KHALIGRAPH JONES ALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA YA MAISHA

KHALIGRAPH JONES ALALAMIKIA KUPANDA KWA GHARAMA YA MAISHA

Rapa Khaligraph Jones ameonekana kulemewa na shughuli za ujenzi wa nyumba yake ya kifahari. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Papa Jones amelalamika kupanda kwa gharama ya vifaa vya ujenzi nchini huku akitoa wito kwa serikali kuingia kati na kushusha bei ya vifaa hivyo kama njia moja ya kuwasaidia wakenya wa kawaida kukamilisha miradi yao. “Sirkali Saidia, Bei Ya Chuma ya Kujenga imepanda kuliko Iphone 13 pro Max, Sikuizi Kwa nyumba Beef tunakula once a week, kama leo Usiku ni Ugali na mboga tu. #respecttheogs“, Ameandika kupitia Instastory yake. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kumtolea uvivu rapa huyo kwa kuwakejeli wakenya ambao wanaishi maisha ya uchochole kwa kujaribu kuonesha namna ambavyo analamimikia vitu vya starehe. Utakumbuka juzi kati Khaligraph Jones alishare kupitia Instagram yake maendeleo ya mjengo wake wa kifahari ambao amekuwa akiujenga.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AHIRISHA KUACHIWA KWA VIDEO YA MAOMBI YA MAMA KISA MSIBA WA MWAI KIBAKI

KHALIGRAPH JONES AHIRISHA KUACHIWA KWA VIDEO YA MAOMBI YA MAMA KISA MSIBA WA MWAI KIBAKI

Rapa Khaligraph Jones ameahirisha kuachia video ya wimbo wake uliokuwa ukisubiriwana mashabiki uitwao ‘Maombi ya Mama’ kwa ajili ya kumuenzi Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki aliyefariki mwishoni mwa juma lilopitwa. Kupitia ukurasa wake wa instagram bosi huyo wa Blue Ink, amesema video hiyo ilipaswa kuachia rasmi wiki lakini italazimika kusubiri hadi marehemu rais mwai kibaki atakapozikwa. Maombi ya Mama ni wimbo namba 7 kutoka kwenye albamu yake Invisible Currency na ni wimbo ambao amemshirikisha msanii wa kike nchini Adasa. Wengine walioshirikishwa kwenye Albamu ya Khaligraph Jones ni pamoja na; Alikiba, Prince Indah, Mejja, Blackway, Rudeboy, Kev the Topic, Scar, Xenia Manasseh, na Dax. Album ya “Invisible Currency” iliachiwa rasmi Machi 7 mwaka 2022 ikiwa na jumla ya ngoma 17 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  Khaligraph Jones  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Testimony 1990 iliyotoka mwaka 2018.

Read More
 ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAFIKISHA STREAMS ZAIDI YA MILIONI 2 BOOMPLAY

ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAFIKISHA STREAMS ZAIDI YA MILIONI 2 BOOMPLAY

Rapa Khaligraph Jones anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Album yake ” Invisible Currency ” ambayo tayari ina takriban wiki tatu tangu itoke rasmi. Goods ni kwamba Album ya “Invisible Currency” imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams millioni 2 kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya. Album ya “Invisible Currency” iliachiwa rasmi Machi 7 mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  Khaligraph Jones  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Testimony 1990 iliyotoka mwaka 2018.

Read More
 INVISIBLE CURRENCY ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

INVISIBLE CURRENCY ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

Rapa Khaligraph Jones anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Album yake ” Invisible Currency ” ambayo tayari ina takriban wiki moja tangu itoke rasmi. Goods ni kwamba Album ya “Invisible Currency” imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams million moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya. Kupitia Instagram page yake Papa Jones amewashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia album yake ya Invisible Currency huku akiwataka waendelea kuisikiliza album hiyo kwenye mtandao wa Boomplay Kenya. Album ya “Invisible Currency” iliachiwa rasmi Machi 7 mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  Khaligraph Jones  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Testimony 1990 iliyotoka mwaka 2019

