Sammy Kioko Ashukuru Wakenya kwa Kumsaidia Kifedha
Mchekeshaji wa Kenya, Sammy Kioko, ametoa shukrani za dhati kwa Wakenya na mtangazaji Oga Obinna kwa kusimama naye wakati alipokuwa akikabiliwa na changamoto kubwa za kifedha. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kioko ameandika ujumbe wa shukrani akisema amepata faraja kwa ukarimu na upendo aliooneshwa na marafiki pamoja na mashabiki wake, hasa Oga Obinna. Amesema misaada waliyotoa imeleta mabadiliko makubwa katika maisha yake, na sasa madeni ya kodi ya nyumba yamelipwa yote huku akibakiwa na kiasi kidogo cha kujikimu. Mchekeshaji huyo aliyekuwa akisusua kiuchumi, amesema hatua hiyo imempa faraja kubwa na kumtia moyo kuendelea kupambana, akiwataka mashabiki waendelee kumuombea na kumsaidia kimawazo. Shukrani hizo zinakuja wiki chache baada ya Kioko kuilaumu Serikali ya Kaunti ya Machakos kwa kushindwa kumlipa deni la shilingi milioni 19, jambo lililomwacha katika hali ngumu kifedha na kuathiri miradi yake ya ubunifu.
Read More