Willy Paul Afunguka Kujihusisha na Kiki Kabla ya Kuachia Nyimbo
Msanii wa muziki wa Kenya, Willy Paul, amefunguka hadharani baada ya kukosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kujihusisha na kiki au kuvutia umaarufu kabla ya kuachia kazi zake mpya. Kupitia Insta Story, Willy Paul ameeleza kuwa tabia hiyo ya kudhaniwa kuwa anafuata umaarufu ni sehemu ya mitazamo potofu ya baadhi ya mashabiki, na kwamba lengo lake ni kushirikiana na mashabiki wake na kuhakikisha nyimbo zake zinawafikia watu wengi. Mkali huyo wa Toto, ameongeza kuwa kutumia mitandao ya kijamii kuendesha mijadala au kuunganisha mashabiki siyo kutafuta kiki au clout bali ni mbinu ya kisasa ya kukuza muziki. Aidha, msanii huyo amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijitahidi kuunda uhusiano wa karibu na wapenzi wa muziki wake, huku akisisitiza kuwa kila hatua ya matangazo ya nyimbo yake ni kwa lengo la kushirikisha mashabiki na si kwa kujihusisha na umaarufu bandia. Kauli yake imekuja mara baada ya kushtumiwa na VJ Patelo kwa kukaidi makubaliano ya malipo baada ya video shoot, madai yaliyowafanya mashabiki kuhisi alitengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni kabla ya kuachia wimbo wake mpya Ijumaa wiki hii.
Read More