Read More
 KHALIGRAPH JONES AMPA SCAR MKADINALI MAUA YAKE AKIWA HAI, AMUITA MWAANDISHI BORA KWA WASANII WA HIPHOP KENYA

KHALIGRAPH JONES AMPA SCAR MKADINALI MAUA YAKE AKIWA HAI, AMUITA MWAANDISHI BORA KWA WASANII WA HIPHOP KENYA

Mkali wa muziki wa hiphop nchini Khaligraph Jones amehamua kumpa Scar Mkadinali maua yake akiwa hai, kwa kumtaja kama mwaandishi bora wa nyimbo kwa upande wa wasanii wa hiphop nchini Kenya. Akizungumza kwenye listening party ya album yake mpya Papa Jones amesema Scar anastahili kupewa heshimu hiyo kwa sababu anaitendea haki kiwanda cha muziki nchini. Hitmaker huyo wa ngoma ya Hiroshima amesema anafurahia mafanikio ambayo wasanii wa kundi la Wakadinali wamepata kwenye muziki wao ambapo am meenda mbali zaidi na kusema kwamba anashangazwa na watu wanaomshindanisha na wasanii wa kundi hilo ikizingatiwa kuwa yeye ndiye aliwakutanisha na prodyuza Big Beats mwaka wa 2012, kipindi ambacho walikuwa wanachipukia kwenye game ya muziki wa Hiphop nchini Kenya. Sanjari na hilo Khaligraph Jones amemtaja Msanii Mejja kama moja kati ya wasanii wakarimu aliowahi kutana na kufanya kazi nao. Kwa sasa Khaligraph Jones anafanya vizuri na Album yake ya Ngoma 17 za Moto ya “Invisible Currency” ambayo inapatikana Exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay Kenya.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI ALAMA ALIYOPATA KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE

KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI ALAMA ALIYOPATA KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE

Rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake ya Elimu kwani ameamua kuweka wazi alama ambayo alipata kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne K.C.S.E. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Papa Jones amesema alipata alama ya D+ katika mtihani wake wa kitaifa baada ya kuacha shule kwa miaka mitatu kutokana na matatizo ya kulipa karo. Hitmaker huyo wa ngoma ya Hiroshima amesema alihamua  kurudi shule ili awe mfano mwema kwa ndugu zake kwani alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto sita kumaliza kidato cha nne. Hata hivyo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii wamempongeza rapa Khaligraph Jones kwa hatua ya kuweka wazi alama aliyopata kwenye mtihani wake wa kitaifa wakisema kuwa itawapa moyo vijana wengi waliokata tamaa maishani baada ya kufeli kwenye masomo yao.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

Rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones ametaja vigezo anavyotumia kumchagua msanii wa kufanya nae na kolabo. Katika mahojiano yake hivi karibuni Papa jones amesema yeye huwa angalii ukubwa wa msanii wala idadi ya wafuasi alionao kwenye majukwaa ya kustream muziki mtandaoni bali uzingatia sana ubunifu na kipaji cha msanii husika anapotaka kufanya kolabo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Champez” amesema hata wasanii aliowashiriki kwenye album yake ya “Invisible Currency” ni watu ambao wana ukaribu nae na hivyo angemshirisha msanii ambaye hana uhusiano mzuri nae kwenye album yake hiyo. Utakumbuka kwa sasa Khaligraph jones anafanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni kupitia Invisible Currency album ambayo inazaidi ya streams laki 5 kwenye mtandao wa Boomplay Kenya tangu iingie sokoni machi 17 mwaka huu.

Read More
 RAPA KHALIGRAPH JONES AACHIA RASMI “INVISIBLE CURRENCY” ALBUM

RAPA KHALIGRAPH JONES AACHIA RASMI “INVISIBLE CURRENCY” ALBUM

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones ameachia rasmi albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Invisible Currency ina ina jumla ya nyimbo 17 za moto huku ikiwa na collabo 10 pekee kutoka kwa wakali kama Ali kiba, Juma Jux, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi. Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ametoa shukran kwa watu wote waliofanikisha mchakato wa kuiandaa album yake mpya ambapo amewataka mashabiki zake kuifutilia album ya Invisible Currency kwenye mtandao wa kustream muziki wa Boomplay Kenya. Invisible Currency inakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones  baada ya “Testimony 1990” ya  mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.

