Khaligraph Jones Afichua Kupunguza Kilo 22 Kwa Miezi Mitatu Kupitia Mazoezi na Kula kwa Mpangilio

Khaligraph Jones Afichua Kupunguza Kilo 22 Kwa Miezi Mitatu Kupitia Mazoezi na Kula kwa Mpangilio

Rapa maarufu wa Kenya, Khaligraph Jones, amefichua safari yake ya kupunguza uzito, akisema kuwa ameweza kupunguza kilo 22 ndani ya miezi mitatu pekee. Akiweka wazi safari yake ya afya kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Khaligraph  alieleza kuwa awali alikuwa na uzito wa 137 kg, lakini sasa ana uzito wa 115 kg, hatua aliyofikia kwa kutumia mbinu ya intermittent fasting (kula kwa mpangilio wa muda) pamoja na mazoezi ya mwili. “Nilikua nakula ngwashe, maji na apple,” alisema rapa huyo, akionyesha kuwa mlo wake ulikuwa mwepesi lakini wenye afya. Katika mahojiano, Khaligraph pia alimpongeza mwanamitandao maarufu nchini Pritty Vishy kwa jitihada zake za kupunguza uzito, akisema kuwa alihamasishwa na kujitolea kwake, hasa alipokuwa akifanya mazoezi pamoja na mkewe. “Vishy alikua anajitahidi sana. Ilikua motisha pia kwangu,” alisema. Aidha, Khaligraph amepuuzilia mbali madai yanayosambaa mtandaoni kuwa Pritty Vishy hutumia dawa kupunguza mwili wake. Alisisitiza kuwa madai hayo hayana msingi na kwamba mafanikio ya Vishy yanatokana na bidii na nidhamu ya hali ya juu. Mashabiki wengi wamepongeza uamuzi wa Khaligraph wa kuchukua hatua za kuboresha afya yake na kuonyesha mfano kwa wengine kuwa inawezekana kupunguza uzito kwa njia salama na za asili.

Read More
 Khaligraph Jones kuzuru Australia mwishoni mwa mwezi huu

Khaligraph Jones kuzuru Australia mwishoni mwa mwezi huu

Siku chache baada ya kufanya shoo yake nchini Sierra Leone, Rapa Khaligraph Jones ametangaza show nyingine ya kimataifa nchini Australia mwishoni mwa mwezi huu. Kupitia mitandao yake ya kijamii amesema anatarajia kufanya show zake kwenye miji ya Perth na Sydney, Januari 27 na 29 mtawalia. “Whats good Australia, OG is coming through, January Friday 27th Perth and Sunday 29th Sydney,” Aliandika. Khaligraph alitumbuiza mjini Free Town, Sierra Leone juzi kati ambapo aliwapa mashabiki zake burudani ya kufa mtu kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri kipindi cha nyuma. Rapa huyo ameanza kufanya shows zake za kimtaifa baada ya kuachia wimbo wa “Avengers Cypher” ambao alimshirikisha rapa anayekuja kwa kasi nchini Katapilla, wimbo ambao unafanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube.

Read More
 Khaligraph Jones aongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari

Khaligraph Jones aongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari

Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones ameongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari siku chache baada kurejea nchini akitokea Sierra Leone. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti video akiwa kwenye harakati ya kuosha ndinga yake mpya aina ya Lexus LX 570 huku akisindikiza na ujumbe unaosomeka “feels good to be back home” Gari hiyo ya kifahari yenye thamani ya shilling million 12 za Kenya ni ya tano kuingia kwenye mikono ya Khaligraph Jones ikizingatiwa kuwa ana magari aina ya Subaru, Chrysler, Toyota Crown na Range Rover. Ikumbukwe juzi kati Khaligraph Jones amekuwa nchini Sierra Leone ambako alienda kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ambapo alipata fursa ya kuwapa mashabiki zake burudani ya kipekee kupitia nyimbo zake tofauti.

Read More
 Rapa Khaligraph Jones akerwa na abiria wanaotumia vyoo vya ndege kwenda haja kubwa

Rapa Khaligraph Jones akerwa na abiria wanaotumia vyoo vya ndege kwenda haja kubwa

Rapper Khaligraph Jones amesikitishwa na watu wanaopenda kujisaidia ndani ya vyoo vya ndege wakati wa safari za ndani ya nchi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Papa Jones amesema sio jambo la busara kwa watu kwenda haja kubwa kwenye vyoo vya ndege kwa kuwa inaharibia hali ya hewa. Hitmaker huyo “Kamnyweso” ameshauri watu wajenge tamaduni za kuvumilia wakati wa safari za ndani hadi ndege itakapotua kwa kuwa jambo hilo linakera mno. Hata hivyo amedai ndege ambayo alikuwa ameabiri ilikuwa inanuka kinyesi cha mtu baada ya abiria mmoja kutumia vyoo vya ndani. “Nashangaa sana na watu wanaenda kwa choo ya ndege kukunia na saa hizo ni a 40-minute flight. Shikilia hiyo kitu mpaka tuland bwana, ndege imenuka pupu leo,” Aliandika Instagram.

