Mike Sonko Amkingia Kifua Binti yake Baada ya Kudhalalishwa na Mume Wake
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, ameingilia kati na kumkingia kifua binti yake, Salma, baada ya madai kuibuka kwamba ameshushiwa kipigo cha mbwa na mume wake. Tukio hilo limeibuka baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha Sonko akimkabili mkwewe mara baada ya kupokea simu ya dharura kutoka kwa binti yake. Sonko anasema sauti ya Salma ilikuwa imejaa hofu na maumivu, jambo lililomsukuma kukimbia mara moja kwenda kumsaidia kama mzazi. Katika ujumbe wake, Sonko amelaani vikali vitendo vya ukatili wa majumbani, akisema hakuna mwanamke au mwanaume anayestahili kuishi kwenye mazingira ya vurugu. Amehimiza wanandoa kuchagua mazungumzo na njia za amani kutatua changamoto zao, badala ya hasira zinazoweza kusababisha madhara. Tukio hilo limezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku Wakenya wakitoa maoni mbalimbali na wengine wakitaka hatua zichukuliwe kulinda waathiriwa wa ukatili wa majumbani.
Read More