Socialite kutoka Kenya, Vera Sidika, amekanusha madai yanayotembea mitandaoni kuwa amefulia kiuchumi kiasi cha kushindwa kulipa kodi ya mansion aliyokuwa akiishi mwaka jana.
Kupitia Insta Story yake, Vera Sidika amepuuza kabisa madai hayo akisema ni uzushi mtupu. Mrembo huyo, amesema kwa zaidi ya miaka 13 sasa, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimuombea afeli kimaisha, jambo ambalo anadai halitawahi tokea hadi mwisho wa dunia.
Vera ameongeza kuwa hata ikitokea amefulia kiuchumi, hawezi kushusha hadhi yake kwa kuishi kwenye nyumba ya kupanga. Amedai ni heri alale ndani ya gari lake la kifahari aina ya Range Rover Voogue kuliko kuhamia kwenye nyumba ya kupanga.
Kauli ya Vera Sidika imekuja mara baada ya shabiki kuibua taarifa zilizoandikwa na blogu moja, zikidai kuwa Vera ameshindwa kulipa kodi ya nyumba yake ya kifahari (mansion) na kulazimika kuhamia kwenye apartment ya kupanga.