Read More
 Rapa Khaligraph Jones afunguka mpango wa kuanza kufanya muziki wa Injili

Rapa Khaligraph Jones afunguka mpango wa kuanza kufanya muziki wa Injili

Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones amefunguka mpango wa kuachana muziki wa Hiphop na kuanza kuimba muziki wa injili. Kwenye mahojiano na Plug tv Khaligraph amesema kwamba amekuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili toka utotoni, hivyo anasubiri muda mwafaka kufika ili aweze kueneza injili kupitia muziki wake kwani hata kabla ya kuanza kufanya muziki wa kidunia alikuwa msanii wa nyimbo za injili. Mbali na hayo Boss huyo wa Blue Ink ameweka wazi sababu za kutocheza kimahaba na wanawake akiwa anatoa burudani jukwaani kama namna wasanii wengine wamekuwa wakifanya. Papa Jones amesema brand au chapa yake ya muziki haimruhusu kufanya vitu kama hivyo ikizingatiwa pia ana familia.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AANDIKA BARUA YA WAZI KWA RUTO KUPITIA WIMBO

KHALIGRAPH JONES AANDIKA BARUA YA WAZI KWA RUTO KUPITIA WIMBO

Rapper Brian Omollo maarufu kama Khaligraph Jones, amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kumuandikia barua ya wazi rais mteule william ruto kupitia singo yake mpya iitwayo “Usiache Akemewe Free style” Kupitia wimbo huo rapa huyo ametoa wito kwa Ruto kuweka kipau mbele suala la kuwaleta wakenya pamoja pindi atakapoapishwa rasmi kuitumikia Kenya kwa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wakenya. Khaligraph Jones ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna baadhi ya watu wanamshambulia kiongozi wa Azimio Raila Odinga bila kujua kwamba matusi yao inamkosesha amani huku akisema kuwa anafahamu kuwa Ruto ambaye ni mcha mungu ana uwezo wa kumaliza uhasama wa kisiasa unaoshuhudia kwa sasa nchini. Papa Jones amefichua kuwa mama yake amekuwa mgonjwa tangu Raila apoteze uchaguzi uliokamilika lakini Ruto akimpa heshima kiongozi huyo mama yake pamoja na wafuasi wengine wa azimio wanaopitia wakati mgumu mioyoni mwao watafarijika. Hata hivyo amemalizia wimbo huo wa dakika 2 sekunde 6 kwa kumpongeza Rais Mteule William Ruto kwa mara nyingine huku akimshukuru kwa kumsikiliza.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA SABABU ZA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA GOSPEL

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA SABABU ZA KUTOFANYA KAZI NA WASANII WA GOSPEL

Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones amefunguka sababu ya kutofanya kazi na wasanii wa nyimbo za injili. Katika mahojiano na Mzazi Willy M. Tuza kwenye Mambo Mseto Khaligraph Jones amesema licha ya kuomba kufanya kazi ya pamoja na baadhi ya wasanii wa nyimbo za injili nchini wengi wao wamedinda kushirikiana naye kimuziki kwa hofu ya kukosolewa na mashabiki. Khalighraph Jones ametoa kauli yake hiyo mara baada ya kuulizwa uhusiano wake na wasanii wa nyimbo za injili ukoje ikizingatiwa kuwa ana wimbo wa injili uitwao “Sifu Bwana” ambao amemshirikisha Nyashinski.

Read More
 KHALIGRAPH JONES ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WAKENYA KUKUZA BRAND ZAO

KHALIGRAPH JONES ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WAKENYA KUKUZA BRAND ZAO

Rapper Khaligraph Jones amesema muziki wa Kenya ulipofika ni wakati wasanii kujitambua na kwendana na nyakati zilizopo kuanzia kazi zao hadi muonekano kwa watu. Akizungumza na Presenter Ali hitmaker huyo wa “Mbona” amesema muonekana wa msanii mbele ya mashabiki wake una nafasi katika kuuza muziki wake anaofanya. Khaligraph Jones amesema kuwa msanii si kuandika nyimbo tu na kuingia studio kurekodi bali hata muonekano wake ni kitu cha kuzingatia. Hata hivyo ameongeza kuwa muuoneka wake ndio kila kitu kwenye muziki wake japokuwa muda mwingine inakuwa tabu kwake kwa kuwa baadhi ya mashabiki wake hufikiri ana fedha nyingi kitu ambacho si kweli

Read More
 MISS CASHY KUMBURUZA MAHAKAMINI KHALIGRAPH JONES KWA KUKWEPA KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAKE

