Sofiya Nzau Aongoza Orodha ya Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube Kenya 2025

Sofiya Nzau Aongoza Orodha ya Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube Kenya 2025

Mwanamuziki Sofiya Nzau ametajwa rasmi kuwa msanii wa kike anayetazamwa zaidi kwenye YouTube nchini Kenya kwa mwaka 2025, baada ya kurekodi jumla ya tazamo milioni 147 katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita. Huu ni ushahidi wa kupaa kwake kimataifa, kunakochochewa na umaarufu wa nyimbo zake za Afro electronic ambazo zimevuma duniani kote na kumweka mbali zaidi ya wasanii wenzake. Katika nafasi ya pili amefuata Dr Sarah K, akiwa na milioni 31.8 za watazamaji. Mafanikio yake yanaakisi uthabiti na mvuto wa nyimbo zake za injili ambazo zinaendelea kutikisa ndani na nje ya nchi. Vicky Brilliance anashikilia nafasi ya tatu kupitia milioni 28.4 za watazamaji, akiendeleza rekodi yake thabiti kama mmoja wa sauti zinazotazamwa zaidi katika muziki wa injili. Takwimu hizi pia zinaonyesha nguvu ya wasanii wengine wa kike walioendelea kufanya vizuri mwaka huu. Shiro wa GP amesajili takriban milioni 23.1 za watazamaji, akifuatiwa kwa karibu na Ssaru ambaye amevuka milioni 22.3, ikiwa ni ishara ya kukua kwa muziki wa Gengetone na rap miongoni mwa wasanii wa kike. Nadia Mukami naye amefanikiwa kuvutia milioni 21.5, akidumisha nafasi yake kama mmoja wa waimbaji wakubwa wa pop nchini. Dyana Cods, ambaye anaendelea kukua kwa kasi katika tasnia, amefikisha milioni 19.6 za watazamaji, wakati Nikita Kering’ amesajili milioni 8, na Maandy akifunga orodha kwa takriban milioni 6.38. Kwa ujumla, takwimu hizi zinaonyesha wazi mabadiliko ya nguvu katika muziki wa kike nchini Kenya, huku wasanii wa aina tofauti wakivuka mipaka na kuendelea kuongeza ushawishi wao kwenye soko la kimataifa. Sofiya Nzau ameweka rekodi mpya, na mafanikio yake yanaashiria enzi mpya kwa wasanii wa kike katika majukwaa ya kidijitali.

Read More
 Mwimbaji wa Kenya Sofiya Nzau Ashirikishwa kwenye Soundtrack ya EA Sports FC 2026

Mwimbaji wa Kenya Sofiya Nzau Ashirikishwa kwenye Soundtrack ya EA Sports FC 2026

Mwimbaji maarufu wa Kenya, Sofiya Nzau, amefanikisha hatua kubwa katika taaluma yake ya muziki baada ya kuhusishwa kwenye soundtrack rasmi ya mchezo wa video wa EA Sports FC 2026. Kampuni ya EA Sports ni kampuni kubwa ya michezo ya video inayojulikana kwa kutengeneza michezo maarufu kama FIFA, NBA, na Madden NFL. Sasa, wimbo wa Sofiya utasikika na mamilioni ya watu duniani kote wanapokuwa wakifuatilia michezo hiyo. Kujumuishwa kwa Sofiya Nzau kwenye soundtrack ya EA Sports FC 2026 inaonyesha jinsi wasanii wa Afrika wanavyopata fursa kubwa kwenye majukwaa ya kimataifa ya michezo na burudani. Mashabiki na wapenzi wa muziki sasa wanaweza kufurahia kazi yake huku wakiwa sehemu ya mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote. Hii ni hatua muhimu kwa Sofiya, ikimshirikisha katika fursa zaidi za kimataifa na kuongeza umaarufu wake katika sekta ya muziki na michezo ya video.

Read More
 Sofiya Nzau Aweka Historia, Aingia Orodha ya Mastaa 10 Bora Barani Afrika Spotify

Sofiya Nzau Aweka Historia, Aingia Orodha ya Mastaa 10 Bora Barani Afrika Spotify

Mwanamuziki wa Kenya Sofiya Nzau sasa amejiweka katika ramani ya muziki barani Afrika baada ya kutajwa miongoni mwa mastaa wakubwa zaidi wa muziki katika bara hili. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, Sofiya ameshika nafasi ya 9 akiwa na wasikilizaji zaidi ya milioni 10.5 kila mwezi kwenye jukwaa la Spotify. Hatua hii inamweka katika daraja moja na majina makubwa kutoka Nigeria na Afrika Kusini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitawala tasnia ya muziki Afrika. Kile kinachofanya mafanikio yake kuwa ya kipekee ni kwamba yeye ndiye msanii pekee kutoka Kenya na Ukanda wa Afrika Mashariki aliyeingia kwenye orodha ya wasanii 10 bora, jambo linaloashiria ukubwa wa mvuto wa muziki wake kimataifa. Mashabiki na wadau wa muziki nchini wamelipokea jambo hili kwa fahari, wakisema kuwa hatua ya Sofiya ni ushahidi kuwa wasanii wa Kenya wana uwezo wa kushindana katika jukwaa la kimataifa endapo watawekeza katika ubora na usambazaji wa kazi zao. Mafanikio haya yanamuweka Sofiya Nzau katika nafasi ya kuendelea kupeperusha bendera ya Kenya na Afrika Mashariki kimataifa, huku mashabiki wakisubiri kuona hatua zake zinazofuata kwenye safari yake ya muziki.

Read More