Ligi Kuu Saudi Yakanusha Ushawishi wa Ronaldo Kwenye Maamuzi ya Vilabu
Wasimamizi wa Ligi Kuu ya soka ya Saudi Arabia imeonya kuwa hakuna mtu yeyote, hata awe na ushawishi kiasi gani, anayeweza kutoa maamuzi nje ya kilabu chake mwenyewe, huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya Cristiano Ronaldo katika kilabu cha Al-Nassr. Mshambulizi huyo wa Ureno aliachwa nje ya kikosi cha Al-Nassr katika mechi ya Jumatatu iliyopita dhidi ya Al-Riyadh, huku vyombo vya habari vya Ureno vikidai kuwa alikataa kucheza kwa sababu ya kutoridhishwa na jinsi Kampunizi ya uwekezaji wa PIF inavyoendesha kilabu hicho ikilinganishwa na wapinzani wao. Inaripotiwa kuwa Ronaldo amekasirishwa na kitendo cha mchezaji Karim Benzema kuhamia kilabu cha Al-Hilal, kutoka Al-Ittihad, ambapo mshambulizi huyo wa Ufaransa alicheza mechi yake ya kwanza kwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Al-Okhdood. Vilabi vyote viwili Al-Nassr na Al-Hilal, zinadhaminiwa na PIF, ambayo pia inafadhili kilabu cha Newcastle United cha Uingereza.
Read More