MISS CASHY KUMBURUZA MAHAKAMINI KHALIGRAPH JONES KWA KUKWEPA KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAKE

Mama mtoto wa Khaligraph Jones, Cashy Karimi amefichua kuwa ana mpango kumshtaki rapa huyo baada ya kukataa kutoa matunzo kwa mtoto wao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cashy amechapisha picha yake akiwa katika Mahakama ya Milimani na kuandika caption inayosomeka, “Ukiitwa unaitika uilvyo, ukiwa mbali njoo na champali. Ujasiri hutoka kwa Mungu, mwamuzi halisi na mlinzi wa haki. Mungu wa milimani na mabondeni, tangulia mbele yetu.” Ujumbe huo umetafsiriwa na ulimwengu kuwa huenda mrembo huyo amemfungulia mashtaka khaligraph jones kwa hatua ya kukwepa kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wake. Wawili hao wana mtoto wa kiume pamoja,aitwaye Xolani lakini Cashy amekuwa akishikilia kuwa Khaligraph amekuwa akimtelekeza mtoto wake, huku akiwahudumu watoto wake wengine. Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo wamemhimiza Cashy kuendelea na hatua ya kumpigania motto hadi pale khalighraph jones atakaporidhia suala la kutoa matunzo kwa mtoto wao. “Wewe peke yako ndiye unayejua unapitia nini, usiwasikilize watu hawatakuwekea chakula, mvulana anahitaji mambo mengi pigana naye” “Pigana kwa ajili ya mtoto wako wakati wote … Yule yule anayekuambia usishtaki mwanamume au kumburuza mahakamani hatamlisha mwanao” “Usijaribu kupata watoto wakati huwezi kuwatunza …

Read More
 KHALIGRAPH JONES AWAPA SOMO WASANII WANAOISHI MAISHA YA KUIGIZA

KHALIGRAPH JONES AWAPA SOMO WASANII WANAOISHI MAISHA YA KUIGIZA

Rapa Khaligraph Jones amewachana baadhi ya wasanii wanaoishi maisha ya kuigiza yasiyokuwa na uhalisia. Katika mahojiano yake na 2mbili Papa Jones amesema ni wakati wa mastaa na watu wenye majina makubwa kuacha kuishi maisha feki katika mitandao ya kijamii na badals yake wabuni vitu vya maendeleo kuliko kujionesha mitandaoni kuwa maisha yao ni bomba ilhali wanaishi kwa madeni Aidha ameweka wazi kwamba mastaa wengi hujisukuma sana kuishi katika nyumba za kifahari na kumiliki magari makubwa kutokana na presha za mashabiki jambo ambalo amesema sio sawa kwa kuwa wanajidanganya wenyewe. Khaligraph Jones  ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wameonekana kutoogopa kukubali hali zao za kimaisha licha ya  shinikizo kutoka kwa mashabiki.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AWAPA SOMO WASANII WA GENGETONE

KHALIGRAPH JONES AWAPA SOMO WASANII WA GENGETONE

Rapa Khaligraph Jones ametoa changamoto kwa wasanii wa muziki wa Gengetone waache kulalamika juu ya kukosa usimamizi. Rapa huyo amewataka wasanii hao, kutotumia silaha ya kukosa uongozi kama chanzo cha wao kushindwa kufanya muziki na badala yake wajifunze kutoa kazi zao wenyewe bila kutegemea lebo za muziki ambazo muda mwingine huwapoteza kimuziki. Katika hatua nyingine, ameamua kuweka wazi kuhusu taarifa za muda mrefu zilizosambaa kuwa hana maelewano mazuri na rapa mwenzake Octopizo. Papa Jones amesema hana ugomvi au mkwaruzano wowote na rapa huyo kwani watu ndio wamekuwa wakiwaingiza kwenye matatizo.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AWAPA WANASIASA RUHUSA YA KUTUMIA NYIMBO ZAKE

KHALIGRAPH JONES AWAPA WANASIASA RUHUSA YA KUTUMIA NYIMBO ZAKE

Rapa Khaligraph Jones amewapa wanasiasa ruhusa ya kucheza nyimbo zake bila malipo kwenye shughuli zao za kisiasa. Katika mahojiano na Ramogi Tv Mkali huyo wa ngoma ya ‘Mazishi’ amesema hatamfungulia mtu yeyote kesi mahakamani kwa kutumia kazi zake za muziki bila idhini yake. “Cheza tu muziki wangu unapoweza, sitampeleka mtu yeyote mahakamani kwa hilo,” alisema. Kauli yake imekuja siku chache baada ya Sauti Sol kutishia kuuchukulia muungano wa Azimio hatua kali za kisheria kwa kucheza muziki wao bila kibali. Sauti Sol, kupitia taarifa walidai kulipwa fidia, ambapo tuliona member wa kundi hilo Bien akisema kuwa wanatarajia kulipwa pesa nyingi. Hata hivyo, sio wanachama wote wa Sauti Sol walikuwa wanaunga mkono hatua hiyo, kwani Savara alijitokeza wazi na kudai  kuwa hana shida yeyote kwa nyimbo zake zikichezwa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Read More