Entertainment

Mike Sonko Aahidi Kumsaidia  Mchekeshaji Sammy Kioko  Kupata Deni la Milioni 19

Mike Sonko Aahidi Kumsaidia  Mchekeshaji Sammy Kioko  Kupata Deni la Milioni 19

Mchekeshaji kutoka Kenya Sammy Kioko amezua hisia mitandaoni baada ya kuangua kilio hewani katika kipindi cha Obinna Show, akifichua kuwa serikali ya kaunti ya Machakos imeshindwa kumlipa deni la takriban shilingi milioni 19 alizofanyia kazi.

Kioko ameeleza kuwa kucheleweshwa kwa malipo hayo kumemweka kwenye hali ngumu kifedha, kiasi cha kushindwa kufadhili miradi yake na kumsaidia mshirika wake wa kibiashara ambaye kwa sasa anahitaji matibabu nchini India.

Baada ya mahojiano hayo ya moja kwa moja, mtangazaji Oga Obinna alichukua hatua ya kumfikishia ujumbe huo kwa aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, ambaye ameahidi kuingilia kati na kusaidia kutatua suala hilo.

Sonko ameahidi kuwasiliana moja kwa moja na Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti ili kuhakikisha mchekeshaji huyo anapokea malipo yake kwa huduma alizotoa kwa serikali ya kaunti.

Hatua ya Sonko imepongezwa na mashabiki mitandaoni, wengi wakimtaka Gavana wa Machakos kuchukua hatua za haraka kumaliza tatizo hilo ambalo limeonekana kumlemea Kioko kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *