rapa wa Marekani, Rick Ross, kusema bado anamiliki BMW iliyotumika kwenye video ya wimbo wake maarufu Hustlin’ zaidi ya miaka 15 iliyopita. Wadadisi wa muziki wanasema hatua ya Khaligraph huenda ni jaribio la kuonyesha kuthamini safari yake ya muziki na mafanikio aliyopata tangu siku za mwanzo.

Read More