Tunisia yatupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia 2022

Tunisia yatupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia 2022

Timu ya Taifa ya Tunisia imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia licha ya kupata ushindi wa 1-0 mbele ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye mchezo wa mwisho wa kundi D Alama 4 za Tunisia hazikutosha kuwavusha katika hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya Australia kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Denmark katika mchezo mwingine wa kundi hilo na kuzima ndoto za Waafrika kushuhudia wawakilishi wao wengine wakifuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya mchezo wa kandanda Duniani baada ya Senegal kutangulia katika hatua hiyo hapo Novemba 30. Matokeo hayo yameifanya Tunisia kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo nyuma ya Australia na Ufaransa aliyeongoza na alama 6.

Read More
 MWAMUZI WA MCHEZO WA TUNISIA NA MALI AZUA UTATA UWANJANI

MWAMUZI WA MCHEZO WA TUNISIA NA MALI AZUA UTATA UWANJANI

Hali ya sintofahamu imezuka baada ya mwamuzi Janny Sikazwe kutoka nchini Zambia kumaliza mpira kabla ya wakati kwenye mchezo wa Kundi F kati ya Tunisia dhidi ya Mali. Katika dakika ya 85 mwamuzi Janny alipuliza kipyenga kuashiria kumalizika kwa mchezo huo lakini baada ya vuta ni kuvute alibadili mawazo na kurejesha mchezo, lakini katika hali isiyo ya kawaida Janny Sikazwe alimaliza mpira tena katika dakika 89 na sekunde 43. Hata licha ya kuvutana na viongozi wa timu ya Taifa ya Tunisia, Janny Sikazwe aliendelea kushikilia maamuzi yake na mechi hiyo ikamalizika kwa Mali kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Tunisia

Read More