Vera Sidika Awaziba Midomo Wambea kwa Video Mpya Akila Bata Dubai Baada Kudaiwa Kufilisika Kiuchumi
Socialite kutoka Kenya, Vera Sidika, ameamua kuwajibu watesi wake baada ya kuzuka kwa madai kuwa ameshindwa kulipa kodi ya nyumba yake ya kifahari (mansion) na kulazimika kuondoka. Kupitia video aliyochapisha akiwa Dubai, Vera ameonekana akila bata, akifurahia maisha ya kifahari na mazingira ya kuvutia, hatua ambayo wengi wameitafsiri kama ujumbe mzito kwa waliokuwa wakimshambulia mitandaoni. Video hiyo imewaacha wengi midomo wazi, ikionyesha kuwa bado anaendelea kuishi maisha ya kifahari licha ya tetesi zilizokuwa zikisambaa amefulia kiuchumi. Katika siku za karibuni, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walidai kuwa Vera alishindwa kulipa kodi ya mansion aliyokuwa akiishi na hivyo kuhamia kwenye makazi ya chini (Apartment). Hata hivyo, bila kuzungumza sana, mrembo huyo ameonekana kuchagua vitendo badala ya maneno, akionyesha wazi kuwa hana presha na madai hayo.
Read More