Read More
 KHALIGRAPH JONES ALAANI KITENDO CHA WAHUDUMU WA BODABODA KUMDHULUMU MWANAMKE MMOJA JIJINI NAIROBI

KHALIGRAPH JONES ALAANI KITENDO CHA WAHUDUMU WA BODABODA KUMDHULUMU MWANAMKE MMOJA JIJINI NAIROBI

Rapa kutoka kenya Khaligraph Jones ameungana na Wakenya wengine kwenye mitandao ya kijamii kulaani kitendo cha wahudumu wa Boda Boda jijini Nairobi kumdhalilisha kijinsia mwanamke mmoja mara baada ya kudaiwa kumgonga kwa gari mhudumu mwenzao Machi 7 mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ameonekana kutofurahishwa na kitendo cha wanabodaboda hao kumpakata mwanamke huyo hadi kumvua nguo ambapo amehapa kuwa mstari wa mbele kushinikiza vyombo vya usalama nchini iwape kifungo cha maisha waliohusika kutekeleza kitendo hicho cha kikatili. Hata hivyo Mastaa mbali na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameonekana kumuunga mkono rapa huyo huku wakitaka maafisa wa polisi kuhakikisha waliohusika wote wanatiwa baroni na kufunguliwa mashtaka mahakamani Kauli ya Khaligraph Jones imekuja mara baada ya idara ya usalama kutoa taarifa kuwa takriban washukiwa 16 waliomdhalalisha mwanamke huyo wamekamatwa huku msako ukiendelea kuwasaka washukiwa wengine waliotekeleza kitendo hicho.

Read More
 ALBAMU MPYA KUTOKA KWA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MACHI 7

ALBAMU MPYA KUTOKA KWA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MACHI 7

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones yupo tayari kuiboresha playlist yako hivi karibuni, kwa mujibu wa Papa Jones anasema albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” itatoka rasmi mwezi huu wa Machi. Khalighraph Jones ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo itaingia sokoni Machi 7 mwaka wa 2022. Tayari Papa Jones tayari ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya ambayo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee. Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Ali kiba, Juma Jux, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi. Invisible Currency itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones  baada ya “Testimony 1990” ya  mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17

Read More
 KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

Rapa Khaligraph Jones ameungana na wapenzi wa muziki wa hiphop Barani Afrika kumuomboleza kifo cha rapa riky Rick ambaye alifariki februari 23 mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ameshare screen shot ya mazungumzo ya siri kati yake na rapa huyo ambapo amesema kuwa mwaka wa 2018 alikuwa na matamanio ya kufanya kazi ya pamoja na riky rick lakini hakufanikisha suala hilo kutokana na ugumu wa kumfikia. Kwa upande wake Rapa King Kaka amesema walikutana na Riky Rick miaka kadhaa iliyopita nchini ufaransa kwenye moja ya party ambapo alipata wasaa mzuri kubadilishana mawazo na rapa huyo ambaye kwa mujibu wake alikuwa mtu mkarimu zaidi kuwahi kukutana naye. Riky Rick alifariki dunia februari 23 mwaka huu baada ya kujitoa uhai nyumbani kwake kaskazini mwa Joburg Jumatano asubuhi. Chanzo cha Kifo chake hakijatajwa lakini baadhi ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vinaripoti kwamba Riky Rick alijinyonga baada ya kusumbuliwa na msongo wa mawazo. Rapa huyo alianza kujipatia umaarufu mwaka 2015 kupitia ngoma yake iitwayo, Boss Zonke.

Read More
 MISS CASHY AKATA TAMAA KUMSHINIKIZA RAPA KHALIGRAPH JONES KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAO

MISS CASHY AKATA TAMAA KUMSHINIKIZA RAPA KHALIGRAPH JONES KUTOA MATUNZO KWA MTOTO WAO

Female Rapper kutoka Kenya Miss Cashy amedai kuwa licha ya vipimo vya DNA kubaini kuwa rapa Khaligraph Jones ndiye baba wa mtoto wake rap huyo amekataa kutoa matunzo kwa mtoto wake huyo. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni amesema mwaka wa 2021 alifanya vipimo vya DNA baada ya rapa huyo kumshinikiza afanye hivyo ambapo amedai kuwa amelazimika kuhama nairobi kwa ajili ya kumshughulikia mtoto wake huyo. Mrembo huyo amesema hataki tena kuzungumzia suala la Papa Jones kukimbia majukumu ya kumlea mtoto wake kwani amechoka kuonekana anatafuta uhuruma kwa mashabiki wa rapa huyo. Ikumbukwe Miss Cashy amekuwa akimshinikiza Khaligraph Jones  ajukumikie mahitaji ya msingi ya mtoto wao ila rapa huyo amekuwa kimya juu ya swala hilo na hata kukwepa maswali ya waandishi wa habari anapokuwa kwenye mahojiano mbali mbali.

Read More