Msanii wa muziki nchini Kenya, Willy Paul, amejitokeza kufafanua kuhusu video ya zamani iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha akisema kwamba hatawahi kuoa.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Willy Paul amefafanua kuwa video hiyo ni ya kitambo, kabla hajaoa, na kwamba kwa sasa yuko kwenye ndoa halali na mke wake anayemuita my Ngunga. Ameonyesha kuchukizwa na jinsi mashabiki wanavyotumia video za zamani kuvuruga maisha yake ya sasa ya ndoa.
Msanii huyo amesisitiza kuwa anataka watu waheshimu ndoa yake na waache kutumia taarifa za zamani kumharibia jina. Aidha, ametumia fursa hiyo kueleza kuwa kwa sasa yuko katika kipindi kipya cha maisha kinachozingatia familia na kazi yake ya muziki.
Kauli yake imekuja mara baada ya video yake kusambaa mitandaoni akisema hana mpango wa kuoa, akisisitiza kuwa kiwango cha usaliti katika mahusiano ya sasa kimekuwa kikubwa mno, jambo linalomfanya asione sababu ya kuingia kwenye ndoa.