Rapper Khaligraph Jones ameonyesha heshima yake kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Raila Amolo Odinga, kwa kufichua michoro kadhaa (murals) ya kiongozi huyo zilizowekwa ndani ya jumba lake.
Katika video iliyosambaa mitandaoni, Khaligraph anaonekana akitembea ndani ya nyumba yake ya kifahari, akionyesha kuta zilizopambwa kwa picha kubwa za Raila Odinga katika mitindo tofauti ya kisanaa.
Msanii huyo amesema hatua hiyo ni njia yake ya kuenzi urithi na mchango wa Raila katika siasa na maendeleo ya Kenya, akimtaja kama kiongozi aliyeinua matumaini ya vizazi vingi.
Mashabiki wake wengi wamepongeza hatua hiyo, wakisema ni ishara ya heshima na upendo kwa kiongozi ambaye amekuwa na athari kubwa katika historia ya taifa.